This section covers selected frequently asked questions by participants of No Apologies workshops. The answers provided are by no means exhaustive. Please refer to the list of recommended resources for a more in-depth study of the issues highlighted.
Kama sheria ya utu, unapokuwa katikati ya watu usiowapenda, ni muhimu kuwa mwungwana, sema machache, na usionyeshe ubaya na ufidhuli!
Lakini wasichana wanapojifanya kuwa waungwana kwa marafiki kisha wakawasengenya baadaye, wanaanza kupoteza kitu cha thamani-uhalisi. Kama ningekuwa wewe ningejiepusha na watu kama hao – wasichana ama wavulana!
Itakuwa vigumu kuwaamini na utagundua kuwa urafiki huo ni wa ndumilakuwili ama wa nazi kukutania chunguni.
Kwa hivyo basi ni kwa nini wasichana wengine hufanya hivyo? Inaelekea wasichana wana ufahamu zaidi na wanaeleza hisia zao, hasa ikiwa ni jambo ambalo hawalipendi. Ila wanaona haifai kumkabili mtu huyo. Sio kwamba vitendo hivi ni sawa, lakini kuelewa ni kwanini wanafanya hivyo kutasaidia kuwaonyesha neema.
Nitakuhimiza ama nitakutia moyo hivi: iwapo una marafiki ambao ni halisi na wa kweli, wahifadhi wadumishe. Ukweli usemwe, marafiki wa dhati sio rahisi kuwapata. Huchukua juhudi na unyenyekevu. Lakini utaridhika unapozeeka, kwani hawa ndio marafiki ambao ungependa kukabiliana na maisha nao pamoja na changamoto zake.
This section covers selected frequently asked questions by participants of No Apologies workshops. The answers provided are by no means exhaustive. Please refer to the list of recommended resources for a more in-depth study of the issues highlighted.
Iwapo unataka kumjua mtu kwa kuwa anakuvutia, si lazima kufahamu kama ana ugonjwa. Zaidi ya yote ni kutaka kufahamu yale anayoyapenda na anayoyachukia, tabia, ndoto na malengo yake. Hatua hii haifai mkishiriki ngono. Urafiki lazima ujengwe kwa misingi ya uaminifu na ukweli. Baadaye huenda mkazungumzia masuala ya afya, lakini sio lazima kwa urafiki.
Hata kama unafikiria kumwomba awe mpenzi wako na kumchumbia, uhusiano wenu haupashwi kushiriki ngono. Ni muhimu sana kwamba wote wawili mmejitolea kutoshiriki ngono – au matendo yanayoamsha uchu. Zingatia kukuza urafiki wenu na kumheshimu.
Wakati wote wawili mmejitoa na mnatarajia kufunga ndoa, huo ndio wakati mwafaka wa kushiriki kuhusu mahusiano yako ya awali pamoja na masuala yoyote ya afya.
Ikitumiwa kwa uangalifu na kwa madhumuni yanayofaa (yaani, kutafuta uhusiano mzuri wa muda mrefu ambao unaweza kusababisha ndoa na sio ya “kuunganisha tu”), basi programu na tovuti za kuchumbiana zinaweza kuwa za muhimu. Wanandoa wengi ambao wako kwenye ndoa zenye furaha na utulivu walikutana kupitia mitandao ya kutafuta mwenzi.
Kumbuka kwamba watumiaji wengi, walio kwenye programu za mitandao ya kutafuta mwenzi wanauwezekano wa kutoshiriki maadili yako. Pia ni muhimu kutambua kwamba programu na huduma zenyewe hutofautiana sana. Ukiamua kujihusisha na huduma za mtandaoni, tafuta zile zinazolenga kuunda mahusiano mazuri ya muda mrefu. Hizi nyingi hupatikana kupitia maswali ya kuuliza kufahamu wasifu wa mtu binafsi, utangamano, imani na maadili na kadhalika. Epuka programu ambazo zimeundwa kuwezesha kukutana na kuwa na uhusiano wa usiku mmoja tu.
This section covers selected frequently asked questions by participants of No Apologies workshops. The answers provided are by no means exhaustive. Please refer to the list of recommended resources for a more in-depth study of the issues highlighted.
Kamusi ya Merriam-Webster inafasili tamaa kuwa “tamaa kali au isiyozuilika ya ngono; unyonge.” Ufafanuzi huu pekee, unaozungumza juu ya hisia za ubinafsi isiyo na kifani, inapaswa kutumika kama onyo dhidi ya tamaa. Ni mbaya na inaharibu mahusiano ya binadamu.
Kumbuka kwamba kuvutiwa na mtu wa jinsia tofauti na wewe ni tofauti na tamaa. Mvuto wa kijinsia ambao ni sehemu ya ubinadamu wetu ni wa kawaida. Kuhisi mvuto kuelekea mwenzi wako ni jambo la kawaida na linapaswa kulindwa kwa uangalifu.
Zaidi ya mvuto huo wa kawaida, ni kuruhusu mawazo au maisha yako yatawaliwe na tamaa mbaya. Hata katika ndoa, ambapo tendo la ngono linafaa, tamaa haina nafasi. Uhusiano wa kimapenzi katika ndoa unahusu kujitoa, kujitolea, na kufurahiana. Sifa hizi ni kinyume na tamaa.
Kujaribiwa na tamaa ni jambo la kawaida sana; kujizuia ni fadhila. Ingawa upendo unaweza kuwa mwingi katika mahusiano kabla ya ndoa, na msisimko wa uchumba unaongezeka kadiri muda unavyopita, kujizuia kutaimarisha uhusiano wa kihisia hatimaye.
