Mwongozo huu utatumika pamoja na slaidi za uwasilishaji na kijitabu kilichotolewa na Focus on the Family. Mwongozo umeandaliwa kama ifuatavyo:
Kuna vitengo vinne katika mtaala wa Hakuna Majuto .
Kila kitengo kina moduli nne hadi tano. Kwa mfano, 2.1 inaonyesha Moduli ya 1 chini ya Kitengo cha 2.Kila moduli itaeleza malengo, usuli na mantiki yake.

Mazoezi ni sehemu za warsha zinazohusisha kushiriki. Kila shughuli inasema nyenzo/ vifaa inavyohitajika, pamoja na maelekezo ya jinsi ya kulitekeleza zoezi.

Klipu za video zinapendekezwa ili kuwashirikisha washiriki na kuonyesha hoja maalum. Ama filamu inayofaa au kiungo cha mtandaoni kitapendekezwa.

Aikoni hii inaonyesha kuwa maudhui yanaweza kupatikana katika slaidi zinazotolewa na Focus on the Family.

Aikoni inaonyesha kwamba washiriki wanapaswa kurejelea vitabu vyao vya mazoezi, kwa kawaida ama kukamilisha zoezi, au kusoma kwa habari zaidi. Hapa, nambari inaonyesha kwamba unapaswa kurejelea ukurasa wa 7.

Aikoni inaonyesha mada au maswali ya majadiliano ya kikundi kidogo (washiriki 4 hadi 6) ikiwa muda unaruhusu.

Aikoni inaonyesha maelekezo maalum kwa ajili ya mwezeshaji kuzingatia wakati wa ku kuelezea yaliyomo.

Aikoni inaonyesha mahali panapofaa kwa mwezeshaji kushiriki hadithi ya maisha halisi. Inaweza kuwa hadithi ya kibinafsi au akaunti ya mtu mwingine ya uzoefu wake. Kwa kawaida hadithi ya mfano hutolewa

Aikoni hii inaonyesha maudhui ya ziada ambayo mwezeshaji anaweza kutumia wakati wa warsha ikiwa ni yanafaa kiutamaduni.

Aikoni hii inaonyesha shughuli za ziada ambazo zinaweza kutumika kama zoezi la kupeleka nyumbani kwa washiriki au mahali ambapo zaidi ya saa nane zitatumika kwa warsha. Kwa kawaida, shughuli hizi zitahitaji muda zaidi.

Aikoni hii inaonyesha kuingia ndani zaidi katika mada. Wahimize washiriki kutumia muda zaidi wa kutafakari.

Aikoni hii inaonyesha Kwenda Nyumbani. Wahimize washiriki kujadili na wazazi wao kile walichojifunza. 7
Ili kuchangamsha washiriki jenga mazingira ya utulivu na ya furaha.
Wapatie fomu za kabla ya uchunguzi washiriki na uzikusanye wakisha zikamilisha. Wahimize washiriki kutoa majibu yao halisi kwa ajili ya swali hili, ““Ni wakati gani unaofaa kwa mtu kushiriki ngono, na kwa nini?” wahakikishie ya kwamba haitajulikana ni nani ametoa jibu gani. Sio lazima washiriki kuweka majina yao kwenye fomu. Uwaonyeshe kwamba maoni yao ya uaminifu yatakuwa msaada katika kufanya utafiti. Majibu yao yatakuwa kielelezo juu ya maoni ya washiriki.
Kijitabu cha mwanafunzi: Moja kwa kila mshiriki.
Kadi za maswali/maoni: Himiza washiriki kuandika maswali waliyo nayo kuhusu maisha, mapenzi ama ngono, kisha wayaweke maswali hayo kwenye kisandulu kilichowekwa kwa sababu ya warsha. Iwapo hawaoni uhuru maswali yao kujibiwa wakati wa warsha, waruhusu wakuachie anwani/namba za mawasiliano kwenye kadi ili uwasiliane nao kando.


Wachangamshe washiriki na uwatambulishe mada zitakazojadiliwa—Maisha, Mapenzi na Ngono.




Kama programu hii si ya kiingereza katika jamii yako, maneno kushoto na kulia yanaweza yasitafsiriwe vyema katika zoezi hili.

Carol hakujua ni jozi gani ya viatu vilivyolifaa kuvaliwa kwenye hafla hiyo. Viatu vyake vyeusi vya michezo ama vile visivyo na visigino? Alikuwa akienda kwa tamasha lamichezo na kundi la marafiki, na Nathan beki wa KULIA wa timu ya soka ambaye alimpenda sana, alikuwa awepo pia. Alitaka kuhakikisha kuwa atamvutia leo.
“Bor boooooooor!” Carol alipumua, akachukua viatu vya michezo na kukimbia nje ya nyumba kukutana na rafiki yake.
Kikundi chake kilipitia vituo mbalimbali vya michezo kilikuta bango lililosema, “Mechi ya Soka ya Mchanganyiko. Saa kumi jioni. Wachezaji sita kila timu. Jisajili KUSHOTO.” Kilikuwa na idadi iliyotosha hivyo kilijisajili. KULIA
Kikundi hicho kilikimbilia uwanjani na kuchukua nafasi zao. Katika kipindi cha kwanza walifungwa mabao matano kwa bila; timu hiyo nyingine ilikuwa inacheza mpira mchafu hasa jamaa mkubwa aliyekuwa KULIA. Katika kipindi cha pili kikundi hicho kiliwafikia wapinzani wake. Dakika mbili kabla ya mechi kuisha mabao yalikuwa 5 kwa 4.
Kikundi hicho kilikuwa na mpira wakati jamaa mnene alipomkimbiza Nathan ghafla kutoka KULIA. Nathan aligeresha KUSHOTO naye jamaa huyo mnene alimpita na kumkimbilia Carol. Alimwangukia na kumvunja mguu wake wa KULIA. Carol aliteguka kisigino chake cha KUSHOTO. Refa alipuliza filimbi kusimamisha mpira. Jamaa huyo mnene aliinuka akasonya na kutoweka uwanjani.
Nathan alikimbia alipokuwa Carol akamshika mkono wake wa KULIA na kumsaidia kuinuka. Polepole walichechemea pembeni ambako Nathan alimkalisha Carol chini. Baada ya kuhakikisha kuwa Carol yuko sawa alirejea uwanjani; hata kama hawangeweza kushinda hawakutaka kukata tamaa.
Huku zikisalia sekunde 90 mechi ilianza tena. Hiyo timu nyingine ilikuwa inacheza mpira mchafu zaidi ikiiumiza ile timu nyingine KUSHOTO na KULIA na hivyo walipoteza milki ya mpira. Baada ya bidii kubwa timu hiyo iliupata tena mpira. Nathan ndiye aliyekuwa na mpira na zikiwa zimesalia sekundi 12 na hakukuwa na mchezaji mwenzake aliyekuwa bila upinzani, aliendelea mbele, akielekea KULIA kwa uwanja.
Ghafla akakata KUSHOTO, akaifanya ya KULIA, akaifanya ya KUSHOTO, akageuka KULIA, kisha KULIA tena, akakata KUSHOTO, na hatimaye akaupiga mpira a akidhania umeingia wavuni.
Lakini uligonga mlingoti. Refa alipuliza filimbi mchezo ukaisha. Walikuwa wameshindwa.
Kwa vile Carol alikuwa ameumia kila mtu aliamua kwenda nyumbani. Wote waliingia kwenye gari lililokuwa KUSHOTO kwa lango la kuingilia, na kuendesha hadi machweo ya jua..



1. Kabla ya warsha, kata kamba moja (kwa kila mshiriki), yenye urefu wa sentimita 150 kutoka kwenye mpira wa kamba.
2. Funga kitanzi kinachoweza kubadilishwa kila mwisho wa kila kamba .
3. Angalia maagizo ya video ya jinsi ya kutenganisha-suluhisho la shughuli hii kama matayarisho.
4. Wakati wa warsha, toa kamba kwa kila mshiriki.
5. Waombe washiriki kutafuta mwenzao wa jinsia moja.
6. Waombe washiriki kuweka kitanzi kwenye ncha zote mbili za uzi na kuziweka kama pingu kwenye mikono yao.
7. Baada ya hayo, pamoja na mwenzao, mmoja wao atachukua kamba kutoka kwenye mkono mmoja, ipitishe kwenye kamba ya mwenzao na kuiweka tena kwenye mkono wake (angalia maagizo ya video).
8. Wajulishe washiriki kuna sheria 2 tu za zoezi hili:
9. Kwa sheria hizi 2, lengo lao ni kujikomboa kutoka kwa mwenzao . Wendelee kujikomboa hadi muziki utakaponyamaza. Anza!
10. Fafanua kwa kuuliza:



Wajulishe washiriki wazo sahihi la mapenzi na ngono.


1. Kabla ya semina, jaza hewa puto na uzibandike kote kote chumbani kwenye ubao mweupe au ukutani. Bandika kadi za “Hadithi au Ukweli?” kando ya kila puto.

2. Wakati wa warsha, weka slaidi ya “Wanachosema kuhusu mapenzi na ngono” na uelezee kikundi kwamba hizi ni baadhi ya kauli tunazozisikia kuhusu vijana, mapenzi na ngono.

Mwezeshaji achague sentensi zisizozidi nane zinazoakisi hadithi potofu zilizoenea katika jamii yako kutoka kwa taarifa iliyo hapa chini


3. Wape washiriki dakika 5 kuzunguka chumbani ili kusoma kadi. Iwapo wanafikiri kuwa kauli hiyo ni hadithi, wanapaswa kuweka kanda/kibandiko kwenye puto, ili “kupiga kura” ni puto gani ipasuliwe.
4. Muombe mtu ajijitolee kusimama karibu na kila puto na ampe kila mmoja sindano/pini.
5. Pitia kila oni lililoshikiliwa na watu wengi. Waulize waliopigia kura puto hiyo kupasuliwa watoe sababu zao. Inapothibitishwa kuwa maoni hayo ni hadithi, mwambie aliyejitolea kuipasua puto. Ambapo maoni ni ukweli, iache puto bila kuipasua.

Wawezeshaji watumie muda huu kueleza kwa ufupi kwa nini maoni hayo ni hadithi au ukweli, na kutaja kwamba itajadiliwa katika warsha ujao. Hakuna haja ya kwenda kwa kina; Lengo la shughuli hii ni kuwasaidia washiriki kuanza kufikiria maoni yaliyoenea kuhusu mapenzi na ngono.

Mstari mwingine wa kawaida unaosikika kutoka kwa vijana ambao wamefanya ngono:

Lakini “Haitokei tu.” Ni wakati mipaka haikuwekwa kwa uwazi na vijana hawafikirii juu ya matokeo ya vitendo vyao ndipo wanajikuta wamenaswa katika hali zinazoathiri na jambo moja husababisha lingine.

Mtazamo mwingine wa kawaida ni mawazo ya “ mimi si wa kawaida”. Vijana wengi hufikiri kwamba hawahitaji kulichukulia kwa uzito suala la kushiriki ngono kabla ya ndoa bila kujua kwamba iwapo hawataamua mapema maadili na mipaka yao, watakumbwa.
Kitengo hiki kinasisitiza upekee na thamani ya kila mtu binafsi, umuhimu wa tabia njema zinazojenga mahusiano yenye afya na kukabili maisha ya baadaye kwa makusudi imara.
Dk. Juli Slattery katika kitabu chake, Ngono na Msichana Mseja (Sex and the Single Girl), alisema kwamba tumeumbwa wanaume na wanawake “tukiwa na maumbile ya kimwili na sifa za kibayokemikali za kijinsia.” Hii ina maana kwamba tunayo hamu ya urafiki wa karibu, uhusiano na furaha ya kimwili. Hivyo ndivyo tulivyo na tulivyoumbwa na si wakati tu tunaposhiriki ngono au tunapoolewa/kuoa. Matendo haya katika hali hizi huthibitisha jinsi tulivyoumbwa.
Ngono, ujinsia na urafiki wa karibu mara nyingi maneno haya yanatumiwa bila kutofautishwa katika utamaduni wetu. Hii inaleta matata katika kujadili mambo haya. Ujinsia wako ni zaidi ya tendo la kushiriki ngono. Hamu yako ya kuwa na urafiki wa karibu ni zaidi ya tamaa ya ngono. Kumbuka ufafanuzi huu ufuatao:
Ujinsia: Dhana pana inayojumuisha nyanja zote za jinsia ya mtu, hamu ya ngono, imani juu ya ngono na uzoefu wa ngono.
Urafiki wa karibu: Uhusiano wa karibu na wenye upendo kwa mtu unayemfahamu sana. Ukaribu unahusisha kujisikia uko salama na huyo mtu, kufahamiwa kwa kina naye na kujua siri za ndani baina yenu.
Ngono: Zoezi la kimwili ambalo mara nyingi ni pamoja na kujamiiana.
Tunaweza kuzingatia sana tendo la ngono (ambalo huonekana mara kwa mara kwenye vyombo vya habari) na kukosa picha kubwa ya ngono, ambayo inajumuisha mtu mzima na hamu yetu ya uhusiano wa kweli. Au tunaweza tu kuishi kwa baadhi ya miongozo na tukaepuka sababu ya kina ya ujinsia wetu, ambayo ni kujisikia tuko na usalama, kufahamiana kwa kina na kujuliana siri za ndani. Hebu tuanze safari hii ya kujitambua kwa kuelewa sisi ni nani na jinsi tulivyoumbwa ili tuwe na mahusiano ya kweli na yenye afya.
Kuwafahamisha washiriki kuwa wao ni watu wa kipekee, tofauti, wana mseto wa mambo yanayowajenga na thamani ya ndani, na kwamba wanafaa kuchukuliwa kwa uangalifu na heshima.
Kila kijana ni wa tofauti, wa kipekee na thamani ya ndani, anayepaswa kuchukuliwa kwa uangalifu na heshima. Kipindi hiki cha kubaleghe ama kuvunja ungo ni wakati ambapo maoni ya vijana wenzao huwa muhimu, vijana wanahitaji kusikia ujumbe huu “ wewe ni wa thamani” bila kujali ufanisi wa masomo, sura na hata mambo mengine.
Haijalishi ni jinsi gani vijana wanavyojiona, hawajakomaa, sio watu wazima na kwamba wangali wanakua katika sehemu zote, kiakili, kijamii, kihisia, kimwili, kiadili na kiroho. Mwanadamu ni mseto wa mambo mengi na kila mara anafaa kuzingatiwa hivyo – kwa ujumla na sio kwa sehemu. Uamuzi mkubwa wanaoufanya unaweza kuwaathiri katika kila sekta ama sehemu.
Hili linahusu hasa kwenye eneo la ngono, ambalo sio tu tendo la kimwili ama hisia tu. Uamuzi wa kushiriki ngono kabla ya ndoa unaweza kwenda kinyume cha malengo ya mtu ya elimu, viwango vya kibinafsi/maadili, maadili ya familia na uhusiano na marafiki. Mtu anaweza kuwa amekomaa kimwili lakini mchanga kwa maswali ya kijamii.


