Archive Page

1. Wawezeshaji lazima wajilinganishe na maudhui, falsafa na mkakati wa Focus on the Family Familia (FOTF) – (Kuzingatia Familia).

Wawezeshaji wanatakiwa kufunzwa katika mtaala wa Hakuna Majuto® na kuidhinishwa

2. Wawezeshaji lazima wafuate msimamo wa sera ya FOTF kuhusu masuala yafuatayo:

2.1 Ngono Kabla ya Ndoa

  • Matendo ya kujamiiana kabla ya wakati yanaiharibu nafsi yako na nafsi za wengine.
  • Uharibifu unaoletwa na shughuli za ngono za vijana ni pamoja na madhara ya muda mrefu ya afya na ya mahusiano.
  • Shughuli za ngono na watu ambao hawajafunga ndoa ni hatari hata bila kujali ni nani uliyeshiriki naye.
  • Kutoshiriki ngono hadi ndoa ni chaguo lenye afya bora kwa kila mtu.

2.2 Utoaji mimba

  • Kwa mujibu wa thamani yetu ya msingi ya Utakatifu wa Maisha ya Mwanadamu: Tunaamini kwamba maisha ya mwanadamu ni ya thamani na umuhimu usio na kifani katika nyanja zake zote, ikiwa ni pamoja na watoto ambao hawajazaliwa, wazee, wajane, walemavu wa akili, wasiovutia, wenye changamoto za mwili na kila hali nyingine ambayo inaonyesha uhai wa binadamu kutoka mimba hadi kaburi.

2.3 Kuzuia mimba

  • Kuzuia mimba ni vyema kuagizwa kama njia ya uzazi iliyokubaliwa kwa pande zote mbili katika kuchelewesha kupata mimba ndani ya ndoa. Haipaswi kutambuliwa kama njia bora ya kuzuia mimba katika kushiriki ngono kabla ya ndoa. Kwa kifupi, sio uthibitisho wa asilimia 100 kama njia salama ya kuzuia mimba au magonjwa ya ngono, haswa katika kushiriki ngono kabla ya ndoa.

2.4 Kupiga punyeto

  • acronymn FOTF inaona upigaji punyeto kuwa hauna madhara kiasili isipokuwa iwe tabia ya kupita kiasi ambayo inaambatana na uraibu wa ponografia au inatumiwa tu kama njia ya kuridhisha utimilifu wa ngono. Kupiga punyeto kunaweza pia kuleta athari mbaya za kijamii kwani kunaweza kuchukua nafasi ya uhusiano mzuri na mtu wa jinsia tofauti kabla na baada ya ndoa

2.5 Ushoga na Ndoa za Jinsia Moja

  • Ushoga ni suala tata, ambalo kwa jumla, ni chaguo la mtindo wa maisha kujihusisha na uhusiano wa jinsia moja. Hakuna uthibitisho unaotegemeka na wa uhakika kwamba ushoga ni tabia mtu amezaliwa nayo au umepangwa wakati wa kuzaliwa (kijeni). Kuwasaidia na kuwaelewa wale wanaopambana na ushoga limebakia kuwa ni jambo la msingi linalotuletea wasiwasi.
  • Tunaamini kwamba ndoa inategemea ukweli wa kibiolojia kwamba uzazi unategemea mwanamume na mwanamke, na ukweli kwamba watoto wanahitaji mama na baba. Tunaamini kwamba ndoa ni msingi wa ustaarabu wote wa binadamu, na inawaleta pamoja wenzi wanaokamilishana kingono, katika uhusiano wa mke mmoja, ambapo wanaahidiana kuwa waaminifu kwa viapo vya kudumu na kutengwa.

3. Wawezeshaji hawapaswi kubinafsisha maudhui ya mazungumzo.

4. Ili kujiwakilisha wenyewe na FOTF (Zingatia Familia) vyema, wawezeshaji wanapaswa kuwa wamevalia vizuri ipasavyo na nadhifu.

Sifa 3 za mshirikishi mwenye ufanisi

Kushirikisha/Kujumuisha

Changamsha – utakuwa unazungumzia masuala ya kibinafsi. Tulia uwe muwazi - tumia hadithi na mifano yenye nguvu! Uweze kufikiria umri wa wasikilizaji wako, hatua ya maisha waliyopo:

Kwa vijana wadogo (Wanafunzi wa sekondari za chini)

Kwa vijana wakubwa (Wanafunzi wa sekondari za juu)

Ngazi ya chuo kikuu (Wanafunzi wa baada ya sekondari)

Mtazamo mwema

Mtazamo wako utakusaidia kuwashawishi na pia kuthibiti majibu utakayopata kutoka kwa hadhira.