Ni vyema kuwa umejiwekea mwongozo wa lini unafikiria kuingia kwenye uhusiano. Na ninafurahi kuwa una hofu kuhusu jinsi ya kumkataa msichana ama mwanamume kiupole bila kumpatia matumaini ya uwongo. Hii inaonyesha ukomavu na kujitolea kwa malengo yako.
Kuwa na hisia kwa mtu wa jinsia tofauti ni jambo la kawaida na hupashwi kuwa na hofu. Hisia hizo zinapojitokeza zikubali, lakini si lazima kuzitekeleza hisia hizo na kujitosa kwenye uhusiano. Ama tazama hivi, kuwa na malengo kutakusaidia kupata mtu anayeelekea kwenye barabara sawa nawe. Baada ya kusema hayo, yafuatayo ni baadhi ya mapendekezo ya jinsi ya kuwa na urafiki na mtu wa jinsia tofauti
This section covers selected frequently asked questions by participants of No Apologies workshops. The answers provided are by no means exhaustive. Please refer to the list of recommended resources for a more in-depth study of the issues highlighted.
Kupiga punyeto ni kitendo ambacho mtu hutafuta kujiridhisha kwa kugusagusa ama kutomasa tomasa sehemu zake za siri kwa madhumuni ya kupata raha ya ngono.
Tuanze kwa uhalisia wa mambo,
This section covers selected frequently asked questions by participants of No Apologies workshops. The answers provided are by no means exhaustive. Please refer to the list of recommended resources for a more in-depth study of the issues highlighted.
Ni jambo la kusikitisha, kwamba mambo haramu ya ngono yameenea sana katika ulimwengu wetu hivi kwamba taraja la kuyaepuka linaonekana kuwa jambo gumu sana. Hata hivyo, kuna baadhi ya hatua za vitendo unazoweza kuchukua ili kuwa na mawazo chanya katika nyanja hii.
Ya kwanza ni kuunda urafiki mzuri na watu wa jinsia moja ambao wanaweza kukusaidia kuwajibika, na ambao unaweza kuwahimiza katika kufuatilia usafi. Mahali pazuri pa kuanzia patakuwa marafiki wa jinsia moja ambao wameshiriki nawe katika mpango wa Hakuna Majuto. Kuna nguvu katika idadi, ukijua kwamba kuna marafiki wenye nia moja na wewe kwenye safari hii kutaleta tofauti kubwa.
Unaweza pia kuchunguza programu ya kuchuja kwa kompyuta yako nyumbani au programu ya simu yako. Programu hizi si kamilifu, lakini zinaweza kukusaidia kuchuja ponografia na maudhui mengine haramu. Na tena, ikiwa una marafiki wenye nia moja ambao wanatumia programu sawa, programu nyingi zina kipengele cha uwajibikaji ambacho kitawawezesha kutiana moyo katika kufuata usafi wa ngono.
Hata kama utakosa nyakati fulani—kama sisi sote—kuwa na uhakika kwamba inafaa kujitahidi kujitolea tena kufuata usafi wa kingono na kuchukua hatua kuufanikisha. Iwe hujaoa au umeolewa, ukikuta unakabiliwa na kushindwa mara kwa mara katika uwanja huu, kama vile uraibu wa ponografia, tunakuhimiza umtafute mshauri aliyehitimu au mshauri wa kidini ili kukusaidia kushughulikia suala hilo.
Ikiwa unataka kujiandaa kwa ajili ya maisha ya ngono yenye afya, yenye kuboresha ngono unapokuwa kwenye ndoa, ponografia ni mahali pa mwisho kabisa unapotaka kutazama. Utafiti thabiti umetoa ukweli wa kimsingi kuhusu ponografia, kama ifuatavyo:
Dk Mary Anne Layden, mtaalamu wa magonjwa ya akili na mkurugenzi wa elimu katika Kituo cha Tiba ya Utambuzi katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania alisema:
“Ujumbe wa ponografia ya mtandao ni sumu ya kisaikolojia, si ya kweli, ni ngumu kutengua na inaundwa na watu ambao malengo yao ni kupata pesa bila kujali matokeo”
Tuna deni kwa vijana wetu kuwapa kilicho bora zaidi, kuwalinda dhidi ya mabaya, na kutumia hekima, elimu na uzoefu wetu kufanya maamuzi mema.
Hatuungi mkono mtaala wowote wa elimu ya ngono unaohimiza utumizi wa ponografia au upigaji punyeto kama njia ya kukabiliana na tamaa za ngono.
Badala yake, elimu ya kutoshiriki ngono, ambayo hutoa matokeo ya juu zaidi ikilinganishwa na “elimu ya kina ya ngono,” inapaswa kuwa njia ambayo wanafunzi wanafundishwa kuhusu ujinsia shuleni. Hii inapaswa kuongezwa na maagizo yanayolingana na umri nyumbani.
Ndiyo, kutazama ponografia sikuzote ni kosa, ndani na nje ya vifungo vya ndoa. Inaharibu siri na maana ya ngono, inajenga matarajio ya uongo, na inakuza uharibifu wa kihisia na kisaikolojia kwa wanaume na wanawake. Sekta ya ponografia imefungamanishwa na biashara haramu ya binadamu na kwa asili yake inawanyonya wanawake. Wale wanaotumia ponografia, hata ikiwa ni “bure,” wanaunga mkono kwa njia isiyo ya moja kwa moja tasnia hii mbovu. Kwa kupendekeza kuleta ponografia kwenye chumba chako cha kulala, kimsingi unamwambia mwenzi wako kwamba unataka kuwa na wapenzi wengi wa ngono kwa wakati mmoja. Kuna njia chanya za kuongeza maisha yako ya ngono katika ndoa, lakini ponografia sio mojawapo.