Washiriki wafahamu thamani ya upekee wa kila mtu.


Mapendekezo: iwapo washiriki hawajitolei, unaweza kuuliza mshiriki aliyepata maksi nyingi kuliko wote kwenye somo la hesabu au aliyezaliwa wa kwanza katika kundi.

1. Uliza, “Kisia uwezekano wa wewe kuzaliwa (kama wewe?

2. Uliza:

3. Je, wajua?

4. Sisitiza hoja hii kuwa uko wa kipekee – na hilo ni la muhimu. Hakuna mtu anayefanana na wewe. Waombe washiriki kumwambia mtu aliye karibu nao ‘wewe ni wa kipekee!’


Mwanadamu – mtu ni mseto wa mambo mengi.


1. Pata mtu mmoja wa kujitolea alale chini kwenye shuka kubwa la kitanda ama karatasi kubwa akiwa ameangalia juu na mtu mwingine achore nje ya mwili wake kwenye shuka hilo kwa kutumia kalamu ya rangi.
2. Akisha kamilisha, omba watu wawili wa kujitolea watakaloliinua shuka hilo ili kila mmoja alione.

3. Chora sehemu tano za mwanadamu kisha ufafanue kila moja.

4. Elezea washiriki kuwa kuna sehemu ya kiroho ambayo hatuwezi kuiona lakini imo ndani ya kila mmoja wetu. Ni hamu iliyopo ya ndani la kila mmoja wetu kuwa kuna mtu ama kitu kilicho juu zaidi yetu kuliko sisi wenyewe.
5. Waombe washiriki warudie vipengele vitano vya sehemu za mwanadamu bila kuangalia slaidi


Kila linalofanywa na sehemu moja ya mwili wako huathiri sehemu nyingine.


1. Hawa watu 5 wa kujitolea, wachague kibandiko watakachovalia kwenye shingo zao. Waombe wapige foleni wakiangalia kundi huku mikono yao imeunganishwa kwa mkazo. Eleza kuwa hiyo inamwakilisha binadamu.
2. Waambie watu 5 waliojitolea kuwa lazima waendelee kuunganishwa kwani wanachukuliwa kama mtu mmoja. Mnyororo hauwezi kukatika hata itokee nini.
3. Wapatie kundi mfano wa tukio na uwaulize ni sehemu gani ya binadamu ambayo inaathirika zaidi katika hali hii.
Matukio :

Badilisha matukio ili kuonyesha yale ambayo hutokea ama yameenea sana katika jumuiya yako.
4. Kwa kila tukio, omba mmoja wa watu 5 waliojitolea kupiga hatua 2 mbele ikiwa wanahisi kuwa kipengele chao ndicho kinachobainisha jibu. (Waombe waliojitolea kurejea kwenye nafasi yao ya awali kabla ya kuendelea na tukio lifuatalo). Kikundi kitagundua kuwa mnyonyoro wote wa binadamu unasonga kila mtu mmoja anaposonga mbele.

Kwa kuwa kipengele kimoja kinaonekana kuathirika zaidi ama kuhisi athari mara moja, haimaniishi kuwa sehemu zingine haziathiriwi.


Kwa sababu bongo zetu, “zingali zinakua” tukiwa vijana, ni muhimu tutafakari kabla ya kufanya maamuzi badala ya kutegemea tu hisia au tamaa zetu za kimwili..


Kinyume cha imani za muda mrefu kuwa ubongo hukamilika kukua mwisho wa umri wa utoto, utafiti unaonyesha kuwa vijana huingia awamu ya pili ya ubongo kukua wakati wa kuvunja ungo ama kubalahe [3]. Awamu hii ya ukuaji huongeza kiwango cha kufanya uamuzi wa ukomavu, udhibiti wa msukumo, huku ubongo ukihama hatua kwa hatua kutoka kituo cha mihemko (amygdala) hadi kwenye gamba la mbele la ubongo (kituo cha sababu na mantiki)[4]. Hii ina maana kuwa ubongo wa kijana haswa sehemu inayothibiti uamuzi inaendelea kukua. Kwa vijana wengi awamu hii ya ukuaji huishia katika miaka 20 na zaidi.[5]
Kila mtu hupitia awamu ama kipindi cha kukua kinachoitwa kubalehe ama kuvunja ungo kwa wasichana. Kwa wasichana, kipindi hiki hutokea kati ya umri wa miaka 10 hadi 12, lakini kwa wengine huanza mapema miaka 9; kwa wavulana, mchakato huo huanza baadaye, kati ya umri wa miaka 12 hadi 14. Katika kipindi hiki, mwili wa mtoto hupitia mabadiliko mbali mbali ili uwe mwili wa “mtu mzima”; wasichana hukua matiti na kuanza kupata hedhi, huku wavulana huanza kuwa na ndevu, nywele kwenye uso na mwili, sauti nzito, na sehemu zao za siri kuongezeka. Kwa vijana wengi mchakato huo hukamilika wakiwa na umri wa miaka 16; kwa wakati huo wanaweza kufanya kazi za watu wazima.


Unawezaje kujipa changamoto ya kukua katika kila moja ya maeneo haya? Taja baadhi ya mifano.


[Mifano inaweza kujumuisha: kusoma kitabu kisichoeleweka kwa urahisi na kuangalia
ndani zaidi, au kujadili mada na mtu fulani. Kuwa na mlo na watu walio nje ya “kikundi”
cha mtu, kudhibiti hasira ya mtu kwa kuhesabu hadi 10 wakati kawaida yake ni kulipuka, kutimiza ahadi ikiwa kuna tabia ya kuzivunja.]


Upekee wako ni zaidi ya kile chembechembe zako za msimbojeni-DNA zinavyokuelezea. Kwa kila sehemu andika jambo linalokuhusu na uone jinsi ulivyo wa kipekee.

Kuwapa washiriki moyo wa kuota ndoto, kuweka malengo ya baadaye na kutambua kile wanachohitaji kufanikisha malengo hayo.
Miaka ya ujana ni wakati wa kutafuta umuhimu wa maisha na kile maisha yatakachokupatia. Ni muhimu kwa vijana kufahamu malengo na ndoto zao na kile kitakachowagharimu kuzifanikisha. Sisi sote tuna ndoto, lakini kama hatuchukui hatua zozote zitasalia kuwa ndoto tu.
Kujifahamu kuwa wewe ni nani, jinsi unavyojifunza, nguvu zako, na vipaji vyako kutakusaidia kufika mbali katika kufanikisha malengo yako.
Jambo kuu ni kuyaandika malengo na ndoto zako kwenye daftari kisha kuchunguza jinsi unavyoweza kuzifanikisha kihalisi – hata kama ina maana kuchukua hatua moja kwa wakati mmoja kuelekea lengo lako. Kumshirikisha lengo hilo mtu mwengine na huyo mtu akakutia moyo wakatindoto yako inavyoendelea kuanza kutimilika mbele yako, utasikia furaha waisikiayo watu wenye mafanikio.
Vijana walio na mipango ya kuafikia ndoto zao – na wana watu wanaowaunga mkono kufanya hivyo - wana uwezekano mkubwa wa kuafikia ndoto zao badala ya kuhatarisha ndoto hizo kwa kujihusisha na kukidhi tamaa ya mwili ya muda mfupi.


Kuonyesha umuhimu wa kuweka malengo.
1. Andaa mapema bila ya ufahamu wa washiriki, sanduku tupu, lililowekwa kwenye kona moja ya chumba.
2. Mkabidhi kila mshiriki sehemu ya gazeti. Waambie kila mmoja wao, kurarua gazeti katika sehemu tatu kisha waikunje iwe mipira mitatu.
3. Waombe washiriki kuchukua mpira mmoja wa karatasi “na kuutupa baada ya kuhesabu hadi tatu”. Utatarajia kuona mipira ya karatasi ikitupwa pande tofuati.
4. Waombe washiriki kuchukua mpira wa pili na “kuutupa mbele baada ya kuhesabu hadi nambari tatu”.
5. Hatimaye, weka sanduku tupu mbele ya washiriki na uwaombe kuchukua mpira wa tatu na kuutupa ndani ya sanduku tupu baada ya kuhesabu hadi tatu.

Washirikishi hawapashwi kutoa maagizo zaidi ya yale yanayohitajika kutolewa. Mpira wa karatasi wa kwanza – tupa”, mpira wa pili – “tupa mbele”, mpira wa tatu – “tupa kwenye sanduku tupu”.

6. Waeleze washiriki kwamba kuwa na malengo ni sawa na kujua ni wapi pa kulenga mpira wa karatasi. Iwapo hawana malengo na hawana mpango wa kuyatimiza, huenda wasifanikiwe kupata kitu chochote mwishoni (kama mpira wa kwanza). Hata hivyo iwapo watachukua muda kuweka malengo yaliyo wazi wana uwezekano wa kuyafikia ama kuwa karibu na kuyafikia (mpira wa tatu).



Kuwasaidia washiriki kuanza kufikiria kuhusu siku zao za baadaye na kuanza kutekeleza mambo yatakayowafikisha wanapotaka.
1. Uliza:

2. Uliza washiriki ina maana gani kuwa na NDOTO KUBWA

3. Uliza washiriki maswali haya ili waweze kufikiria:

4. Uliza washirki kurejea kwenye vitabu vyao na kuandika kile ambacho wangependa kutimiza kwa wakati ujao. Vijana wengine huenda wakaogopa kuelezea ndoto zao kwa kuhofia kufanyiwa dhihaka ama mzaha.
5. Kuandika husadia kuhuisha ndoto zao mawazoni na pia kwenye mioyo yao. Himiza washiriki kuwa mahususi iwezekanavyo kuhusu malengo yao. Wape washiriki dakika 7 – 10 kuandika majibu yao wakianza na malengo ya kipindi cha muda mfupi (mwaka mmoja) na kuendelea hadi malengo ya muda mrefu (miaka 10) ukitoa mifano inayuhusu maisha yako ili kuwapa moyo. Cheza muziki wa mandharinyuma kwa sauti ya chini unaowatuliza washiriki.
Uliza maswali haya ili kuwasaidia washiriki kuzingatia athari za nje kwenye ndoto na malengo yao:
Kwa mfano msichana ambaye angependa kuwa tabibu wa mifugo ama mwalimu, akipata mimba shuleni itamrudisha nyuma ama kukatiza masomo yake na huenda asifanikishe ndoto yake.
6. Kwa mfano msichana ambaye angependa kuwa tabibu wa mifugo ama mwalimu, akipata mimba shuleni itamrudisha nyuma ama kukatiza masomo yake na huenda asifanikishe ndoto yake.

Zoezi hili linaweza likafanywa kwa makundi madogo au watu wawili huku kila mshiriki akitathmini malengo ya rafiki yake..



Wakati mwingine ni vigumu kufikiria malengo na ndoto kwa sababu vijana bado wako kwenye safari hii ya kujitambua. Orodha ya Maslahi ya Uholanzi itawasaidia kupima yale wanayoyapenda, kuchunguza kazi gani wanaipendelea na waifuatie, na kuzingatia mipango yao ya baadaye. Kujua maeneo yao wanayoyapenda kutawasaidia kufanya mpango sahihi. Wahimize kutumia zana hii. Inatoa ripoti ya kina ya maana ya alama zao, kile kitakachowasaidia kwenye kufanya maamuzi sahihi kuhusu kazi watakayoifanya.
Jua alama yako ya Maslahi ya NA na kiungo hiki cha tathmini.


Inaweza isiwe rahisi kufikia malengo yetu lakini inawezekana. Waombe washiriki waorodheshe vikwazo mahususi vya malengo yao kwenye vitabu vyao. Baada ya hapo, washiriki wanapaswa kuafikiana na vikwazo chini ya mojawapo ya kategoria tatu zinazopatikana katika kitabu chao cha mazoezi: Tabia Hatarishi, Kasoro za Tabia au Mazingira. Mifano ya vikwazo kwa malengo yao inaweza kuwa:
Kunywa pombe na kuendesha gari, ngono nje ya ndoa, kutumia dawa za kulevya, kuzagaa nje sana (bila kufanya kazi), kuingia kwenye mapigano, kuvuta sigara au kuvuta bangi.

Kukosa heshima, kukosa uaminifu, kutowajibika, ubinafsi, kutokuwa na fadhili, mvivu.
Matatizo ya afya ya muda mrefu, wazazi hawawezi kumudu “vitu vya ziada”—ni mahitaji ya kimsingi tu, mzazi akipoteza kazi, kuonewa shuleni, wazazi wakiachana.
Zoezi hili linafaa kufichua kuwa hali nyingi hazichangii vizuizi vingi. Ijapokuwa hali huwa hazizuiliki, tunaweza kuamua jinsi ya kukabiliana na hali hizo kwa mienendo yetu. Watu ambao wanaweza kuangalia kihalisi jinsi vikwazo vinavyoweza kuzuia ndoto zao, hujiandaa vizuri kubuni mipango mbadala na kuendelea kusonga mbele katika maisha yao.



Taja vitendo ambavyo unaweza ukachukua kusaidia kufanikisha malengo yako ya siku za baadaye. Mifano ni pamoja na kuepuka mahusiano ambayo yatakutatiza kufikia malengo yako, kufanya bidii kwenye masomo, kujitolea kufanya kazi kwenye jamii na kudumisha afya.
Kutafuta watu kadhaa wakusaidie (wazazi,marafiki, mtu mzima anayeamika, mchungaji wa vijana) ambao watakuhimiza kufikia ndoto na malengo yako. Andika majina ya watu hawa kwenye kitabu chako.
Washiriki watahakiki sifa ambazo zinajenga tabia nzuri na kuchunguza tabia zao wenyewe kwa kufanya mtihani.
Tabia sio kitu unachozaliwa nacho. Ni kitu unachokijenga. Mahusiano mema yanajengwa kwa misingi ya tabia njema kama vile heshima, uwajibikaji, uaminifu, fadhili na kujithibiti. Tabia njema inahitaji tu uamuzi kuwa nayo na sio vigumu. Tabia njema inasaidia kushinda changamoto na hata hali ambazo zinaweza kutuzuia kufanikisha ndoto na malengo yetu. Kimsingi tabia ndio kichocheo cha ufanisi wa mtu.