Mawasiliano mwafaka

Sekunde 15 za kwanza za ufunguzi wako ni muhimu. Dhana ya wengi kwenye hadhira yako hujengwa wakati huu, kutokana na kile wanachokiona. Hivyo jinsi unavyosimama, kile ulichovalia na jinsi unavyotembea ni muhimu sana.

Mwasilishaji mzuri ni yule ambaye:

Pitia orodha hii tena na uweke alama kwenye hoja ambazo umefuza vyema kwa sasa. Zile ambazo hukuziwekea alama zishughulikie unapofunza kwenye warsha ijayo.

Kudumisha uchangamfu na mazingira ambayo kila mmoja anaweza kushiriki:

 Makosa 10 ya Mshirikishi

1. Maandalizi mabaya – kusahau nakala zako, mtaala au vifaa, kuchelewa n.k

2. Kumwaibisha mshiriki ili achekwe.

3. Kutozungumza na chumba kizima.

4. Kushindwa kuthibiti kikundi.

5. Kutumia muda mwingi kwa mada zisizohusiana.

6. Kufundisha bila kuwajumuisha ama kuwashirikisha washiriki.

7. Kukosa kuwashirikisha hadithi yako ama uzoefu wako.

8. Kutoangalia muda na kupitiliza muda uliowekwa.

9. Kutovaa kiheshima au ipasavyo.

10. Kukosa kufanya utathmini baada ya warsha kukamilika

Maswali ni ishara nzuri kuwa washiriki wamevutiwa na kile unachosema. Unapoyajibu, yajibu kana kwamba ni mazungumzo ya ana kwa ana, huku wengine kundi zima wakisikiliza.

Tarajia maswali. Jifunze jinsi ya kudhibiti vipindi vya maswali na majibu kwa urahisi na unyenyekevu. Tengeneza majibu yako ukitumia yale yaliyomo kwenye mwongozo ama mtaala huu ukikariri hoja zilizomo. Ukifanya mazoezi na kujiandaa vya kutosha unaweza ukajibu maswali mengi ambayo yataulizwa kwenye warsha. (ama kwenye mazungumzo na mwanao wa kike ama kiume).

“Neno lililosemwa wakati unaofaa ni kama matofaa ya dhahabu kwenye sahani ya fedha. Ni kama hereni ya dhahabu ama pambo la dhahabu safi ndivyo alivyo mwonyaji mwenye busara kwa sikio linalosikia.”
– Ancient Proverb

Mambo 11 muhimu ya kukumbuka

1. Hakuna maswali ya ujinga, ila tu majibu ya ujinga.

Majibu yako ya busara yatakabiliana na majibu ya ujinga ya vijana wanayoyasikia kutoka kwa vyombo vya habari, kutoka kwa vijana wenzao na vipindi vingine ambavyo si vya manufaa kwao.

Maswali ndio wakati wa maneno ya hekima, uponyaji na kuwatia moyo. Majibu yako kwa swali hayasikilizwi tu na yule aliyeuliza bali yanasikilizwa na wote wanaoshiriki. Maneno yana nguvu – kisaikolojia na pia kihisia. Yanaweza kufahamisha, kuumiza ama kuponya. Maneno yanaweza kuleta matumaini.

Washiriki wako wanaweza kuwa wanauliza jambo ambalo ni gumu kulielezea. Sikiliza kwa masikio, ubongo na moyo. Unaposikiliza kwa makini, chuja kila swali ili uweze kufikia kina cha suala hilo. Huu ni wakati wako wa kuwa mjumbe wa matumaini na uponyaji.