This section covers selected frequently asked questions by participants of No Apologies workshops. The answers provided are by no means exhaustive. Please refer to the list of recommended resources for a more in-depth study of the issues highlighted.
Nafurahia kuwa umeamua kutoshiriki ngono hadi siku ya ndoa! Ni uamuzi bora kwa siku za baadaye. Wacha pia nikuhimize kwa kusema hivi: makosa sio mwisho.
Mwanzoni huenda isiwe rahisi, lakini unaweza ukafanya maamuzi madogo ambayo yatakusaidia kudumisha ahadi yako:
Inachukua tabia thabiti na uamuzi mkubwa kuishikilia ahadi mliyoweka kwenye mahusiano. Lakini siku ya harusi yako, ukiangalia nyuma utagundua thamani yake ni kubwa!
Kama wanadamu, wakati mwingine tunaanguka kwenye majaribu na tunafanya maamuzi yasiyo ya busara na makosa – makosa ambayo huenda yakawaumiza watu wengine na hata sisi wenyewe. Kushiriki ngono kabla ya ndoa kunaumiza mahusiano yetu yote ya siku za baadaye.
Iwapo unajisikia vibaya kwamba kuna uwezekano mwenzako alishiriki ngono hapo awali na marafiki zake wengine, mweleze hisia zako. Utakuwa na wasiwasi ikiwa ameambukizwa magonjwa ya zinaa kutokana na mahusiano ya ngono ya awali. Ikiwa haamini katika uchaguzi wa kutoshiriki ngono, ama anafikiri kuwa ngono kabla ya ndoa sio jambo kubwa, huenda ikawa vigumu na kukuletea maumivu ukiendelea na uhusiano huo.
Hata ikiwa mtu amekuwa na mahusiano ya ngono, huo sio mwisho – anaweza kuamua kutoshiriki ngono kuanzia sasa mpaka wakati wa ndoa. Ikiwa yupo tayari kuahidi kutoshiriki ngono tena, itakubidi uamue iwapo uko tayari kumpenda na kumkubali jinsi alivyo, na kusahau yaliyopita ili ujenge uhusiano mpya na mwema ambao utasababisha ndoa inayoridhisha baadaye.
Itakuwa changamoto sana kujenga uhusiano unaotegemea upendo wa kweli na wa kujitoa na mtu ambaye alikuwa ameisha shiriki ngono hapo awali. Kinachoweza kusaidia ni wote wawili kupata mwongozo na uwajibikaji kutoka kwa mtu mzima mnayemwamini..
This section covers selected frequently asked questions by participants of No Apologies workshops. The answers provided are by no means exhaustive. Please refer to the list of recommended resources for a more in-depth study of the issues highlighted.
Ukweli ni kwamba kufanya uamuzi wa kutoshiriki ngono mara moja tu hakutoshi. Unapashwa kufanya uamuzi huo mara kwa mara, kwa njia ndogo na kubwa pia. Nyakati fulani unapojaribiwa, inaweza isiwe rahisi, inahitaji tabia, kudhamiria, na kujithibiti ili kudumisha uamuzi wako.
Ili udumishe uamuzi wako wa kutoshiriki ngono, unafaa kumwambia mtu kuhusu maamuzi yako ili uwajibike. Mtu ambaye atakukumbusha kuendelea na uamuzi wako. Huyo mtu anafaa kukuzidi umri, anayeaminika kwa mfano mzazi, mwalimu, kiongozi ama mshauri. Hii inamaanisha utabidi kumwambia mtu huyu kuhusu maisha yako hasa mahusiano na jinsia tofauti. Faida ya kufanya hivyo ni kubwa sana na pia utatiwa moyo kujua kwamba hauko peke yako katika hilo.
Iwapo uko tayari kwenye mahusiano, amua usijingize kwenye hali ambazo unaweza kujaribiwa zaidi ya kile kiwango cha ‘maji kuzidi unga’. Hii inaitwa mwanzo wa kuamsha hisia za ngono, wakati ubongo wako unasita kufikiria na homoni zako zinatawala, na kuchangia kushiriki ngono haraka. Epuka kugusana na kutomasana kwani hivi vitendo vitakusukuma kwenye majaribu ya kushiriki ngono. Amua LEO, kwamba hautakuwa peke yako na mpenzi wako, pamoja wakati wanafamilia hawapo karibu, na pamoja naye chumbani wakati mlango umefungwa.
Hatimaye, uwe mwangalifu kwa kile unacholisha ubongo wako. Jiepushe na picha ama filamu ambazo zitaamsha tamaa. Leo picha za ngono zimesheheni kila mahali kwenye vyombo vya habari (magazeti, mitandao, filamu) na kwamba ni rahisi kuzizoea bila kujua zitaweza kuathiri uwezo wetu wa kuthamini mahusiano halisi.
Ni matumaini yangu kuwa mwongozo huu utakusaidia kufanya uamuzi wa kutoshiriki ngono hadi siku ya ndoa na kuwa utajitolea kusubiri hadi siku ya harusi yako.