Kuwawezesha kuzitambua tabia zao wenyewe.
1. Waombe washiriki kuorodhesha tabia nyingi nzuri kuanzia herufi A, hadi herufi Z.

IKama hii program haiwasilishwi kwa lugha ya kiingereza basi washiriki na waorodheshe sifa 10 za tabia nzuri].

Mifano ya sifa za tabia nzuri:

2. Ili kusaidia washiriki kuanza kufikiri kuhusu tabia zao, uliza: Kwenye mizani ya sifa za tabia hizo uko wapi?
3. Wape washiriki dakika 10 kukamilisha mtihani wa tabia kwenye vitabu vyao Weka muziki mandharinyuma kujenga mazingira matulivu.
4. Cheza muziki wa kutuliza chinichini ili kuunda hali ya utulivu.
5. Wakikamilisha, washiriki waorodheshe viwango vya alama walizopata ili kukadiria tabia zao.
6. Waulize washiriki zipi zilikuwa sifa zao tatu kuu kisha uwaafiki.
7. Wasaidie washiriki kutathmini tabia zao tatu bora, uliza “Marafiki zako wanaweza kusema kuwa una hizo tabia?”
8. Waombe washiriki kuzingatia ni tabia gani ambayo wangependa kuboresha na kufanya tena huo mtihani baada ya miezi kadhaa ili waone kama wameimarika..
Kamilisha “Mtihani wa Urafiki” mtandaoni kwa kiungo hiki kiungo hiki cha tathmini.

KICHWA - KUFAHAMU mazuri
MOYO - KUHISI kilicho kizuri
MIKONO - Kutenda yaliyo mema


Pana haja kuwa na uwiano kwa kile tunachojua ni kizuri, hamu yetu ya kufanya mema (kujisikia vizuri) na kutenda mema.
K.m, tumefundishwa kuwa ni vyema kuwapa watu wakongwe ama wanawake wajawazito wakae kwenye viti ndani ya magari ya abiria ya umma. Huenda tukahisi vibaya kuwa mtu mkongwe ama mjamzito anasimama kwenye safari kwenye basi ama treni. Lakini kile kitakachothibitisha iwapo tuna tabia nzuri ni iwapo tutampatia kiti chetu.
Mazoea ni uwanja wa vita vya kila siku dhidi ya tabia. Fanya mazoea ya kutenda yale yanayoonyesha tabia njema kama vile, subira, heshima na fadhili, haitapita muda utafahamika kuwa mtu mwenye sifa hizo.



Washirikishi wajumuishe hadithi zao binafsi au za washindi wa jumuiya.


Sifa za tabia yako huonekana kwenye matendo yako. Fikiria jinsi ambavyo umeonyesha baadhi ya tabia hizo.
Tambua ama elezea sifa tatu kuu za tabia yako baada ya majaribu.
Jaribu kukumbuka matukio matatu yaliyopita ambapo ulionyesha ama kudhihirisha sifa hizo.
Piga picha ya watu waliokusanyika kwenye ibada ya mazishi yako. Ungependa watu hawa waseme nini kukuhusu wewe?
Kuwasaidia washiriki kuelewa umuhimu wa marafiki na jinsi wanavyoathiri uamuzi na matendo, halikadhalika kutambua sifa za urafiki wa kweli ili waweze kuchagua marafiki kwa hekima.
Kubalehe ama kuvunja ungo ni wakati muhimu ambapo shinikizo kutoka kwa marafiki huwa na athari kubwa kwa vijana.
Sote tunahitaji marafiki. Marafiki hushiriki wakati mzuri, hutusaidia kihisia kupitia wakati mbaya, hutusaidia kujua maeneo ya upungufu wetu na hutuhimiza kuimarika. Urafiki ni kiungo muhimu cha ustawi. Hutoa nafasi kwa vijana kujitambua, kujisikia kukubalika na kukuza hali ya kuhusika. Hata hivyo urafiki unaweza kukuletea uchungu mwingi.
Ni muhimu kutambua kuwa kuna shinikizo hasi ama mbaya na vilevile kuna zile nzuri. Vijana wanastahili kujifunza kutofautisha kati ya hizo mbili ili wafanye uamuzi bora katika maisha.


Kutafakari juu ya sifa za tabia zilizo kwenye ushawishi chanya.

1. Waulize washiriki kutazama orodha ya maelezo ya marafiki zao kwenye kitabu na 😠 kuchora iwapo wanadhani 🤩 kama rafiki mzuri.
2. Maelezo yanaelezea rafiki MBAYA, na J iwapo yanaelezea rafiki MZURI. Mwisho wa zoezi , soma vielelezi 12 kutoka kwenye orodha kamili na waombe washiriki majibu yao kwa kunyoosha mikono inapoeleze rafiki mzuri. Vinginevyo, unaweza kuwaomba washiriki kusimama, wakati inaelezea rafiki mzuri na kukaa wakati inaelezea rafiki mbaya.
Orodha ya vielelezi:

3. Uliza washiriki:

4. Shiriki kuhusu rafiki yako mwema na sababu gani unamchukulia hivyo.

Je, una marafiki wa kweli? Wataje.Ni nini huwafanya wawe marafiki wa kweli kwako?
Ninawezaje kujenga urafiki utakaodumu?
Kamilisha “Mtihani wa Urafiki” mtandaoni kwa kiungo hiki kiungo hiki cha tathmini.


Wa kijuu juu, Unaofahamu: Watu unaowajua kwa sura, lakini huwezi kushiriki nao nje ya shule
Kikundi Chako: Watu unaoshinda nao unahisi kuhusishwa nao.
Marafiki wa dhati: Watu unaowaita marafiki bora na wa milele (BFF)/ndugu wanajua kila kitu “kinachokuhusu”
Urafiki haujengeki tu kwa usiku mmoja. Kwa “viungo” sahihi, uhusiano unaweza kuhama kutoka kuwa wa kijuu juu hadi ukawa ule wa karibu-wa dhati.
Rafiki wa kweli ni yule ambaye hakufichi chochote na ni mkweli kwako na wewe ni mkweli kwake. Lakini kuwa na rafiki mwema kunaanza sisi tunapokuwa wema, hapo ndio urafiki mzuri unajengwa.


Tabia
Sifa bora za urafiki ni uaminifu na ukweli. Unafaa kuwa na athari nzuri kwa marafiki zako.
Uamuzi mwema
Unahitaji uamuzi mwema kutambua kati ya rafiki mzuri na yule mbaya na kujua namna ya kuhusiana nao ipasavyo.
Subira
Mahusiano mema huchukua muda na juhudi kujengeka. Urafiki unaopitia misukosuko ya maisha unakuwa na uthabiti.
Ujasiri
Unahitaji ujasiri kujenga marafiki na kukabiliana na kukataliwa na wengine. Wakati mwingine unahitaji ujasiri kuzungumzia mambo mabaya yanayohitaji kurekebishwa.

Kumbuka.Kumbuka mambo muhimu kuhusu rafiki zako kama vile, kile wanachopenda, wasichopenda, siku yao ya kuzaliwa n.k.
Usijifanye/Uwe mkweli.Kuna marafiki wa kijuu juu na kuna marafiki. Marafiki wana uhusiano mzito. Kuwa muwazi na rafiki yako-Usijifanye kuwa mzuri mbele yao, na huku nyuma unawasengenya.
Uwe mwelewaji.Msikilize rafiki yako hata kama mnagombana, kabla ya kuanza kujitetea. Jaribu kuangalia mambo kwa mtazamo wake. Siku zote kuna kutoa na kupokea katika urafiki.
Kuwa nyeti.Usijifkirie wewe tu wakati wote hata ukashindwa kutambua rafiki yako anapokuwa hajisikii vizuri au ni mgonjwa. Pia uwe mwangalifu sana mnapokuwa na maongezi yanayogusia hisia kama vile wapenzi wenu na hali za familia..
Usiwe kupe.Usimkwamilie rafiki yako masaa 24/ siku 7 kama kupe, mpatie rafiki muda wa kuwa peke yake na wewe upate kuwafahamu marafiki wengine.
Uwepo.Usiwe kupe, lakini pia usipotee kabisa. Mara kwa mara ili uonyeshe kwamba unawajali marafiki zako, waandikie ujumbe mfupi, shiriki nao kwa muda, hata wapatie zawadi. Tumia ujumbe wa simu ama barua pepe kama njia ya mwisho –kukutana uso kwa uso ni bora wakati wote. Tenga muda wa kuwa na rafiki yako wakati wa mema na wakati wa mabaya, hata kama ni wewe tu uliyebakia naye, kwa maana wakati huo ndipo anapokuhitaji zaidi.


Tambua wewe ni rafiki wa aina gani kwa kujibu maswali machache kuhusu urafiki. Nakili matokeo. Alama 40 inaonyesha kuwa wewe ni rafiki wa kweli katika hali zote. Alama kati ya 25 – 39 inaonyesha kuwa wewe ni rafiki mwema lakini kuna nafasi ya kuboresha zaidi. Alama kati ya 15 – 24 inapendekeza kuwa una kibarua cha kujifunza kuweka marafiki mbele kabla ya maslahi yako. Alama chini ya 15 inaonyesha kuwa una kibarua kikubwa zaidi cha kuboresha mbinu zako za urafiki.
Kamilisha “Mtihani wa Urafiki” mtandaoni kwa kiungo hiki kiungo hiki cha tathmini.


Kila mtu anataka kuhisi kuwa yumo kundini — yumo ndani. Unataka kuhisi unakubaliwa na watu wanaopenda mambo ambayo na wewe unayapenda. Kabla ya kufanya kitu, mara nyingi huwa tunajiuliza, “Marafiki zangu watafikiriaje?”

Shinikizo Chanya la Warika Lako:
Shinikizo Hasi la Warika Lako:

Shiriki hadithi za kweli ambazo vijana wanaathiriwa na marafiki kwa mfano:


Kuonyesha umuhimu wa kukumbatia maadili imara ya kibinafsi.
1. Mmoja wa waliojitolea asimame juu ya kiti na mwengine kando yake kwenye sakafu.
2. Waelezee kuwa yule aliye juu ya kiti anawakilisha mtu mwenye viwango vya juu kimaadili kama vile, mwaminifu, anayejali, mnyenyekevu, mwerevu, anayewajibika na yuko tayari kuwasaidia wenzake wakati wote. Upande mwingine yule aliye kando yake anawakilisha mtu mwenye viwango vya chini kimaadili, ambaye huwahimiza wenzake kushiriki vitendo vibaya wala hawaheshimu watu wengine.
3. Waambie waliojitolea kuwa ukihesabu hadi tatu, waanze kuvutana, yule aliye juu ya kiti aanze kumvuta mwenzake na yule aliye chini aanze kumvuta aliye kwenye kiti. Itakuwa rahisi kwa mshauri aliye chini kumvuta mwenzake aliye juu ya kiti.
4. Hii inaonyesha kuwa ni rahisi kuathiriwa na kundi baya, lakini inachukua juhudi kubwa kuwaathiri watu kufikia viwango vya juu.
Ni muhimu kuwa na malengo wazi na kuzungukwa na watu wataokusaidia kushika hivi viwango vya juu kimaadili. Mtu aliye weka viwango si rahisi kushawishiwa na shinikizo za marafiki.


Kuhimiza washiriki kuwa gurudumu la mabadiliko yanayohitajika. (Ushawishi Chanya).
1. Iandae mapema: Chupa mbili zilizojazwa nusu; moja ina maji, nyingine ina bleach.
2. Inua ile chupa yenye maji na uwaelezee washiriki kuwa chupa hiyo inawakilisha mtu asiye na viwango.
3. Ongeza tone la rangi nyekundu ya chakula kwenye chupa iliyo na maji nauitikise, ukielezea washiriki kuwa rangi ya chakula inawakilisha athari mbaya zinazomkabili kijana, km, shinikizo ya kushiriki ngono, kuvuta sigara, dawa za kulevya, pombe, kutoroka darasani, kutumia lugha chafu, nk. Iwapo mtu hajaweka viwango kuhusu mambo muhimu maishani, atakuwa kama maji yanayochukua rangi yoyote- ataathirika kwa urahisi.
4. Inua chupa yenye bleach kioevu lakini usifichulie washiriki kuwa imejazwa bleach kioevu badala ya maji. Waeleze washiriki kuwa chupa hii inawakilisha mtu aliyeweka viwango vya juu na malengo maishani. Ongeza tone la rangi nyekundu ya chakula kisha utikise chupa hiyo. Kioevu hicho hakitachukua rangi nyekundu. Hii inawakilisha mtu ambaye ana viwango vyake na kuwa hawezi kuathirika kwa urahisi.
5. Taratibu mwaga maji yaliyo na rangi nyekundu kwenye maji yaliyo kwenye chupa yenye bleach. Waombe washiriki waangalie jinsi maji ya rangi nyekundu hayawezi “kuchafua” “maji” safi. Waelezee kikundi kuwa mtu mwenye viwango anaweza kuhimili shinikizo la watu wa rika lake.
6. Mwishowe mimina chupa iliyo na bleach kwenye chupa yenye rangi nyekundu. Waeleze kwamba sio tu mtu mwenye viwango anaweza kuhimili shinikizo la rika, lakini pia anaweza kuathiri marafiki zake kwa uzuri. Wahimize washiriki wawe wale wanaowashawishi vyema wenzao na sio wale wanaoshawishika.

Badala ya kuathiriwa vibaya na wengine, unaweza kuwashawishi na kuwatia moyo wengine kufanya mambo mazuri na sahihi.

Mwezeshaji: Baadhi ya chapa za bleach hufanya kazi vizuri zaidi ya nyingine, hivyo mshirikishi anafaa afanye majaribio ama uchunguzi kabla ya majaribio yenyewe.


Kuonyesha jinsi ya kuhimili shinikizo la rika.
1. Kwenye vikundi vidogo, waombe washiriki wafikirie na kujadili hali tofauti hapo chini, kwa kutumia mbinu ya Ieleze. Iuze. Isogeze.

Kwenye vikundi vidogo, waombe washiriki wafikirie na kujadili hali tofauti hapo chini, kwa kutumia mbinu ya Ieleze. Iuze. Isogeze.

Badilisha hali ama taswira kuwakilisha mambo yanayofanyika kwenye kijiji ama jumuiya yako.