2. Sio maswali yote yanayohitaji majibu.

Mara nyingi kutakuwa na yamkini kijana mmoja kwenye kundi ambaye atakuwa akitaka kukujaribu. Swali hili mara nyingi ni la moja kwa moja na linaaibisha na hata huenda likafanya sura yako ikabadilika. Huenda aliyeuliza anataka washiriki wacheke. Swali pia linaweza kuelekea kwenye maudhui yenye ubishani au kukutaka ufichue maelezo yasiyofaa umri wa kundi hilo. Pumua kwa kirefu na usijibu mara moja mbele ya kundi lote. Badala yake chagua mojawapo ya majibu haya:

3. Sio maswali yote yanapaswa kujibiwa nawe

Waelekeze vijana kwa wazazi wao, walimu ama watu wazima wanaoaminika. Iwapo majibu yamo kwenye nyenzo ambazo tayari umezishughulikia au utazishughulikia, jaribu kulirejesha kwa vijana walijibu:

Iwapo kijana atakosea jibu , una nafasi nzuri ya kufundisha dhana hiyo tena.

4. Huhitaji kufahamu kila jibu la kila swali litakoloulizwa.

Usiwe na hofu ya kusema, “Sijui jawabu la swali hilo.” Iwapo ni sawa, nitaleta ama nitakujibu wakati mwingine tutakapokutana. Iwapo utaulizwa swali gumu, likubali, kisha pata jina la mtu aliyeuliza na uahidi kulijibu baadaye:

Unaweza ukaulizwa swali ambalo linasababisha kicheko. Huenda ukacheka hata wewe. Iwapo hujajiandaa unaweza ukasema hivi:

5. Tumia fursa hiyo kufundisha kanuni nzuri.

Chora taswira ama picha ambayo vijana watakumbuka. Maswali mengi yatatumika kutoa fursa ya kutafakari na kufundisha tena dhana hiyo. Tumia vifaa na miongozo ambazo tayari imeishafundishwa ili kuwasaidia vijana kuweza kusisitiza ukweli katika bongo zao.

6. Chukua muda wa kujibu swali kwa umakinifu.

Unapotaka kutumia maneno yaleyale, usiogope kutumia maandishi kwenye nakala yako ama mwongozo wa mkufunzi. Utakuwa unawafunza vijana kuwa unapotaka kupata jibu mwafaka na sahihi, unatafuta chanzo cha habari hizo.

7. Punguza idadi ya maswali utakayojibu.

Sema kitu kama, “Tuna muda wa maswali matatu.”

8. Hakikisha kuwa washiriki wanauliza maswali.

Muda mwingi unaweza ukatumiwa kutoa maoni, ambayo huenda yakawachanganya washiriki wengine. Iwapo hili litafanyika, taratibu ingilia kati na useme, “Samahani, lakini kwa sababu ya wakati, unaweza kufafanua swali lako, tafadhali?”

9. Use question cards (or Slido.com).

Waelekeze washiriki kuandika maswali wanapofikiria na kuyatumbukiza kwenye sanduku la maoni ambalo liko kwenye chumba. Tazama ndani ya sanduko hilo wakati wa mapumziko na uchague kati ya maswali yaliyomo kwenye sanduku ili uyajibu. Hii itamsaidia kijana mwoga na pia kumpa ujasiri yeye ambaye hataki kuuliza swali mbele ya wengine. Usiwatangaze wale ambao hawangependa kutambulika wakati wanapotaka kuuliza maswali kwa njia ya siri. Iwapo swali litaendelea kuulizwa na washiriki wengi, lijumuishe kwenye wasilisho lako.

10. Uliza maswali.

Uliza maswali ambayo huibuka kwenye warsha nyingine. Huenda washiriki wakawa na swali moja lakini wasiwe na ujasiri wa kuuliza mbele ya wengine.

11. Shirikisha yale ambayo ni ya manufaa na epuka yasiyofaa.

Shiriki tu kile kinachohitajika na kusaidia, haswa linapokuja suala la mada juu ya ujinsia. Unaposhiriki mfano au hadithi yako mwenyewe, toa maelezo ya kutosha ili kueleza jambo kuu na uepuke kutoa maelezo ambayo ni ya ziada, kwa mfano, maelezo ya picha ya ngono ambayo yanaweza kuibua udadisi wa vijana kwa njia isiyofaa au kuwasababishia usumbufu. Isipokuwa ukiulizwa, usitoe habari zaidi kuliko inavyohitajika. Na hata wakati kijana anataka kuchunguza zaidi, elekeza upya au urejeshe swali ikiwa unahisi litaingia katika maudhui yenye ubishi. Inapobidi, unaweza kueleza kuwa hutajibu swali kabisa au wakati wa warsha (rejea nukta 2).

LOG IN

Ishi Maisha Yako Bila Kuomba Msamaha