Mojawapo ya sababu kuu za usafi wa kiadili kutopendwa na watu wengi ni kwa sababu vyombo vya habari na utamaduni maarufu huendeleza wazo potovu kwamba kujieleza bila kikomo ngono ndiyo ishara kuu ya “uhuru.” Hata hivyo, kwa kweli, ngono nje ya mipaka ya ndoa kati ya mwanamume na mwanamke huleta uonevu kwa njia ya hatia, aibu, na uwezekano wa kupata mimba isiyo na ndoa au maambukizi ya zinaa. Zaidi ya hayo, jamii inashindwa kuunga mkono na kuwatia moyo wale wanaolenga kuishi maisha safi, badala yake inahimiza kinyume chake - utamaduni ambao karibu kila kitu huenda kingono.
Ukweli ni kwamba kwa wale ambao hawajafunga ndoa, usafi wa kiadili huleta uhuru wa kweli - kutokana na matokeo ya kihisia ya ngono kabla ya ndoa, kutokana na magonjwa ya zinaa, na kutoka kwa mimba. Usafi hukupa fursa ya kufuata malengo ya maisha, kufuatiliwa jinsi ulivyo kama mtu na si kwa ngono tu, kupata urafiki wa kweli na mwenzi wako wa baadaye, kujiheshimu mwenyewe na wengine, na kuishi maisha yako kwa ukamilifu wake bila shida zisizo za lazima.
Mojawapo ya sababu kuu za usafi wa kiadili kutopendwa na watu wengi ni kwa sababu vyombo vya habari na utamaduni maarufu huendeleza wazo potovu kwamba kushiriki ngono bila mipaka ndiyo ishara kuu ya “uhuru.” Kinyume chake, na ukweli ni kuwa kushiriki ngono nje ya ndoa kati ya mwanamume na mwanamke huleta kunyanyaswa katika hali ya hatia, aibu, na uwezekano wa kupata mimba isiyo halali au maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Zaidi ya hayo, jamii inashindwa kuunga mkono na kuwatia moyo wale wanaolenga kuishi maisha safi, badala yake inatia moyo kinyume—utamaduni ambao unaunga mkono ngono ya nje ya ndoa.
Ukweli ni kwamba kwa wale ambao hawajafunga ndoa, usafi wa kiadili huleta uhuru wa kweli— hakuna hisia hasi ya moyo inayotokana na kushiriki ngono kabla ya ndoa, hakuna magonjwa ya zinaa, na hakuna mimba haramu.
Usafi hukupa fursa ya kufuata malengo yako ya maisha, kupendwa kwa jinsi ulivyo na si kwa ajili ya ngono tu, kuweza kushiriki urafiki wa kweli na mwenzi wako wa baadaye, kujiheshimu wewe mwenyewe na pia kuwaheshimu wengine, na kuishi maisha yako mpaka ukafikia kilele chake bila kujiletea shida zisizo za lazima.
Ndio, uko sahihi. Ngono na ndoa zinakwenda sambamba. Hii ni kwa sababu ngono ni uzoefu mkali wa kimwili unaojenga kuungana kati ya mwanamume na mwanamke. Muungano huu sio wa miili tu, ni wa hisia na wa kiroho pia! Ngono ni karama ambayo ina uwezo wa kuunganisha watu kwa maisha yao yote.
Lakini kama vile ngono inavyoweza kuunganisha watu wawili maishani mwao, inaweza pia kuharibu watu maishani mwao. Bila ya kujitoa kwenye ndoa inayodumu, hili tendo linaweza kuwa jinamizi kwa viwango mbali mbali. Katika kiwango cha kimwili, mimba za haramu na kuambukizwa kwa magonjwa ya zinaa. Katika kiwango cha hisia, hisia ya kwamba umetumiwa, kutojiamini, upweke, uchungu na wivu.
Wakati mwanaume na mwanamke wanapooana, wanaahidi kuwa waaminifu, kupendana bila masharti hadi kifo kiwatenganishe. Ahadi hii ndio inayojenga mazingira salama na kinga ya mipaka kwa mwanamume na mwanamke kujitoa kikamilifu (kimwili, kihisia na kiroho).
Hakuna mtu aliye na uhakika wa kuoa ama kuolewa katika siku zijazo. Lakini leo, unayo fursa ya kufanya uamuzi wa kuokoa ubikira wako kwa yule utakayefunga ndoa naye baadaye. Usidanganyike kufikiria kuwa kuna kitu unachokosa iwapo hushiriki ngono sasa, ama kwamba hutaoa au kuolewa kamwe, kwa hivyo shiriki ngono sasa. Usikubali majaribu yakushinde kuuza kilichobora kwa kile kilichobandia. Ninakuhakikishia kuwa kila dakika unayosubiri utagundua kuwa ni ya thamani kabisa!
This section covers selected frequently asked questions by participants of No Apologies workshops. The answers provided are by no means exhaustive. Please refer to the list of recommended resources for a more in-depth study of the issues highlighted.
Kwanza, tunaipongeza imani na uelewaji unaokuja na chaguo lako la kutoshiriki ngono kabla ya ndoa. Hili ni chaguo ambalo wewe na mwenzi wako wa baadaye hamtajutia kufanya na uwekezaji ambao huongeza sana nafasi zenu za kuwa na ndoa yenye afya baadaye.
Hata hivyo, tunashauri sana dhidi ya kulala kitanda kimoja na mpenzi wako hata bila nia ya kufanya ngono. Sababu ni rahisi: majaribu. Kukaribiana katika mazingira ya faragha bila watu wengine kuwa karibu wa kuwawajibisha nyote wawili, ni kichocheo cha makosa katika uamuzi. Usafi wa kijinsia kabla ya ndoa ni vigumu kuufikia hata bila kuwa kwenye nyumba moja, na hata kwa wale walio na azimio kubwa sana.