2. Viagize vikundi viigize matukio hayo na majibu wanayoyapendekeza.
Ni muhimu kwetu kufahamu mapema kile tutakachosema kwa mtu anayejaribu kutushinikiza kwenye hali mbaya. Kila kijana ana fursa ya kukubali au kukataa maoni ya umati. Inabidi kuwa jasiri kwenda kinyume na umati, hasa inapokuwa ni wewe pekee yako usiyekubaliana nao. Katika kujifunza mbinu za kukataa kuna hatua tatu za kukumbuka. Katika kila hatua, kuna mapendekezo kadhaa ya watu kuelezea hoja zao.
Ieleze: Sema “hapana” na uwaeleze ni kwa nini.

Iuze: Pendekeza njia mbadala..
Isogeze: Tekeleza mpango wako na uache mlango ukiwa wazi kwa yeyote kuingia.
Jambo la muhimu ni kushikilia mpango wako na usishawishike. Ondoka na usiangalie nyuma.
Kuwajulisha washiriki kuwa thamani yao haiamuliwi na kile wanachosema watu au jamii, bali kwamba wao ni watu binafsi.
Kujenga utambulisho wa kijana ni mchakato mrefu. Bila kujua, vijana wengi huacha wengine wawambie wao ni akina nani; wanaruhusu kile wengine wanachosema kuwaathiri taswira yao binafsi. Hivyo wengi huishia kujichukia na hata kujihisi kuwa hawafai kitu. – “sio warembo wa kutosha, hawana nguvu za kutosha, si werevu wa kutosha, sio maalumu, hawastahili”.
Vijana walio na taswira nzuri ya ubinafsi wao hawategemei kuthibitishwa na wenzao. Wanajiamini utambulisho wao na wana uwezo wa kujithibiti wanapokosolewa kuhusu thamani yao. Wana uwezo mkubwa wa kuendelea kushikilia maadili yao licha ya shinikizo za vijana wenzao na athari nyingine.


Kila kijana hupitia mchakato mgumu wa kujitambua.

1. Wasilisha “Fumbo la slaidi A” na washiriki wajaribu kulitatua.

2. Suluhisho:
3. Kupitia maisha ya ujana ni kama kufumbua fumbo. Kutaka kujua sisi ni akina nani na iwapo ni wazuri vya kutosha, mwanzoni inaonekana kama haiwezekani na inaonekaana kuwa ngumu na masuala tata. Hata hivyo kwa subira, uvumilivu na mipango makini ya hatua-kwahatua tunaweza kufaulu kutatua masuala tata tunavyoendelea kukua.


Mashaka juu ya uthamani wetu ni kawaida lakini hayatufafanui.

1. Weka slaidi ya “Je Unaweza ukatambua?”.

2. Mwisho wa zoezi, jumlisha alama zote na ufanye utafiti mdogo kuhusu majibu ya washiriki. Wahakikishie kuwa hawafai kuonyeshana majibu yao bali jumla ya sentensi zilizo wekewa alama.

Badilisha sentensi zifuatazo ili ziangazie mambo yanayofanyika sana katika jumuiya ama eneo lako.

3. Waeleze washiriki kuwa kila mtu katika kiwango fulani huhisi hivyo, haswa vijana, kwa sababu miili yao inapitia kipindi kikali cha mabadiliko. Lakini hisia hizi sio sawa na sio kweli.


Hisia kuwa sisi si bora vya kutosha inafananishwa na bonde lenye kina kirefu ambalo hutuingiza kwenye huzuni kila wakati..

Tunaanguka bondeni iwapo:
Sio makosa kutaka kuwa mtu mzuri ama kuwa na viwango vya juu, lakini tatizo huanza wakati tunapotaka “kuwafurahisha wengine”. Iwapo hatutaweza kukabili hali ya kushindwa, ni rahisi kuanguka ndani ya korongo la kukosa thamani.
Mfano:
Mbona ninahisi hivi?


Kwa sababu watu wengi huingia kwenye korongo la kukosa thamani, inaonekana kama kawaida ya kila kijana. Lakini, hii sio njia ya lazima ya kufikia utu uzima. Unaweza kuiepuka iwapo:

Utatambua kuwa hauko peke yako
Kabiliana na Matatizo yako
Fidia “udhaifu” wako
Kuwa na marafiki wa dhati


Kuwasaidia vijana kutiana moyo na kuthamini upekee wao.
1. Waagize wanafunzi kuunda vikundi vya watu 3-4
2. Waombe washiriki waandike kitia moyo kimoja kwa kila kategoria:


3. Waombe washiriki waandike kitia-moyo kimoja kwa kila mtu katika kikundi chao.
Hata kama hisia zetu za kuwa duni ni za kweli, hazitufafanui. Badala yake, hutufanya kuwa wa kipekee! Hebu tujifunze namna ya kutiana moyo na kuthamini upekee wetu.


Wewe ni wa KIPEKEE – kama mwanamume au mwanamke -mzima, wa thamani, uliyeumbwa kwa ajili ya mahusiano yenye afya na matumaini ya siku zijazo!


Safiri kutoka kwenye kushikilia kwa shida na ufikie kwenye kushikilia kwa nguvu.
Mahitaji ya maisha ya ujana yanaweza kuwafanya wahisi wasiwasi, mkazo au hata huzuni. Kila mtu anapambana na ustawi wa kihisia na ni sawa kutokuwa sawa, wakati wote. Ni sawa kuhisi kila aina ya hisia na ni muhimu kukubali na kukubalina na hisia zetu.
Hisia chanya mara nyingi hupuuzwa katika safari yetu ya afya ya akili. Kiwango Chanya cha Ukadiriaji wa Hisia (PERS) ni dodoso jipya la kujiripoti kwa kupima hisia chanya katika watu wanaopambana na hisia zao.
Taarifa katika hati hii haikukusudiwa kuchukua nafasi ya ushauri wa kitaalamu wa matibabu, utambuzi au matibabu. Unapohisi kuelemewa, tafadhali wasiliana na mshauri au mtu mzima anayewajibika ili kukusaidia kushughulikia hisia zako.

Afya ya Akili na Masuala Mengine Mazito
Wawezeshaji wanahitaji kufahamu upungufu wao wenyewe na wanashauriwa sana
kuwaelekeza washiriki kwa vyombo au mashirika husika kwa ajili ya kuingilia kati zaidi na
usaidizi katika masuala ya afya ya akili, unyanyasaji wa kijinsia, kutelekezwa, vurugu au
masuala mengine makubwa ya familia.
Kamilisha “Mtihani wa Urafiki” mtandaoni kwa kiungo hiki kiungo hiki cha tathmini.

Mzazi mpendwa,
Hakuna Majuto ® Sura ya 1, inasisitiza upekee na thamani ya mtu binafsi; umuhimu wa tabia njema kwa mahusiano yenye afya na kukabili siku zijazo kwa makusudi.
Mada hii inawasaidia vijana kuelewa kwamba mtazamo na fikira zetu kuhusu upendo, ngono na mahusiano kwa kiasi kikubwa zinaundwa na vyombo vya habari—kwa ubora au ubaya—inabidi kutumia utambuzi wa hekima [uwezo wa kuhukumu vyema, kuwa na hekima ya kutofautisha kati ya mema na mabaya, sahihi na isiyo sahihi], na kutumia vyombo vya habari kwa usalama, uwajibikaji na kimaadili.
Kuwawezesha wahusika kuelewa ya kwamba jumbe wanazopokea kutoka kwa vyombo vya habari zinaathiri mtazamo wao kuhusu upendo, ngono, na mahusiano hivyo basi kuwasaidia kuona umuhimu wa kutathmini na kutumia vyema vyombo vya habari na kuwa na utambuzi mwema.


Vijana wengi hutoa majibu ya aina mbalimbali wanapoulizwa kuelimika kwenye masuala ya vyombo vya habari ni nini. Wanapodadisiwa iwapo vyombo vya habari vina jumbe nyingi sana zenye fujo/vurugu na ngono, wanaitikia ndiyo, japo wanalichukulia kama jambo linalowaathiri watu wengine - lakini sio tatizo lao. Kuelimika katika maswala ya vyombo vya habari ni kuwa na ujuzi na uwezo wa kuchuja jumbe mbali mbali na kuelewa athari za ujumbe huo kwa jumuiya au utamaduni kama ni huduma za utiririshaji au mitandao.
Ni hali ya kusisitiza umuhimu wa mtu kuchunguza kwa makini na kuchuja ujumbe wowote wa vyombo vya habari unaomfikia akielewa ushawishi wa aina mbali mbali ya vyombo vya habari, kwa mfano redio, magezeti, televisheni, muziki na mtandao na huduma za utiririshaji kama vile Netflix, Disney+, Amazon Prime Video na video za YouTube, IG reel au TikTok.
“Kuanzia redio ya saa inayotuamsha asubuhi mpaka kabla ya kulala usiku tunapotazama kipindi cha mazungumzo ya usiku, tunaonyeshwa picha nyingi sana kadiri ya mamia—hata maelfu na kupewa mawazo mengi kutoka vyombo mbalimbali ikiwamo televisheni, vichwa vya habari vya magazeti, picha zilizo juu ya magazeti, filamu, tovuti, michezo ya video na mabango. Vyombo vya habari havibadilishi tu utamaduni wetu. vimekuwa ndio utamaduni wetu.”
- Kituo cha Elimu ya Vyombo vya Habari Tunawezaje kuwasaidia vijana kuelimika kuhusu vyombo vya habari? Hebu tuwasaidie wawe na uwezo, wawe na fikra makini na walioelimika katika aina zote za vyombo vya habari, ili waweze kutafsiri na kudhibiti kile wanachokiona, wanachosikia na kuingiliana nacho badala ya kuruhusu ujumbe wa vyombo vya habari kuwadhibiti.
Kuwa na ujuzi wa vyombo vya habari ni kujifunza kuuliza maswali sahihi kuhusu kile tunachotazama, tunachosoma na tunachosikiliza.
Mwandishi wa Kufundisha Vyombo vya Habari, Len Masterman, anauita huu uhuru muhimu au uwezo wa kufikiria mwenyewe, ukiwa na utambuzi.


Pata maelezo ya ziada kuhusu kuwasaidia vijana kukuza uhuru muhimu—akili ya utambuzi, katika Kituo cha Elimu ya Vyombo vya Habari, Elimu inayotegemea mfumo wa utafiti.
Ujumbe wote wa vyombo vya habari umeundwa.
1. Swali kuu la kujiuliza: Ni nani aliyeunda ujumbe huu?
2. Swali muhimu la kujiuliza: Je, ni mbinu gani za ubunifu zinazotumiwa ili kuvutia usikivu wangu?
3. Swali kuu la kujiuliza: Je, watu mbalimbali wanaweza kuelewa ujumbe huu kwa njia zipi tofauti?
4. Swali muhimu la kuuliza: Ni maadili gani, mitindo ya maisha na mitazamo gani inayowakilishwa katika, au kuachwa kutoka, ujumbe huu?
5. Swali kuu la kujiuliza: Kwa nini ujumbe huu umetumwa?


Kuonyesha jinsi vyombo vya habari vinavyotuathiri.
1. Eleza mhusika huyohuyo kurejelea neno” spot” mara kumi.
2. Mwombe arudie neno spot tena ila wakati huu, kwa mwendo wa kasi.
3. Kisha bila kukawia, mwulize,” Wewe hufanya nini unapoona taa zikigeuka rangi ya kijani kibichi unapokuwa waendesha gari?’

4. Uliza: Je, unaweza kufafanuaje utambuzi?
5. Je, unafanyaje mazoezi ya utambuzi unapokuja kwenye suala la vyombo vya habari?


Kuwahimiza washiriki kuwa makini wanaposikiliza nyimbo.

Tumia maneno ya nyimbo kuakisi taswira iliyoko katika jumuiya yako. Tafadhali hakikisha kuwa uchaguzi unaofanya hauharibu maadili kwa kuonyesha matusi ama vitendo vyenye kuudhi.

1. Swali:: Ni nini hufanya wimbo uwe wa kuvutia?
2. Swali:: Kati ya hayo hapo juu ni lipi linalokuvutia zaidi wewe?
3. Onyesha maneno ya wimbo uliyochaguliwa katika slaidi au cheza sehemu ya wimbo.
4. Wakiwa katika vikundi vidogo waombe wanafunzi wajadili maswali yafuatayo:
5. Sisitiza kuwa ingawa nyimbo ni kama maneno tu, yanaweza kuwa na athari kubwa sana katika maisha ya watu na matendo yao. Hii ni muhimu sana kuona jinsi sauti ya virusi inavyoweza kuchukua udhibiti wa majukwaa maarufu ya mitandao ya kijamii kama vile TikTok, ambapo kila mtu anaonekana kushiriki katika hisia za virusi au aina fulani ya dansi au matendo.
Hivi majuzi, uchunguzi wa Uingereza uligundua jinsi muziki wa “kuchimba” - aina ya rap inayojulikana kuwa na maneno ya kutisha - inahusishwa na watu wanaotafuta kufanyika mashuhuri kwa kufanya uharibifu. Sio kwamba hilo ni jambo jipya, lakini kuibuka kwa mitandao ya kijamii kumeruhusu kusambaa kwa kurekodi na kushirikisha watu wengi zaidi.
[Hata hivyo], utafiti unaonyesha matokeo yaliyo mchanganyiko sana . . . watu ambao tayari wana mwelekeo wa ujeuri wanaweza kuvutiwa na muziki wenye ujeuri, lakini hiyo haimaanishi kwamba kila mtu anayefurahia muziki huo ni jeuri.
Muziki unatufanya tuhisi hisia za kila namna, baadhi zikiwa hasi . . . na muziki mwingine unaweza “kuwaleta watu pamoja na kuchochea ukaribu wa jamii,” ambayo inaweza kuwa chanya na hasi vile vile.
Muziki una nguvu juu ya hisia zetu. Hakuna viumbe vingine ambavyo vimeibuka kwa njia ya kuhusisha maana na kuunda majibu ya kihemko kwa muziki kama wanadamu. Ni “sehemu ya urithi wetu wa kibiolojia” kwamba muziki hauna upande mzuri tu wa uhusiano wa kijamii lakini pia upande mbaya. “Tunahitaji kutambua hilo ikiwa tunataka kutumia muziki kwa njia nzuri.”


Kuwahimiza washiriki kuwa na utambuzi na kutumia ujuzi wao wa kutathmini wanapotazama matangazo ya biashara katika vyombo vya habari.

[Washirikishi wana uwezo wa kubadilisha tangazo husika na yale yanayopatikana katika mazingira lengwa.Vile vile kuna uhuru wa kuamua kutumia gazeti au jarida katika matangazo husika. Tafadhali hakikisha kuwa uteuzi wako hauna maudhui ya ngono, machafu au vurugu ambayo yanaweza kuudhi au kukasirisha.]

1. Tazama matangazo na/au chunguza kwa makini matangazo katika magazeti/majarida kwa karibu.
2. Ukitumia orodha iliyoko kwenye madaftari ya wanafunzi, fuatilia kwa makini mvuto wa hisia ambao umetumika katika matangazo mbalimbali. Weka alama katika kijisanduku kila mara unapokutana na mvuto huo mahususi.

3. Uliza: Ni mvuto upi ambao unahisi kuwa ulikuvutia au kukuteka? Ni kwa nini?
4. Elezea kikundi hicho kwamba hisia ina jukumu muhimu katika utangazaji.

Uliza: Ni wapi unapata matangazo ya biashara?
Uonyeshe mfano wa filamu au onyesho la TV lenye matangazo ya bidhaa
Uliza: Ni bidhaa, sura ya bidhaa ipi ambayo huonyeshwa kwenye vipindi husika.
Je, unafikiri kampuni hulipa kiasi gani ili bidhaa zao kuwekwa kwenye filamu/onyesho?
Kwa nini makampuni yako tayari kulipa pesa ili bidhaa zao zionyeshwe kwenye filamu/onyesho?


Kusaidia washiriki kukuza jicho pevu kwa kile ambacho ni halisi au bandia.
Wasaidie washiriki kukisia ni nembo gani ni ya asili na ipi ni bandia.
Uliza: Je, itachukua nini kwa mtu kujua ni nembo gani halisi au bandia?
Je, itachukua nini kwa mtu kukuza jicho pevu kwa kile ambacho ni halisi na kilicho bandia kwenye vyombo vya habari?

Vidokezo kwa wawezeshaji:
Kulingana na commonsensemedia.org, vijana wengi wanapata habari zao kutoka kwenye mtandao. (https://www.commonsensemedia.org/press-releases/new-survey-reveals-teens-get-their-news-from-social-media-and-youtube). Ni muhimu kuwasaidia vijana kusitawisha jicho pevu, kuwa na utambuzi, kuhusu mambo wanayoyasoma mtandaoni.

Maswali ya kuzingatia wakati wowote vijana wanapokutana na chombo cha habari:


Kuwasaidia washiriki kukuza utambuzi na kufanya maamuzi ya busara katika matumizi yao ya televisheni/filamu.
1.
2.
3.
4.
5.
🥋🙅🐼
🎈🏠
🔝🔫
🚀🧑🚀 1️⃣3️⃣
⚰️🏊🏊
Jibu: Kung Fu Panda
Jibu: Juu
Jibu: Top Gun
Jibu: Apollo 13
Jibu: Deadpool
Vipindi vya televisheni na sinema vinaweza kuathiri mitazamo, tamaa na tabia za watazamaji wachanga. Bila shaka, burudani huathiri hisia zetu. Inafuata, basi, kwamba lazima kuwe na mabadiliko fulani katika uchaguzi na matendo yetu. Watu wengi wanaamini kuwa kuna uhusiano baina ya vyombo vya habari na tabia halisi. Uchunguzi unaonyesha kuwa maudhui ya ngono na vurugu yameenea sana katika vyombo vya habari, na vijana wanaoangalia maudhui haya wana uwezekano mkubwa wa kuwa na tabia hatarishi za ngono na tabia za fujo.
Ingawa kuna mabadiliko chanya katika mitazamo ya vijana baada ya kutazama filamu,https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7288198/bado wanahitaji kuamua na kutambua jumbe wanazopokea kutoka kwa jukwaa hili maarufu la vyombo vya habari.
Ukweli ni kwamba vijana wachache wataruhusu ushawishi wa vyombo vya habari kuwageuza kuwa wahalifu au wanyanyasaji wa ngono. Lakini ni vijana wangapi ambao watavutwa wanaposhawishiwa na mtu wa jinsia tofauti kwa kufuata ushauri wa sinema walizoona zenye hisia za kimapenzi au picha chafu?
Ni wangapi watajaribu kuvuta sigara au dawa za kulevya kwa sababu tu programu maarufu ya televisheni ilizifanya zisikike zenye kupendeza? Uwezekano kwamba matendo ya vijana yataathiriwa angalau kwa kiasi fulani na chaguo lao la vyombo vya habari ni kubwa mno, hasa kwa kuzingatia wingi wa burudani zinazotumiwa na vijana
Je, utachaguaje kipindi/filamu yako?

| USHAWISHI MKUBWA | USHAWISHI KIASI | LITTLE/NO INFLUENCE |
| 1) Marafiki zako wanasema nini juu yake 2) Muhtasari (onyesho fupi) unaonekanaje 3) Nani ni mwigizaji 4) Nani ni mkurugenzi wa filamu 5) Ni filamu ya aina gani-vichekesho, vitendo, vitisho, mapenzi 6) Imekadiriwaje 7) Maoni ya wakosoaji |
Unaweza kupata taarifa muhimu kutoka kwenye orodha hii lakini huwezi kuamini kabisa sifa hizi. Kuchagua filamu kutokana na ni nani mwigizaji, aliyeitengeneza, imekadiriwa nini, au aina yake sio jibu kamili. Waigizaji na wakurugenzi wengi wana filamu nzuri na mbaya kwenye wasifu wao.
Muhtasari (vionyesho vifupi) unaweza kufichua sauti ya filamu lakini hauwezi kukupa habari kamili kwa sababu huitayarisha kwa ajili ya hadhira ya jumla, na kwa kawaida hawaonyeshi picha za walio uchi au wenye majivuno.
Muhtasari wa Filamu ni kipengele muhimu kinachoelezea ukadiriaji wa filamu. Muhtasari wa kawaida unaweza kusema kitu kama “Iliyokadiriwa R kwa vurugu ya picha, matumizi ya dawa za kulevya, hali ya ngono na uchi.” Hayo ni maelezo muhimu kuwa nayo unapojaribu kuamua.
Kutegemea wengine wakufanyie maamuzi kuhusu sinema yako ni kosa. Kupata habari ambayo itakusaidia kufanya maamuzi yako mwenyewe ni wazo nzuri. Tovuti yenye manufaa: www.pluggedinonline.com


1. Maonyesho/filamu zinazo kufuru

2. Maonyesho/filamu za uchawi
3. Maonyesho/filamu Potofu
4. Maonyesho /filamu za ngono


Miongozo kwa zile zilizo na ukungu: Hata baada ya kuondoa kategoria hizo zilizo wazi, bado kuna chaguo nyingi za filamu ambazo zina baadhi ya ngono, vurugu, lugha chafu au mchanganyiko wa hizo tatu.

Je, ni muda gani unaokubalika kwa tukio la ngono kupita? Vipi kuhusu idadi kamili ya watu katika filamu wenye jeuri? Je, una mfumo wa uhakika wa kuhesabu maneno ya matusi?
Nambari yoyote itakuwa ya chini sana au ya juu sana. Badala yake zingatia baadhi ya maswali unapotathmini kipindi/sinema:
1. Toni ya kipindi/filamu ni nini?
2. Je, kuna maadili katika hadithi?
3. Je, unaweza kujifunza chochote kutokana na kipindi/filamu?
4. Je, filamu inaweza kuzidisha tatizo ambalo tayari unalo?
5. 💭 Je, utajuta baadaye ikiwa matukio kutoka filamu hii yatajirudia kichwani mwako?

Kwa sinema zingine, majibu ya maswali haya yatakuwa dhahiri lakini kwa nyingine, majibu yake ni magumu kuyapata. Huenda ukajihisi kama mpuuzi mwanzoni, ukifanya “utafiti” na kujibu maswali kuhusu kitu ambacho ni burudani tu, lakini itakufaa baada ya muda mrefu na utambuzi unapokuwa mazoea, utakuza fikra makini na uchaguzi bora katika maisha yako.
Kuwasaidia washiriki kuelewa namna ya kujishirikisha katika changamano la ulimwengu pepe (wa dijitali) na kukuza ufahamu wa uzuri na ubaya wa michezo ya kitekinolojia, mitandao ya jamii, na kustawi kwa ujuzi katika jumuiya hii ya pepe wakitumia mazungumzo na mahusiano yaliyo mema na ya afya njema.
Mtandao na ulimwengu pepe, kama tunavyoujua, unabadilika na kubadilisha jinsi tunavyofanya kazi, kufanya biashara, kucheza na kushirikiana. Ukuzaji wa ulimwengu pepe una maana kuwa tunaweza kufanya kitu chochote na, mahali popote.
Bob Hoose kutoka Plugged In alitoa angalizo hili muhimu:
“Sasa hivi ulimwengu pepe haujafanya kazi kikamilifu”. Lakini, kama mtandao, polepole kutakuwa na mabadiliko kidogo kidogo mpaka utakamilika, nasi tutaukubali. Lakini wakati huu, tunao ujuzi wa kile tunachokitegemea katika mabadiliko ya ulimwengu wa mtandao, na iliyo vyema zaidi ni kwamba tunayo mawazo ya mahali ambapo tungependa mambo haya kwenda. Na huo ni mwanzo mzuri hata kama ni wa kudhania tu.”
Tofauti kati ya ulimwengu halisi na ulimwengu pepe inapoanza kupungua na kukawa kama kuna ukungu, ni rahisi kuelemewa. Kuzuia kabisa ufikiaji wa jukwaa hili la media haiwezekani, kwani shule nazo zimeanza kuitumia katika elimu. Kukosoa mara nyingi maovu ya vyombo vya habari kutapanua pengo la mawasiliano kati ya watu wazima na vijana.
Tunachoweza kufanya ni kuwasaidia vijana kustawi katika nafasi hii ya ulimwengu pepe, na kuwawezesha kuwa na ujuzi (kuitumia huku wakiwajibika na kwa usalama) makini (uwezo wa kutathmini) na elimu (maarifa ya kutafsiri).
Pia ni muhimu kuwasaidia vijana kuweka mipaka mizuri kuhusu lini, wapi na jinsi wanavyopata mitandao. Wahimize kuweka njia za mawasiliano wazi, kiuhalisia na kimwili, na marafiki zao, wazazi na watu wazima wanaoaminika kuhusu mambo yanayowavutia na uzoefu wao mtandaoni. Pia ni muhimu kujifunza kujenga uaminifu na mahusiano ya maana pamoja nao.
Ulimwengu pepe upo hapa sasa, na utawasilisha changamoto mpya kila wakati kadri teknolojia inavyoendelea kukua. Kuwasaidia vijana kujenga mwingiliano wao wa kijamii na kihisia katika ulimwengu pepe na ulimwengu halisi kutawasaidia kustawi katika jumuiya hii..


Kuwasaidia washiriki kuelewa wema na ubaya wa michezo ya mitandaoni na jinsi ya kufurahia kuzama kwenye hii michezo kwa usalama na kuwajibika huku wakiweka mipaka inayofaa.

Tumia picha kuakisi baadhi ya faida na hasara za michezo ya mitandaoni. Tafadhali hakikisha kuwa uteuzi wako hauna maudhui ya ngono, lugha chafu au vurugu ambayo inaweza kuleta usumbufu.


Waweke washiriki katika vikundi vidogo au wahimize kuinua mikono yao ili kuchangia mjadala wa darasa. Washiriki wachague meme za michezo zinazowavutia zaidi—zile wanazoweza kuzitambua zaidi. Waambie waeleze ni kwa nini.

Baada ya mwingiliano huu, endelea kuwauliza washiriki wakueleze faida na hasara za michezo mtandaoni, na uandike majibu yao kwenye ubao mweupe.
ULIZA: Unafikiri vijana wanawezaje kucheza kwa usalama na kwa kuwajibika wakiwa na mipaka na vikomo?


Kuwasaidia washiriki kuelewa wema na ubaya wa michezo ya mitandaoni na jinsi ya kufurahia kuzama kwenye hii michezo kwa usalama na kwa kuwajibika huku wakiweka mipaka inayofaa.

Wakusanye washiriki katika vikundi vidogo kwa ajili ya majadiliano au wahimize kutoa majibu yao kwa sauti kubwa.
Waombe washiriki kuorodhesha faida na hasara za uchezaji mtandaoni.
Andika ubaoni wakati washiriki wanapotaja majibu yao. Hitimisha shughuli hii kwa maswali haya.
ULIZA: Unafikiri vijana wanawezaje kucheza kwa usalama na kuwajibika wakiwa na mipaka na vikomo vya afya?
Kwa mashirikiano ya kina, wawezeshaji wanaweza kuendeleza majadiliano yao na maswali haya.


Kuwasaidia washiriki kugundua vipengele vinavyofanya michezo ivutie sana, na mitego yake (matatizo).
Waweke washiriki katika vikundi vidogo kwa ajili ya majadiliano au wahimize kutoa majibu yao kwa sauti kubwa. Wanafunzi wajadili mambo ya kusisimua ya uchezaji wa video na mitego yake.
Uliza: Kwa nini ni vigumu kuacha kucheza michezo ya mtandaoni? Ni vipengele gani vinavyoifanya kuvutia sana?
Je, kuna programu maalum za michezo ya mitandaoni au aina ambazo zinaleta “uraibu” zaidi?
Tunaweza kujifunza nini kutokana na michezo ya mitandaoni?
Je, kuna matatizo gani ya michezo ya mtandaoni siku hizi?
Tufanye nini basi sisi ili tusiwe na uraibu wa michezo”?