Watu wanaolala kwenye nyumba moja mara kwa mara wanaishia kuishi pamoja. Ikiwa wewe na rafiki yako wa kike mnaamini kwamba uhusiano wenu utafikia hatua ya ndoa, basi inafaa kukumbuka kuwa kuishi pamoja kabla ya ndoa kunasababisha uwezekano wa talaka wa asilimia 50-80. Kuishi na kulala mbalimbali kabla ya ndoa kunatoa tazamio bora la mafanikio ya ndoa.
Ikiwa kwa sasa mnaishi kwenye nyumba moja na mpenzi wako, basi tunakuhimiza utafute njia ya kuzungumza naye kuhusu jinsi mnavyoweza kuboresha mpangilio wenu wa kuishi. Ingawaje mabadiliko ya makazi yenu yanaweza kuonekana ni magumu, ni jambo sahihi la kufanya na litaleta ndoa yenye afya baadaye.
This section covers selected frequently asked questions by participants of No Apologies workshops. The answers provided are by no means exhaustive. Please refer to the list of recommended resources for a more in-depth study of the issues highlighted.
Tamaa ya urafiki wa kimapenzi wakati wa msimu wa useja inaeleweka. Mahusiano ya kimapenzi na ndoa yanaonekana kuahidi utimizo wa tamaa nyingi za kina: hitaji la kuonekana uko na umaalum kwa mtu mwingine, kutamani urafiki, na, linapofikia kwenye suala la ndoa, matarajio ya kushiriki ngono na hatimaye kupata watoto. Hisia zako ni za asili kabisa.
Hata hivyo, tunakutia moyo kutambua kwamba kuwa mseja huleta changamoto na fursa pia. Usifanye makosa ya kuamini kuwa uhusiano wa kimapenzi au ndoa ndio suluhisho la kutokuwa na furaha au hisia za kutoridhika. Kwa kweli, uhusiano wa kimapenzi mara nyingi unaweza kutatiza kazi ya ukuaji wa kibinafsi, na kuchanganyikiwa kwa hisia kukiletwa katika ndoa wakati fulani huongeza tu nguvu zake. Kuna mahitaji mengi katika maisha yetu ambayo mpenzi, rafiki wa kike/ kiume, au mwenzi wa maisha hawezi kamwe kutimiza. Ingawa useja si chaguo lako kwa wakati huu, tunasadiki kwamba unaweza kuutumia kwa manufaa yako kwa kukazia fikira ukuaji wako binafsi, kwa kuwekeza katika urafiki wa afya, na kwa kufanya kila jitihada kuwa mtu sahihi badala ya kutafuta mtu anayefaa.
Katika ulimwengu wetu uliojazwa na mambo ya ngono mengi, inaweza kuwa vigumu sana kwa waseja kutoshiriki ngono. Tunaelewa hali yako, lakini tunakuhimiza utumie uwezo mkubwa wa kujidhibiti wakati huu muhimu maishani mwako. Hakuna chanya kinachoweza kuja kutokana na kuafikiana katika eneo hili muhimu. Uzinzi wa kingono utahatarisha ukuaji wako wa kibinafsi na wa kiroho na unaweza kudhoofisha uhusiano wako wa ndoa ikiwa utahisi kuitwa kufanya hivyo baadaye.
Uzinzi na ponografia vitazuia tu uthabiti wako wa kihisia na kiroho. Badala ya “kukidhi” mahitaji yako, vitu hivi vitazidisha tu kuvunjika kwako kijinsia baada ya muda. Kujizuia kwako na kuchagua usafi vinaweza kuwa vigumu, lakini ni kitu cha thamani kubwa sana.
This section covers selected frequently asked questions by participants of No Apologies workshops. The answers provided are by no means exhaustive. Please refer to the list of recommended resources for a more in-depth study of the issues highlighted.
Baadhi ya mila za kidini na kitamaduni hushauri dhidi ya matumizi ya uzazi wa mpango. Tunaamini kwamba maisha yote ya mwanadamu yana thamani, na kwamba maisha huanza na utungisho wa mimba (muungano wa manii na yai). Kwa sababu hii, hatuamini kwamba ni makosa kuzuia kurutubishwa kwa kutumia aina fulani za uzazi wa mpango, lakini tunapinga njia yoyote ya inayojulikana kama udhibiti wa uzazi ambayo hufanya kazi kama kiondoa mimba (hufanya kazi baada ya kutungwa mimba, kwa kuzuia mimba kupandikizwa kwenye tumbo la uzazi, ambayo huondoa uhai wa mwanadamu).
Kwa wale walio kwenye ndoa na ambao wana maswali au wasiwasi kuhusu uzazi wa mpango, tunawashauri kumwona mshauri au kiongozi wa kiroho anayeaminika.
Katika hali nyingi, hakuna sababu kwamba upigaji punyeto wa pande zote mbili uchukuliwe kuwa ni mipaka kwa wenzi wa ndoa, mradi wenzi wote wawili wanakubaliana.
Tunaamini kuwa shughuli hii, pamoja na aina zingine za ngono bila kujamiiana halisi, zinaweza kuachwa kwa uamuzi wa wanandoa.
HATA hivyo, ni muhimu kwamba:
Kwa maoni zaidi kuhusu kujieleza kwa ngono katika ndoa, tunawahimiza wanandoa kutafuta ushauri wa mshauri wa ndoa anayeaminika au mshauri wa kiroho.