Ulimwengu pepe ni mahali pa kuvutia kwa sababu unaweza:

Tabia - kufichuliwa mara kwa mara kwa vurugu katika michezo ya mitandaoni huathiri tabia. Tabia ya mtu kwenye hiyo michezo huwafanya watu fulani kuathiriwa zaidi na jeuri baada ya kumuona. Bila kujali kama mtu anakuwa na jeuri kwa sababu ya michezo ya mtandaoni, mtu yeyote anaweza kutohisi vurugu na kutopenda vurugu katika maisha halisi. Mtu anapoona matukio ya jeuri/vurugu mara nyingi, inasababisha kukosa huruma kwa wahasiriwa halisi wa vurugu.
Dhidi ya jamii - Ingawa michezo mingi inaweza kuwa na jumbe chanya au kuwapatia nafasi vijana wenye haya kuungana na wenzao, kuna hatari pia ya ujumbe dhidi ya jamii au kuwahimiza wachezaji kuona vikwazo kama ni vitu vinavyopaswa kuharibiwa.
Tabia hizi huwa zinaathiri ujuzi wa kujua namna ya kuwa na mahusiano ya kweli na jamii.
Michezo ya video imeundwa ili kuangaza vituo vya zawadi kwenye ubongo wetu kwa kutoa changamoto zinazoendelea, na kutoa dopamini kila tunapokuwa na mafanikio. Tusipokuwa waangalifu, hii inaweza kusababisha msukumo, kutokuwa na subira na kuonyesha hasira mchezo unapokatizwa.
Limits - Katika nyumba yoyote, pengine kuna skrini nyingi kuliko wakazi. Fursa za michezo ya mitandaoni ziko kila mahali—kompyuta za kibinafsi, koni za michezo, kompyuta kibao, simu mahiri, n.k. Zaidi ya hayo, mtandao hutoa michezo mingi isiyolipisha hela na bila vizuizi au kanuni za umri unaofaa, muda unaotumika na maudhui. Wakati mwingine, maudhui katika michezo hii yanaweza kuwa kinyume kabisa na maadili yetu, na huna udhibiti wa picha unazoziona (asili ya ngono au vurugu). Matumizi ya kupita kiasi yanaweza pia kusababisha hali ya kuwa na msisimko mkubwa wakati wote.
“Msisimko unajitokeza kwa njia tofauti kati ya mtu na mtu, unaweza kujidhihirisha kwa ugumu wa kuzingatia, kudhibiti hisia, kudhibiti msukumo, kufuata maagizo na kuvumilia fadhaa.” -Fiona Swanson, mfanyakazi wa kijamii wa kliniki katika Saikolojia huko Mankato, Minnesota.
Mfiduo - Kuua ni njia tu ya kuondoa adui bila madhara kwako. Kulingana na Chuo cha Marekani cha Madaktari wa Watoto, 85% ya michezo ya video, hata ile iliyopewa alama ya “E kwa kila mtu,” ina baadhi ya vipengele ambapo mchezaji hudhuru mwingine kimakusudi.
Uraibu - Watafiti wamegundua kwamba kuna mabadiliko ya kiutendaji na ya kimuundo katika neva za waraibu wa michezo ya mtandaoni, kwani wanapowawekea ishara za michezo ya mitandaoni inayoleta tamaa, mfumo wa neva unakuwa na mabadiliko ya aina fulani. Mabadiliko haya ya neva kimsingi ni sawa na yale yanayoonekana katika waraibu wa matatizo mengine.

Dkt. Mitch Prinstein, mwanasaikolojia wa kimatibabu na afisa mkuu wa sayansi wa Shirika la Kisaikolojia la Marekani, alionyesha wasiwasi wake kwamba wakati wa michezo ya mtandaoni, kijana anaweza kujifanya na kucheza kama mtu mwingine ambaye sio ubinafsi wake. Hii ni hatari kwa vijana ambayo inaweza kuathiri kujitambua uhalisi wao wenyewe wakiwa hawako mtandaoni. Vyombo hivi vipya, na uwezekano huu mpya, unaweza kutumika kwa wema au kwa uovu”

Unaweza kucheza kwa usalama na kwa kuwajibika, ukiwa na mipaka na vikomo vinavyofaa, ukitumia miongozo hii michache.
Jipanue - Chunguza mambo yanayokuvutia katika uchezaji wa mtandaoni kwa kutembelea maeneo mbalimbali, watu na mada zinazohusiana na mchezo unaoufurahia. Iwapo unapenda michezo yenye muktadha wa kitamaduni, nenda kwenye jumba la makumbusho linaloonyesha vipengele vya kihistoria. Ikiwa unajihusisha na michezo ya spoti, jaribu michezo yenyewe halisi. Itakushangaza jinsi ambavyo utaboreshwa na mambo hayo.
Uwezekano - Panua uchezaji wako uwe ni zaidi ya kucheza tu mtandaoni. Chunguza jinsi michezo hii inavyotengenezwa hasa vipengele vya ubunifu na ufundi. Pia uangalie utungaji wa hadithi, muziki unaoambatana nazo, wanavyoziuza na hata talanta ya sauti zinazotumika kuongea. Fanya uchunguzi juu ya uwezekano wa kuunda mchezo wako mwenyewe na kila kinachohitajika kuufanikisha. Uwezekano wa kugeuza kupenda kucheza michezo kukawa taaluma yako unasisimua.
Tumia Mzani - Haijalishi jinsi ambavyo unazama na hata kuona uhalisi wa ulimwengu pepe, kamwe hautachukua nafasi ya mawasiliano na watu ana kwa ana. Weka mipaka ya michezo ya mitandaoni na uthamini mahusiano halisi na watu. Onyesha ukomavu na heshima kugawanya muda wako kati ya kucheza na wazazi wako. Utashangazwa na jinsi wazazi wako watakavyokufurahia unapoonyesha kuwajibika.
Usalama - Tabia nzuri za kucheza michezo mtandaoni ni kujua jinsi ya kukaa kwa usalama mtandaoni. Usiwahi kufichua taarifa za kibinafsi na maelezo yako na ya familia yako kwa mtu yeyote—hata marafiki unaowajua. Usipange kamwe kukutana na mtu ana kwa ana ambaye umekutana naye mtandaoni peke yako bila mtu mzima unayemwamini.
Orodha - Amua orodha ya vile utavyovifanya au vile ambavyo hutavifanya. Kwa mfano: Nitaweka kikomo cha muda wa kuwa kwenye michezo yangu mtandaoni; nitakuwa na heshima ninaposhiriki na wengine mtandaoni; nitamweleza mtu mzima ninayemwamini kama jambo baya likinitokea wakati ninacheza; Sitashiriki katika michezo iliyokadiriwa kuwa ya watu wazima (jifunze kuhusu kufaa kwa michezo kupitia kategoria za ukadiriaji wa mchezo wa ESRB: https://www.esrb.org) ; Sitaanza mchezo wangu ikiwa sijatimiza wajibu wangu mwingine kama vile kazi za shule, kazi za nyumbani na miradi.
Kwa ufahamu wa kina zaidi juu ya ulimwengu wa michezo ya mitandaoni:

Vidokezo kwa wawezeshaji:
Vidokezo kwa wawezeshaji:Wawezeshaji hawana haja ya kucheza kila mchezo ambao vijana wanacheza, lakini itasaidia kujua sheria na masharti machache ya michezo ya
mitandaoni. Hapa kuna baadhi ya misingi:



Mnamo mwaka wa 2018, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) liliainisha uraibu wa michezo ya mitandaoni (ugonjwa wa michezo ya mitandaoni) kama hali ya afya ya akili.
Sio tu kwamba mchezo wa video unaweza kuwa wa matatizo na unahusishwa na athari chanya na mahusiano ya kijamii, lakini pia unaambatana na dalili za kisaikolojia, mikakati ya kukabiliana na hali mbaya, hisia hasi, kutojithamini, kupendelea upweke, na utendaji duni shuleni.

Maswali yafuatayo yanatoa zana rahisi ya uchunguzi ili kuwasaidia vijana kuchakata ikiwa tabia zao za uchezaji zimeanza kuwa kitu kinachoweza kuwadhuru.
| NDIYO | HAPANA | WAKATI MWINGINE |
| 1) Kazi ya shule haimaliziki 2) Unaacha masomo na shughuli nyingine ili kucheza mtandaoni. 3) Unashikwa na hasira na kutokuwa na raha unapojaribu kupunguza au kuacha shughuli za mtandaoni. 4) Unawadanganya familia/marafiki kuhusu matumizi, tabia ya mtandaoni. 5) Unahitaji kutumia muda au pesa zaidi kwenye shughuli za mtandaoni ili kuendelea kusisimka kama ulivyozoea. 6) Unakuwa mtandaoni ili kuepuka matatizo, hisia mbaya au mafadhaiko. 7) Unafikiria shughuli za mtandaoni mara nyingi 8) Unaiba hela ili kufanya shughuli za mtandaoni. 9) Unakopa hela ili uzitumie kwa shughuli za mtandaoni. 10) Unajaribu kucheza mara chache au kupunguza muda wa kucheza lakini unashindwa. |
Kamilisha mtandaoni kwa kiungo hiki cha tathmini.
Waombe washiriki kuzingatia maswali haya ndani ya muda wa mwaka uliopita (mwaka 1). NDIYO (1) , HAPANA (0), WAKATI MWINGINE (0.5). Jumla ya alama zako.
Zaidi ya pointi 5: Tafuta usaidizi wa kitaalamu ili kujua ukubwa wa tatizo lako.
Pointi 2 hadi 4.5: Kuwa mwangalifu, kwani shida yako inaweza kuongezeka.
Chini ya pointi 2: Matumizi yako yana usawa kwa kiasi fulani.

Kumbuka kwamba maelezo katika waraka huu hayakukusudiwa kuchukua nafasi ya ushauri wa kitaalamu wa matibabu, utambuzi au tiba. Tafadhali wasiliana na mshauri au mtaalamu kwa usaidizi zaidi.


Kusaidia washiriki kudhibiti teknolojia yao ili wanufaike na kustawi ulimwenguni wanamoishi kulikojaa mitandao ya kijamii.
Dunia inaonekana kuwa ndogo zaidi siku hizi za mitandao ya kijamii. Imekuwa jukwaa bora la kuonyesha wewe ni nani (au unataka kuwa nani), kuendelea kuwasiliana na marafiki wa sasa, kuungana tena na marafiki wa zamani, na kuwasiliana na kile kinachotokea katika maisha ya marafiki zako. Majukwaa ya mitandao ya kijamii yamekuwa nafasi ya kuandaa mikusanyiko, vikundi vya maslahi, na vya misaada mbalimbali. Lakini haya mahusiano ya mitandaoni je yanaweza kuimarika? Je, mahusiano ya ulimwengu pepe ni sawa na mahusiano ya ana kwa ana? Kutegemea mahusiano ya mitandao ya kijamii kunaweza kutoa hisia potofu za urafiki na sio mbadala wa jambo halisi.
Je, itakushangaza kwamba wataalamu wa teknolojia wa wakati wetu huona muda wa kutumia mtandao kama kitu kibaya na huweka mipaka mikali kwa muda wa skrini wa watoto wao wenyewe?
Shida kuu ya mitandao ya kijamii ni hali yake ya uraibu na inahusishwa na watu kutokuwa na furaha, wasiwasi, unyogovu na usingizi duni.


Wakusanye washiriki katika vikundi vidogo kwa ajili ya majadiliano au wahimize kutoa majibu yao kwa sauti kubwa.
Waombe washiriki kuorodhesha wanachopenda na wasichokipenda kuhusu mitandao ya kijamii.

Andika majibu ya wanayoyatoa washirika ubaoni. Hitimisha shughuli hii kwa maswali yafuatayo.
ULIZA: Unafikiri vijana wanawezaje kuwa washawishi chanya (badala ya kushawishiwa) na kuleta mabadiliko katika nafasi hii?
Kwa mashirikiano ya kina, wawezeshaji wanaweza kuendeleza majadiliano yao na maswali haya.


Cheza mchezo wa bingo na uone upande wa kejeli wa mitandao ya kijamii.
Kadi ya Bingo ya Maungamo ya Mitandao ya Kijamii.
Je, Unatumia Teknolojia au Inakutumia Wewe?
| Nimeanguka
kwenye
shimo refu. [kunaswa katika hali ya kushangaza, ya kutatanisha au isiyo na mantiki, na mara nyingi ni ngumu kutoka] | Nimeangalia mtandao badala ya kulala, kusoma au kuhusiana na watu ana kwa ana . | Nilitumia muda mrefu kujipiga picha nzuri au niliiweka kwa gramu [Instagram]. |
| Nimepata maoni kwenye chapisho langu kutoka kwa mtu nisiyemfahamu kabisa [nani huyo]. | Nihudhurie Hakuna Majuto® ili kujifunza jinsi ya kudhibiti [kwa hakika, ninyi nyote]. | Nililiona tangazo likitokea kwenye mipasho yangu nilipokuwa nikilifikiria [inatisha] |
| Naliwafuatia watu ambao walinifanya nijisikie vibaya au hata siwapendi [kwa nini]. | Nilivunja urafiki kwa sababu ya mtazamo na maoni yake ya kipuuzi [hiyo ni kweli]. | Nilichapisha makala bila kusoma ujumbe wote [Vichwa vya habari ni bora zaidi] |
Wagawe washiriki katika vikundi au waambie watafute mshirika wa karibu nao.
Piga picha ya kadi ya bingo na simu yako na utumie lebo ya simu yako au programu ya kuhariri ili utumie simu kucheza bingo. (Kwa warsha wa mtandaoni, unaweza kupiga picha ya skrini na kutumia kalamu.)
Weka mviringo kwenye maungamo yako, na uonyeshe kadi yako kwa kikundi au mshirika wako na uchague kigae kimoja ili kushiriki uzoefu wa kibinafsi.
Katika vikundi au wawili wawili, jadili jinsi unavyoweza kuchukua hatua kupunguza athari mbaya za teknolojia hizi kwenye maisha yako.


Kuwa na majadiliano ya uwazi na washiriki kuhusu swali hili: Je, teknolojia kama vile mitandao ya kijamii inatusaidia au inatuumiza?

Tazama klipu ya video na uwaombe washiriki kuweka maanani nambari na mwenendo.
Wakusanye washiriki katika vikundi vidogo kwa majadiliano au wahimize kutoa majibu yao kwa sauti kubwa baada ya kutazama klipu ya video.

Uliza: Ni sehemu gani ya klipu hii ya video inasema na wewe? Je, una uzoefu wa kibinafsi wa kushiriki?
Ni aina gani ya maudhui kwenye mitandao ya kijamii huwa yanakufanya ujisikie vibaya? Je, unayaona mara ngapi?
Je, unadhani mitandao ya kijamii inaundaje tabia zako za kila siku?

Vidokezo kwa wawezeshaji:
Tuwafundishe vijana kutumia mitandao ya kijamii vizuri na kuwa na ushawishi mzuri. Tunahitaji
kukiri mambo mazuri juu yake. Ikiwa tutazungumza tu na vijana kuhusu jinsi mitandao ya kijamii
ilivyo mibaya, tutawatenga na kushindwa kuwatayarisha kufanikiwa katika nafasi hii.

Inaelimisha. Kuna maudhui yasiyo na mwisho ya kutufundisha kuhusu jambo lolote chini ya jua.
Inaunganisha na hutusaidia Kuwasiliana. Imeruhusu uhusiano mkubwa na wa kina na watu wengine. Imetusaidia kuwasiliana na mtu yeyote duniani kote, wakati wowote. Inatusaidia kukuza ujuzi wa kijamii.
Inatupatia Sauti. Sio kila mtu ana fursa ya kuingia kwenye vyombo vya habari vya kawaida kama televisheni na redio. Imewapa watu wengi sauti na kwa kuongezeka kwa wafuasi, ujumbe wao unasikika kwa njia za nguvu.
Inatupa Kufikia Wengi. Haitoi tu maudhui bali pia kufikia watu kutoka kwa uzoefu mbalimbali na asili tofauti. Tunapata kujifunza kuhusu matukio ya ulimwengu na mambo yaliyopo nje ya mazingira yetu ya karibu. Inapanua mtazamo wetu wa ulimwengu na kutuwezesha kuwa raia wanaoshughulika katika jumuiya.
Inatia Moyo na Inafurahisha. Inatoa maudhui ya kuinua na kuchekesha na inaweza kuwa jumuiya ambayo inatumika kama faraja kwa watu walio wapweke, wanaopambana na maisha, na waliokumbwa na masuala ya afya ya akili. Kicheko kinaweza kuwa dawa nzuri.

Mtu aliyeandika mtandaoni hajulikani ni nani. Kutokujulikana kunawarahisishia watu kuandika maneno ya chuki na ukatili kwa mtu mwingine ambaye hawajawahi kukutana naye au ambaye kamwe hawatakutana naye. Mfano wa kusikitisha wa hili ni hadithi ya Amanda Todd, kijana aliyejiua baada ya kudhulumiwa mtandaoni kwa kuwa alituma ujumbe wa ngono.
Inatufanya tujihisi kuwa duni. Kujilinganisha kila wakati na mwili “mkamilifu” na maisha “makamilifu” huathiri kujithamini kwetu. Tunajisikia vibaya tunapokosa kupendwa vya kutosha mtandaoni na tunahisi kuwa hatufikii picha ya maisha bora tunayoyaona mtandaoni kila wakati.
Inakengeusha. Tunakengeushwa kila wakati arifa ya simu inapotuarifu kuingia kwa ujumbe, na mara nyingi ujumbe ni kuhusu jambo dogo. Ni desturi yetu kukusanyika na marafiki ili kuongea —lakini maongezi yanakatizwa na arifa za simu zetu mara kwa mara.
Inahusu Kutosheka Papo Hapo. Mtandao umetuunganisha kwa hivyo tunatarajia watu wengine watujibu mara moja, wasipofanya hivyo tunakasirika. Pia tunaona kama ni lazima kujibu kila ujumbe tunaoupokea na tunashindwa kuwafurahia watu tulionao, au tunavurugika wakati tukiwa kazini.
Ni kuhusu kuweza kupata kwa wingi maudhui na taarifa . LAKINI, inakuwa vigumu kutambua ni habari gani ni za thamani au za kutegemewa. Kuweza kufikia jumuiya nyingine nyingi ni vizuri lakini pia ni hatari. Unaweza kushawishiwa polepole kuchukua maadili kutoka kwenye jumuiya hizi ambayo ni kinyume cha maadili yako au ya familia yako. Kupata habari kwa wingi pia huleta hofu (Kujihisi Kupungukiwa) kwa sababu sasa tunajua mambo mengi zaidi ya yaliyo uzoefu wetu
Inachukua Muda. Tunaweza tukawa hatufanyi kitu chochote kibaya kwenye mitandao ya kijamii lakini hatufanyi chochote kizuri kwani mtandao unachukua muda na nguvu zetu nyingi na kutuzuia kujenga mahusiano na ujuzi, kwa vile muda mrefu tunautumia kwenye huu ulimwengu pepe.
Kama chombo kilichoundwa kwa sababu nzuri ya uhusiano wa kibinadamu, kina mapungufu yake. Maandishi, picha, meme na emoji haziwezi kujaza kina na wingi wa mwingiliano wa ana kwa ana.

Taarifa yoyote unayoweka kwenye mtandao (anwani ya barua pepe, maelezo ya kadi ya benki, tarehe ya kuzaliwa, wanafamilia, elimu yako, historia ya kazi, n.k.) inaweza kufikiwa na kutumiwa vibaya na mtu mwingine kwa niaba yako. Taarifa hizi zinaweza kutumiwa na “wezi” wanaojifanya kama kwamba wao ni wewe na wakafikia rasilimali au marupurupu yako. Kadiri unavyoweka habari zako mtandaoni, ndivyo unavyojihatarisha zaidi. Sio salama au busara kutembea barabarani na jina na anwani yako vimeandikwa kwenye shati lako, sasa kwa nini uweke habari kama hiyo kukuhusu kwenye mtandao?

Kila wakati angalia mipangilio yako ya faragha ili kuzuia umma kufikia mambo yako ya kisiri?

Mipaka ya mtandaoni mara nyingi hukosekana—kutoka kwa kushiriki mara nyingi sana au kuunganishwa na watu usiowajua. Inapashwa kututia wasiwasi jinsi ilivyo rahisi mtandao kuwa na maudhui yasiyofaa (maudhui ya ngono, vurugu au ya kutatanisha). Kushiriki picha mtandaoni ukifanya mambo ya kipuuzi na ya kitoto kunaweza kukachekesha ukiwa na umri wa miaka 15, lakini picha hizi zinaweza kukudhuru baadaye maishani, kwa mfano, mwajiri mtarajiwa au mama mkwe anapokutafuta mtandaoni. Hata kama picha uliyoweka wewe imeshaondolewa, mtu mwingine anaweza akawa ameichapisha mahali pengine. Alama yako ya kidijitali inaweza kufuatiliwa. Kama huamini hebu tafuta jina lako mtandaoni, uone.
Mitindo mingine ina uwezo wa ajabu wa kuenea na kuwa na uwezo wa kushawishi watu kufanya maamuzi ya kubadilisha maisha yao. Mitindo mingine ni ya ucheshi na mingine ina nia njema kama vile Shindano la Ndoo ya Barafu - Ice Bucket Challenge.
Walakini, zingine ni za kushangaza na hatari kabisa kama Shindano la Tide Pod.
Vijana nchini Indonesia wamekuwa wakiruka mbele ya malori yaliyo mwendoni barabarani huku wakishiriki katika shindano hatari la TikTok linaloitwa “mzaha wa malaika wa kifo” ambao umesababisha vifo vya watu wawili tayari.
Unyanyasaji mtandaoni unazidi kuwa ni jambo linaloenea kwa kasi duniani kote, hasa miongoni mwa vijana. Kwa sababu ya upatikanaji mkubwa wa mtandao, na kwa sababu ya urahisi wa kusambaza habari, inakuwa rahisi kwa watu wenye nia mbaya kueneza uvumi, dhihaka, vitisho au kuwaogopesha wengine. Ingawa si vigumu kutambua chanzo cha vitisho na uvumi, athari ya jumbe hizi inaweza kusababisha uharibifu zaidi kuliko inavyotarajiwa. Katika baadhi ya matukio, inaweza hata kusababisha mtu kujiua.
Kuanzia vyumba vya mazungumzo katika michezo maarufu hadi mifumo ya mitandao ya kijamii, watu wanaonyanyasa kingono huwalenga vijana ambao wanaweza kuwahadaa, kuwadanganya au kuwatishia kwa urahisi. Wanachukua fursa ya kwamba vijana wanapotumia mitandao ya kijamii hujibu maombi yasiyo na hatia na kukubali kuunganishwa. Basi wanawaambia maneno ya kuvutia na kuwatia moyo ili wawe na mawasiliano zaidi. Urafiki unaoonekana mwanzoni kutowa na hatia unapoendelea mwishoni mtu anaomba picha za uchi au mazungumzo ya ngono yasiyofaa. “Unyanyasaji wa ngono” pia ni tishio linaloongezeka. Unaweza kutoka kwa mpenzi wa zamani au mtu aliyepata picha au video za ngono za mwathiriwa. Wakitumia hizo na kutishia kuzifichua kwa familia, marafiki au kwenye majukwaa ya umma, wavamizi “hunyanyasa ngono” wakidai picha nyingine za uchi, video au hata kushiriki ngono nao.
Tazama ripoti hizi za ufichuzi kuhusu mada ya urembo wa kingono mtandaoni. Unaweza kuonyesha klipu hizi za video kwa washiriki ili kuleta ufahamu juu ya suala hili. Video Clip: Dating A Predator: “The Teacher” [https://youtu.be/i4iIBEM-gvoMwandishi wa habari wa siri, aliyejificha kama mtoto wa miaka 15, anakutana na mwindaji wa ngono ya watoto ambaye aliwasiliana naye kwenye WeChat. Haikuchukua muda mrefu akamwomba aende naye kwenye chumba cha hoteli.
Video Clip: Social Media Dangers Exposed by Mom Posing as 11-Year-Old
Mama mwenye umri wa miaka 37 anajifanya kama msichana wa miaka 11 ili kufichua hatari zinazowakabili watoto kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii kama vile Instagram, Snapchat, TikTok, na Kik. Wakiachwa bila kusimamiwa, watoto wadogo wanaweza kukabiliwa na wavamizi wa mtandaoni, na unyanyasaji wa kisaikolojia ndani ya dakika chache.
Tunaangazia maswala haya ili kuleta ufahamu na sio hofu. Tunaamini kujifunza kutumia mitandao ya kijamii vizuri na kwa usalama kunawezekana. Badala ya kufuta akaunti yako ya mitandao ya kijamii au kuikumbatia ovyo, unaweza kuwa na hekima na utambuzi kuwa mshawishi chanya badala ya kuathiriwa vibaya.
Unafikiri vijana wanawezaje kuwa washawishi chanya na kuleta mabadiliko kwenye nafasi hii?
Kanuni Ni Muhimu. Kuna sababu nzuri kwa nini tovuti za mitandao ya kijamii zina ruhusu watu wa umri usiopungua miaka 13. Hii ni kwa sababu za kisheria na usalama/faragha. Shiriki kwenye tovuti zinazofaa umri wako, hii itakusaidia kukaa salama. Japo mipangilio ya faragha sio mikamilifu lakini inasaidia sana. Chukua muda ujifunze mipangilio na udhibiti wa faragha inayokufaa.

Chapisho Lako Ni Muhimu. Fikiri kabla ya kuchapisha. Kila kitu tunachochapisha kinaweza kuonekana na hadhira kubwa. T.H.I.N.K (FIKIRI) kabla ya kuchapisha:


Kusuluhisha Migogoro. Usiepuke ugomvi wa ana kwa ana na badala yake ukawasilisha “mawazo” yako kwenye mitandao ya kijamii. Kuwasiliana ana kwa ana na walengwa wako ni njia bora zaidi. Tengeneza nafasi za kuunganishwa na kuongea, sio za kuchanganyikiwa na machafuko.
Omba Ruhusa. Usiweke mtandaoni picha za watu wengine bila idhini kutoka kwa watu wamiliki wa picha hizo.
Tabia. Uwe mtu mwenye adabu wakati wote. Mheshimu kila mtu na usiweke mtandaoni chochote ukiwa na hasira. Fuata Kanuni Bora—Watendee wengine jinsi unavyotaka kutendewa. Watendee na kuzungumza juu yao mtandaoni kama vile ambavyo ungewatendea na kuzungumza nao ana kwa ana. Huwajibikii jinsi watu wanavyoguswa, lakini ni jambo la kuzingatia ikiwa chapisho litamfanya mtu mwingine ajisikie vibaya.
Mambo ya Jumuiya. Endelea kuwasiliana na jumuiya inayoaminika ambayo unajua itakuwa ushawishi mzuri kwako


Kuwawezesha washiriki kubadilisha jinsi wanavyotumia vyombo vya habari .

Waombe washiriki wakamilishe taarifa iliyo hapa chini ili kuwasilisha jukumu la vyombo vya habari vya kidijitali katika maisha yao:
Mifano:
Fanya mpango wa jinsi ambavyo ungependa kubadilisha tabia yako ya mitandao ya kijamii. Fikiria ni wakati gani utafanya kitu tofauti na unavyofanya sasa na kitu gani unachoweza kufanya badala yake. (Kubadilisha tabia si rahisi. Usifikirie tu kile ambacho hutafanya. Orodhesha mambo ambayo utafanya pia!)

[Majibu yatatofautiana, yafuatayo ni baadhi ya majibu yanayowezekana]
Changamoto zangu za media ni pamoja na:
Kuwawezesha washiriki kuelewa madhara ya ponografia (filamu za kuzua tamaa).
Ingawa vyombo vya habari vinaweza kupotosha mtizamo wetu kuhusu upendo wa kweli, kuna njia nyengine ya mawasiliano iliyo na madhara mengi zaidi- ponografia.
Mtazamo wa mtu kuhusu wanawake au wanaume unaweza kubadilishwa kutokana na kuangalia picha potovu za jinsia mbalimbali za kuzua tamaa.Picha hizi potovu hazibadilishi tu mtazamo wetu wa upendo bali pia zinapotosha kuelewa kwetu kuhusu uhusiano wa kindani.
Badala ya kukuza maadili na heshima, ponografia hudunisha watu na kuwafanya kama vyombo vya anasa. Hata kutazama tu picha za ashiki kijuujuu kunaweza kumfanya mtu awe na mtazamo tofauti kuhusu uhusiano wa kindani.
Athari ya picha za ngono ni mbaya kwa uhusiano na inadumu zaidi kuliko athari inayotokana na vyombo vya habari. Nyenzo zinazoonekana kuwa zisizo na madhara kama vile picha kwenye Instagram, zinaweza kumvutia mtu na kumfanya aangalie mambo machafu zaidi. Aidha, mtu huenda akawa mtawaliwa na mraibu wa picha za ngono. Hatimaye, mambo yaliyo kuwa ya kuchukiza yanageuka na kuwa ya kupendeza na kukubalika. Ili kukabiliana na athari hii, basi tunapaswa kufanya zaidi ya kuchagua jumbe tunazopokea na kujiepusha kabisa na picha za aina yoyote zinazozua tamaa.


Kuwezesha washiriri kuelezea maana ya ponografia.

1. Gawa kundi hilo katika vikundi viwili, moja likiwa la wanawake jingine la wanaume. Kisha wajadiliane na uwaambie waandike jinsi wanavyoelewa neno “ ponografia”.