This section covers selected frequently asked questions by participants of No Apologies workshops. The answers provided are by no means exhaustive. Please refer to the list of recommended resources for a more in-depth study of the issues highlighted.
Tunasikitika sana kusikia juu ya uchungu uliopata ulipokulia kwenye nyumba iliyovunjika. Ikiwa hali yako ilibainishwa na matatizo makubwa na kutokuwepo kwa vielelezo imara vya wazazi, inaeleweka kwamba unahisi kukata tamaa kuhusu kuendeleza mzunguko huo wa kuvunjika kwa ndoa na familia yako ya baadaye.
Wakati huo huo, tunataka kukuhimiza kwa mawazo ya kwamba yapo matumaini! Historia imejaa wanaume na wanawake ambao walivumilia maisha magumu sana ya utotoni na bado waliweza kuanzisha uhusiano mzuri na familia thabiti wakiwa watu wazima. Kwa kweli, watu wengi wameshuhudia kwamba kukua katika nyumba ngumu kuliwafanya wajue tabia na mifumo mibaya ambayo inapaswa kuepukwa. Sasa ni wakati wa kuwekeza katika afya na utulivu kwa ajili ya mwenzi na watoto wako wa siku zijazo.
Ukweli kwamba umeshiriki katika mpango wa Hakuna Majuto® unaonyesha hamu yako ya kuwa mwenzi na mzazi mwenye afya ya kihisia na uhusiano katika siku zijazo.
Hata kama hali yako ya sasa ya nyumbani inabaki kuwa ngumu, tunakuhimiza kutafuta vyanzo vingine vya kukuhimiza na kukutia moyo. Kuna vitabu vingi, kozi na programu ambazo zinaweza kukusaidia na kukuandaa kwa ajili ya maisha ya ndoa na familia. Ikiwa wewe ni mshiriki wa mapokeo ya imani, viongozi wako wa kiroho na usharika wanaweza pia kuwa vyanzo vya kutia moyo na usaidizi.
Hatimaye, kumbuka kwamba maisha yako ya baadaye ya ndoa si lazima yawe makamilifu. Changamoto zitaonekana katika uhusiano na mwenzi wako na watoto hata chini ya hali bora na kamili. Lakini kwa imani, maazimio, na kuungwa mkono na marafiki, familia kubwa, na jumuiya ya waamini, kuna kila sababu ya kuamini kuwa una mategemeo ya wakati ujao mzuri kuhusu suala la ndoa na familia!
This section covers selected frequently asked questions by participants of No Apologies workshops. The answers provided are by no means exhaustive. Please refer to the list of recommended resources for a more in-depth study of the issues highlighted.
Jawabu ni ndio! Huwezi kufa usiposhiriki ngono. Iwapo huo ungekuwa ukweli, vijana wengi wangekuwa wamekufa sasa; na pia watu wazima wengi.
Jumbe nyingi huko nje zinatwambia kuwa kila mtu anashiriki ngono, na iwapo hufanyi hivyo umetupa mbao na hauko poa na kuna unachokosa. Lakini hiyo si kweli! Thamani ya mtu haikadiriwi na mara ngapi ameshiriki ngono.
Vyombo vya habari vinaweza kuonyesha kuwa ngono ni ya lazima, na kila mtu anashiriki. Hili si kweli. Sisi ni binadamu — wanadamu wenye uwezo wa kujithibiti na kufanya uamuzi. Iwapo tutachagua kutoshiriki ngono tunaweza kudumisha uamuzi huo. Na kwa hilo, tunaweza kujivunia kuwa tulishikilia kile tunachoamini, badala ya kufuata kile watu wengine walichosema.
Hapana. Si vibaya kufanya ngono na mwenzi wako wakati lengo si kuzaa.
Kuwa na watoto ni mojawapo ya zawadi na baraka kadhaa ambazo ngono hutoa. Watoto huleta furaha kwa familia na wao pia ni kizazi kijacho kitakachojali na kukidhi kizazi kilichopita. Nao ndio watakaozalisha, kuinua, kufundisha, kulinda na kukidhi kizazi kijacho. Zawadi nyingine muhimu ya ngono pia ni kufurahia, na inawaunganisha waume na wake kisaikolojia, kihisia, na kiroho hata wakati ujauzito sio lengo au matokeo.
This section covers selected frequently asked questions by participants of No Apologies workshops. The answers provided are by no means exhaustive. Please refer to the list of recommended resources for a more in-depth study of the issues highlighted.
Jambo la kwanza, nataka ufahamu kuwa hauko pekee. Kuchanganyikiwa kuhusu jinsia yako ni jambo la kawaida kwa vijana wengi.
Tulia kuwa baadhi ya hisia unazokabiliwa nazo ama maswali unayojiuliza — “Mimi ni nani?” “Ina maana gani kuwa mume ama mwanamke?”na “Nahisi vipi kuhusu watu wa jinsia tofauti?” — mara nyingi ni sehemu ya kawaida ya kukua. Kwa umri wako, hisia za ngono, hamu ya kuthibitishwa, kutaka kukubalika, kuidhinishwa na urafiki ni mambo ya kawaida.
Fahamu jambo jingine ambalo ni la kawaida? Kupata mtu wa jinsia moja, anapendeza na anavutia. Vijana na watu wazima huhisi hivi pia. Unaweza ukapenda hulka, sura na uwezo wa mtu. Aidha kwa kufikiria kuwa unapenda mtu wa jinsia sawa ama unapenda kukaa naye, haimanishi kuwa wewe ni basha! Usijipe jina kuwa wewe ni basha ama mlawiti.
Uwe mwangalifu sana na watu wa jinsia sawa ambao huonekana kufurahia kuvutiwa na wewe na kukuhimiza kutenda kulingana na tamaa za watu wa jinsia moja. Huenda wanakabiliwa na mseto hisia na litakuwa jambo la busara kupunguza mahusiano nao.
Elewa kuwa kung’angana na hali ya kuvutiwa na watu wa jinsia moja ama kujaribiwa sio makosa. Lakini kukubali hisia hizi zikutawale si sawa. “Basha” haielezei ni mtu gani. Badala yake, ni neno la kisiasa ambalo linaloelezea utambulisho, upendeleo, na mtindo wa maisha mtu aliyouchagua. Licha ya yale ambayo huenda umeyasikia, wanaume na wanawake hawakuzaliwa mabasha ama wasagaji.
Baada ya miaka 10 ya mjadala kuhusu ubasha, utafiti uliofanywa mwaka 2008, American Psychological Association (APA) unaafiki kuwa ushahidi uliokusanywa hauungi mkono kuwa ubasha unasababishwa na chembe chembe za uzazi wa mtu. Badala yake, moja kati sababu ni mtagusano na jamii unaosababisha ubasha..46 Utafiti wa hivi majuzi uliofanywa na timu ya kimataifa ya watafiti, iliyoongozwa na Benjamin Neale wa Taasisi ya Broad ya Harvard na MIT pia ilihitimisha: hakuna jeni la kuwa shoga, na ingawa jeni zinaonekana kuwa na jukumu katika kuamua mwelekeo wa kijinsia na tabia ya watu wa jinsia moja, ni ndogo, ngumu, na haibadilishi chochote.47
Kutafuta usaidizi ni hatua muhimu ya awali ambayo unafaa kuchukua. Usitaabike peke yako. Tunaweza tukakuelekeza kwa washauri ambao watakuwa tayari kukusikiza na kukusaidia.
Hii ni mada tata, lakini jibu fupi ni, hapana, si vibaya kuwa na mvuto wa jinsia moja. Lakini, kuendeleza kuchochea hisia hizo na kutafuta mahusiano ya kingono na watu wa jinsia moja ni tatizo. Ikiwa wewe au mtu unayemjua anapambana na hisia za kuvutiwa na watu wa jinsia moja, tunakuhimiza ujadili hali yako na mzazi au mshauri unayemwamini, au kiongozi wa kidini.
Hisia za mvuto wa jinsia moja kunaweza kuwa chanzo cha mvutano na maumivu makubwa; hata hivyo, kujisikia hatia sio jibu. Kuhisi jaribu la kuvutiwa na jinsia moja si dhambi, kwa kuwa sisi sote tunajaribiwa kila siku. Kupinga vishawishi ni vyema, na wale wanaovutiwa na watu wa jinsia moja wanaweza kufanya hivyo kwa kutojihusisha na mahusiano hayo na kuwa waseja huku wakitafuta mwongozo.
Tunakuhimiza kuweka kipaumbele cha juu katika kuhifadhi na kudumisha uhusiano mzuri na watu wa LGBT maishani mwako. Ili kufanya hivyo, unahitaji kutafuta njia thabiti za kuelezea na kuonyesha upendo wako kwao. Lakini lazima utambue kwamba upendo na kibali sio kitu kimoja, ni vitu viwili tofauti.
Ingawa shinikizo la kusherehekea uhusiano wa jinsia moja linaweza kuonekana kuwa kubwa, ni muhimu kukumbuka kuwa haya ni maendeleo ya hivi majuzi. Kihistoria jamii zenye nguvu na thabiti zaidi ni zile ambazo hazijakumbatia uhusiano wa jinsia moja au wazo kwamba jinsia inaamuliwa na mtu binafsi.
Unaweza kuwasaidia marafiki na familia ya LGBT kwa hali na mali bila kuunga mkono ndoa za watu wa jinsia moja na mpito wa jinsia. Kuwepo na uangalifu wakati wa kukaribia mada hizi; ukiongoza kwa upendo mazungumzo haya, ukiheshimu kwamba kunaweza kukawapo tofauti ya maoni. Tunajua hili ni somo gumu na la kibinafsi. Hapa tena, tungekuhimiza kutafuta mwongozo wa ziada kutoka kwa mzazi, mshauri au kiongozi wa kidini.
Kuna maswala mbalimbali ambayo yanaweza kusababisha mtu kupata kuvutiwa na jinsia moja. Kama vile mwandishi mmoja alivyobaini, “Ushoga huenda unatokana na mambo mengi . . . utu, mahusiano, kiwewe, masuala ya maendeleo, na athari za kitamaduni.” Kwa hivyo, madai ya kwamba mtu “hajachagua” kuwa sehemu ya jumuiya ya LGBT yanaweza kuwa ya kweli.
Hata hivyo, mvuto wa watu wa jinsia moja unaonekana kuathiriwa kimazingira zaidi ya mwelekeo wowote wa kijeni. Tafiti hazionyeshi kwamba mapacha wote wanaofanana huvutiwa na jinsia moja ikiwa pacha mwenzao amevutiwa.48
Iwe ni rafiki au mwanafamilia anayevutiwa na wapenzi wa jinsia moja, tunakuomba uwasiliane na vyanzo vyenye taarifa nzuri unapomsaidia na kumshauri. Mtu huyu anaweza kuhisi kwa kweli kwamba huo sio mtindo wa maisha aliouchagua. Mtie moyo kwa mawazo kwamba hata kama vivutio havikuchaguliwa, kuna uwezo wa mabadiliko.
This section covers selected frequently asked questions by participants of No Apologies workshops. The answers provided are by no means exhaustive. Please refer to the list of recommended resources for a more in-depth study of the issues highlighted.
Kutuma ujumbe wa ngono hufafanuliwa kama kutuma ujumbe wa maandishi, picha au picha chafu kupitia simu za mkononi au mitandao ya kijamii. Tabia hii ni mwenendo unaokua kati ya vijana. Vijana wengi wanaona kutuma ujumbe wa ngono si kitu zaidi ya kutaniana kimapenzi kwa kutumia teknolojia ya juu. Wanafikiria kuwa, “Haina hatia. Simuumizi mtu yeyote.”
Hiyo si kweli. Vijana wengi wanayo mafikara yale yale ya cheza sasa, lipa baadaye, wanapotuma ujumbe wa ngono au wanapojishirikisha na matendo mengine ya ngono. Ikiwa unatuma au kupokea picha za uchi, itakugharimu na utaumia.
Moja ya kutuma ujumbe wa ngono ni kuhadharishwa hadharani. Uchunguzi unaonyesha kuwa wavulana wengi wanaopokea ujumbe wa ngono wanawashirikisha wengine. Unaweza kutuma picha kwa nia ya kwamba mpenzi wako tu ndiye atakayeiona, lakini kuna uwezekano ujumbe huo hautakuwa kwa macho yake pekee tu. Na picha zinapotoka, zinakaa mitandaoni daima na matokeo yanaweza kukuangamiza. Mwajiri wako wa baadaye anaweza kuziona. Wazazi wako wanaweza kuziona. Mwenzi wako wa ndoa au watoto wako wanaweza kuziona. Kwa hakika kuna mtu atakayeumia.
Imetolewa kutoka kwa McDowell, J. (2011) Ukweli Wazi (The Bare Facts) (uk. 88–89).
Tunasikitika kusikia kuhusu uonevu au unyanyasaji wowote unaoendelea unaokukabili. Bila kujali umri au asili, uonevu ni dharau kwa utu wa binadamu, na unaweza kuwa na madhara makubwa kwa wanaoathiriwa kwenye afya ya mwili na hisia zao. Kunyemelewa na aina nyingine zote za unyanyasaji- pamoja na za mtandaoni-kunaweza kusababisha viwango mbalimbali vya maumivu.
Ikiwa umeathiriwa kibinafsi na unyanyasaji, tafuta msaada! Hiyo inaweza ikawa inajumuisha wazazi, marafiki, viongozi wa imani au walimu wanaoaminika, itasaidia kukukumbusha kwamba wapo wengine wanaokujali na wanaotaka kukomesha unyanyasaji huo. Ikibidi, tumia sheria kushughulikia matukio mazito ya uonevu, pamoja na aina yoyote ya unyanyasaji na kuviziwa.
Ukiona dalili za uonevu kwa ndugu zako au marafiki, usisite kuwauliza kuhusu hilo, lakini uwe mwangalifu. Njia moja ya kuleta mada ngumu ni kuzungumzia kwa jumla. Kwa mfano, unaweza kutaja kwamba “baadhi ya watu” wamekabiliana na unyanyasaji. Unaweza kuzungumzia juu ya shida kama suala la ujumla.
Kisha, wakati nyote wawili mnaona urahisi wa kuliongelea, badilisha mazungumzo na kuyalenga kwake binafsi.
Uonevu unaweza kuwa na athari halisi, mbaya kwa mhasiriwa. Usisite kuwasiliana na mshauri aliyehitimu ikiwa unahisi inaweza kuwa na manufaa kwako au mtu unayemjali.
This section covers selected frequently asked questions by participants of No Apologies workshops. The answers provided are by no means exhaustive. Please refer to the list of recommended resources for a more in-depth study of the issues highlighted.
Jua kwanza kwamba unapendwa na unathaminiwa, na kwamba hata katikati ya kukata tamaa, kuna matumaini. Maisha yako yana makusudi hata kama sasa hivi hujisikii hivyo.
Unaweza kuzishinda hisia za kufa moyo na kutokuwa na matumaini, pamoja na mawazo ya kujiua pia. Una nguvu kuliko maumivu unayoyakabili. Unyogovu na kutaka kujiua ni hali ya kisaikolojia ambayo yapo matibabu yake.
Chochote unachofanya, usifanye makosa kujaribu kukabiliana na changamoto hii peke yako. Wasiliana na marafiki, familia, majirani na wanajamii wengine wanaoaminika. Tengeneza mtandao wa msaada. Wategemee na uwe wazi kuhusu kile unachohisi. Inaweza kuwa vigumu kwa wale walio karibu nawe kutambua ishara zinazowaonya kwa kile unachohisia, kwa hivyo ni muhimu kuwaleza kinagaubaga.
Ikiwa sasa hivi una mawazo ya kujiua, chukua hizi hatua nne muhimu zifuatazo mara moja:
Jipe moyo. Kuna matumaini kwa siku zilizo mbele yako!
If the participants have questions on topics which are not covered in No Apologies (such as LGBTQ or drug addiction), do encourage them to speak with their parents or seek professional advice from school counselors and doctors. They can contact the local Focus on the Family office for help or referrals.