2. Waonyeshe wasichana majibu ya wavulana, na wavulane wayaone majibu ya wasichana pia. Waonyeshe sasa mitazamo tofauti kati ya wavulana na wasichana au uiongelee baadaye wakati warsha inaendelea. Mitazamo tofauti inayowezekana.
| WAVULANA | WASICHANA |
| Kuiangalia ni kawaida | Wavulana au watu wenye matatizo ndio wanaangalia ponografia |
| Kwa ujumla inavutia | Inachukiza japo unataka kujua ni nini |
| Unaweza kuijadili na marafiki zako | Ni siri ambayo huwezi kumwambia mtu yeyote hata rafiki wa karibu |
Ufafanuzi:


Kuwaonyesha washiriki jinsi ponografia hutengeneza na kuimarisha njia ya neva ndani ya ubongo.
1. Kwa kutumia udongo wa mfinyanzi tengeneza umbo la ubongo na uushike mikononi mwako ukiwaelekea washiriki.
2. Waeleze kwamba kila tunapokuwa na tukio, njia ya neva inaundwa kwenye ubongo. [Tumia kisu cha plastiki kutengeneza njia kwenye udongo.]
3. Ikiwa tukio lina manufaa, ni rahisi ubongo kupendelea tukio hilo. [Eleza kwamba kama maji yatamiminwa kwenye ubongo, ni rahisi maji hayo kufuata njia ambayo tayari imeishatengenezwa.]
4. Tunapochagua tukio hilo tena, njia iliyokwisha tengenezwa inapanuliwa zaidi. [Tumia ukingo wa kisu cha plastiki kuipatia njia kina zaidi.]

Wakumbushe washiriki kuwa ponografia SIO uhusiano dhabiti wa undani.

Kwa sababu lengo lake kuu ni kuzua tamaa ya ngono, inadhuru ndoa na mahusiano dhabiti.

Watu katika tasnia ya ponografia mara nyingi ni wale wanaonyonywa. Tasnia ya ponografia inahusishwa na ukahaba na biashara ya kuwauza binadamu ili kuwatumia kingono. Kwa kulipia na/au kutazama ponografia, inahimiza unyonyaji na madhara ya wale walio katika tasnia hiyo.

Wataalamu wanasema kuwa picha za ashiki ambazo zinaweza kuchukuliwa bila uzito wowote zinapochapishwa kwenye magazeti, zina uwezo wa kumfanya mtu kutawaliwa na kuwa mraibu wa ponografia. Hatimaye mtu huyo anaweza kuwa mfuasi sugu wa mambo ya ponografia ambayo yanapatikana kwa wingi na kwa urahisi kwenye mtandao.
Mtu anapokuwa na mazoea ya kutazama picha za kuamsha tamaa, anakuwa na uchu wa kutaka kuzitazama kila mara. Mara nyingi, waraibu hawa hupata msisimko na kilele chake huwa ni aina ya utulivu na amani inayopatikana baada ya aina fulani ya homoni (serotonin) kutolewa. Hali hii ya kupata punyeto au kujichua ndio humfanya mtu kuirejelea kutazama picha hizi za ashiki mara kwa mara.
Baada ya muda fulani, uraibu wa kisaikolojia hubadilika na kuwa uraibu unaoathiri mtu kimwili. Hii ni kwa sababu uraibu wa picha za ngono hufanya kazi kwa njia sawa na uraibu wa dawa za kulevya. Wakati dawa za kulevya husisimua mtu na kumpa furaha ya aina fulani, ponografia huanzisha utoaji wa homoni ambayo inaleta furaha ya aina yake. Iwapo hali hii itarudiwa mara kwa mara, mtu anaweza akawa na uraibu wa kemikali za kusisimua akili yake. Muathiriwa mara kwa mara hutamani kupata msisimuko wa juu kama tu vile mraibu wa dawa za kulevya hufanya, na anataka kurejelea kuona picha za kuzua ashiki. Hii ndio sababu inakuwa vigumu kwa mraibu wa picha za ngono kuacha kuzitazama licha ya kuwa na nia kuu ya kuacha tabia hiyo.
Zaidi ya hapo, kuzoea picha za ngono huleta tabia ambayo huathiri mtu kisaikolojia ambayo inachangia kukosa hisia. Kama tu vile wanasaikolojia wanaweza wakamsaidia mteja wao kuacha tabia ya kuogopa wadudu kwa kumleta mara kwa mara karibu na wadudu kama vile buibui , mtu aliye na uraibu wa picha za ngono ataanza kukosa mnato anapotazama picha hizo na kuzichukulia kuwa dhaifu. Licha ya picha hizo kuwa na uwezo wa kusisimua mtu kiashiki, mraibu wa picha hizo ataanza kuzichukulia kama za kawaida. Ili kupata msisimuko sawa na aliyokuwa akiupata alipoanza tabia hiyo ya kutazama picha za ngono, itambidi atafute fasihi iliyo na picha za mvuto zaidi, kama kifungo na usagaji (BDSM) ponografia, ngono na wanyama, au ngono ya kulazimishwa kwa wanaoshiriki. Wakati mwingine mraibu anaweza kuenenda katika uzoevu wa starehe hizo kama jambo dhahiri maishani mwake.

Ponografia ina mathara kwa mwili na akili kisaikolojia. Aidha ina athari kwa hisia na uhusiano. Ngono ni zawadi ambayo bibi na bwana huhifadhiana ili wazawadiane katika ndoa baina ya mke na mume mmoja. Ponografia na aina nyengine za tamaa huichukulia ngono kama kitu cha kunyakua kutoka kwa mwengine. “Kunyakua” huku badala ya “kutoa” kunaweza kusababisha unyanyasaji, maumivu moyoni, na taabu.

Ponografia inadunisha watu na kueneza dhana kuwa binadamu hana utu bali ni chombo kinachoweza kutumiwa kujipatia anasa. Mara nyingi, wanawake husawiriwa kama vyombo vya kutumiwa na kudhulumiwa kwenye ngono ambavyo hutupwa baada ya shughuli hiyo. Wanaume kwa upande mwingine huchukuliwa kama vyombo vinavyoendeshwa na tamaa.
Mfano:


Mara nyingi watu wanaohusudu ponografia huwa pweke na kukatishwa tamaa na mahusiano yao. Tendo hili laweza kulinganishwa na kutafuna kitu unachokienzi kwa minajili ya utamu wake tu kisha baadaye ukakitema.
Uraibu wa ponografia hauridhishi kwa sababu binadamu aliumbwa kuwa na uhusianao wa kindani na wetu wengine. Lakini kutazama ponografia kunashirikisha picha za mtu mmoja pekee ambaye hana uhusiano wala hawezi kunyoosha hisia zake kwa yule anayemtazama. Hali ya upweke huwatawala sana wapenzi wa ponografia kwa sababu picha hizi za ashiki huchangamsha kitengo cha akili na miili yao vilivyokusudiwa kuwa na uhusiano na watu wengine. Hatimaye waraibu hao wa ashiki hufungia ndani hisia zote za mapenzi zinazokusudiwa kuonyeshwa kwa watu wengine. Ni kutokana na haya ambapo watu ambao hujichangamsha na ponografia wanapaswa kujiepusha na haya na kujumuika na watu na marafiki halisi wanaowajali- Huu ndio mshikamano wanaoukosa!
Katika ponografia, kunakosekana uhusiano wa kindani wa dhabiti baina ya watu halisi, unaopatikana katika uhusiano dhabiti na uliojengwa kwa misingi ya maadili. Uhusiano wa kindani wa kweli haubagui wapendanao kwa misingi ya kasoro za kimaumbile.
Mfano:

Kwa ufafanuzi wa kamusi, kupiga punyeto kunahusisha kujisisimua kimakusudi kwa madhumuni ya kupata furaha ya ngono kwa ajili yako mwenyewe na ukiwa peke yako.
Kupiga punyeto ni shughuli ya ngono, ingawa si kujamiiana yenyewe, lakini inaweza hatimaye kusababisha kujamiiana.
Zaidi ya 95% ya wanaume na karibu 50% ya wanawake wamepiga punyeto. Kwa sababu kitu kimefanyika na wengi/kinajulikana haimaanishi kuwa ni cha manufaa/kizuri kwetu kila wakati. Kwa mfano, hata kama watu wengi wanatupa takataka au kuvuta sigara, hilo bado halitafanya kutupa takataka au kuvuta sigara kuwa kitu chenye manufaa kwetu au kwa jamii.
Kwa sababu ya kutokea kwa wingi miongoni mwa wanaume, punyeto huwa ni tatizo la wanaume zaidi kuliko wanawake.
Masafa: Akili zisizo na kazi husababisha mikono isiyofanya kazi, na wengi ambao walianza tabia ya kupiga punyeto walifanya hivyo wakati hawakuwa na chochote (bora) cha kufanya (yaani, bila kazi). Ingawa hakuna kitu kibaya kuhusu kitendo chenyewe, kinaweza kuwa tabia inayosababisha uraibu wa ngono.
Motisha/Kusudi: Ni kwa ajili ya kujiridhisha tu. Kupiga punyeto kunaweza kuwa tatizo ikiwa mtu anajishughulisha mara kwa mara au kwa madhumuni ya ubinafsi. Hii inathiri vibaya uwezo wa mtu wa kuhusiana kwa karibu na mtu mwingine; inachukua nafasi ya uhusiano wa undani na wa kweli.
Kuoanisha: Kupiga punyeto mara nyingi huambatana na ponografia. Watu wanaopiga punyeto kwa kawaida huangalia ponografia, ndoto za ngono au majaribio ya ngono (ambayo yanaweza kukengeuka kadiri uraibu unavyoongezeka). Kupiga punyeto ni mteremko unaoteleza ambao huongeza tu tatizo la uraibu wa ponografia. Kiasi cha ponografia kinachopatikana kwa urahisi kwa vijana leo kinastaajabisha akili na kinaweza kumwangamiza mtu kupitia uraibu. Inaweza kumfuata mtu katika maisha yake yote, kuathiri mahusiano, maamuzi na amani yake.
Kupiga punyeto huathiri jinsi ulivyo kama mtu kwa sababu kile tunachokifanya na miili yetu ni vigumu kukitenganisha na utu wako.


Kuelewa namna ponografia huathiri mahusiano yetu kwa njia isiofaa.
1. Weka ndoo ya maji kwenye hema ambalo limetandazwa chini au kwenye sakafu ambayo haiwezi kudhuriwa na maji. Waulize washiriki wanachodhani kitatendeka iwapo utatupa mawe kwenye ndoo hiyo.
2. Tupa mawe kadhaa kwenye maji hadi maji yaanze kumwagika.Waambie ya kwamba mawe yanawakilisha picha za ponografia, ndoo inawakilisha mawazo yao, na maji ni mtazamo wao “msafi” juu ya mahusiano ambao haujapotoshwa.
3. Elezea kwamba kama vile mawe yanapozama chini ya ndoo, yanalazimisha maji kumwagika nje. Vile vile tunapotazama picha za ngono, zinazama katika mawazo yetu na kutufanya kupoteza ubikira wetu wa kimawazo kutokana na maswala ya ngono, hali hii aidha inaathiri uhusiano wetu na wenzetu wa jinsia tofauti.
4. Endelea kuongeza mawe zaidi katika ndoo ya maji. Kila jiwe husababisha tone la maji kumwagika, kama vile picha za ngono zinavyotufanya kupoteza usafi wetu katika mtazamo wetu.
5. Acha kuongeza mawe. Uelezee washiriki kwamba hata unapoacha kutazama picha za ngono zile picha ambazo uliona hapo awali zina mnato mkubwa na uwezo wa kusalia kwenye mawazo kwa kipindi kirefu. Huwezi kuzifuta kutoka akilini kwa urahisi. Wala usafi wako wa mawazo kuhusiano na maswala ya ngono hauwezi kurejeshwa tena baada ya kuchafuliwa na picha za ngono, kama vile maji yaliyomwagika ambavyo hayawezi kurudi kwenye ndoo.
Kwa bahati mbaya, picha hizi za ngono hubadilisha mtazamo wetu wa mahusiano na zinakwama akilini mwetu, hivyo basi kuathiri mahusiano yetu ya baadaye. Kile kinachoweza kuchukuliwa kama uamuzi wa mtu binafsi kinaweza kumuumiza mtu mwingine vibaya sana.
Kwa wale ambao wanakabiliwa na athari za uraibu wa maswala ya ponografia, elewa kwamba haupaswi kuficha swala hili. Ni jambo la busara kuchukua hatua bila kuyumbayumba ili kujinasua kutoka kwenye minyororo ya uraibu huu , haijalishi kiwango cha uzito ambacho uraibu huu umekuathiri.

1. Kubali - Uwe jasiri na ukubali ponografia ni tatizo
Kukubali tatizo ni hatua ya kwanza ya mabadiliko. Unaweza kujihatarisha ukakamatwa au
ukapoteza sifa yako, lakini uraibu wa aina yoyote—hasa ngono—si jambo la kuchukulia kirahisi.

2. Badilika – Kubadilika kwa ujumla
Jitahidi kudhibiti nyanja mbalimbali za maisha yako kama vile mwili, akili, hisia na imani na
uhakikishe kwamba viungo hivyo vyote vina mshikamano.
3. Uwajibikaji - Chukua hatua madhubuti
Iwapo una matatizo kuacha hii tabia licha ya kukusudia kuiacha, pata msaada! Zungumza na
mzazi au mshauri wa kitaalamu- kujadili swala hili kutasaidia kuondoa aibu na siri iambatanayo
na tabia hii. Kujitenga hakutasaidia kwani kutaongeza hali ya uraibu. Wengi wamepambana na
swala hili hakuna haja ya kujificha. Unaweza kujiondoa katika mtego wa tabia hii na athari zake
dhidi yako.

Chukua hatua madhubuti kukatisha na kusimamisha tabia hii isiendelee kukolea na kuzama ndani yako na kukita mizizi kabisa. Hatua ambazo unapaswa kuchukua ni pamoja na:

Bila kujali kama umejihusisha na ponografia, unaweza kuuwasha ubongo wako uanze upya ili kuepuka matokeo mabaya ya ponografia.
Ikiwa umekuwa katika tabia hizi kwa muda, usikate tamaa. Jambo lile lile lililosababisha ubongo wako kuwa na mazoea ya kutazama ponografia linaweza kukusaidia pia kutoka.
Kila wakati unapofanya chaguo la kutotenda kulingana na tabia hizi, unadhoofisha njia katika ubongo wako ambayo ilikufanya uvitake vitu hivi.
Kwa hiyo kadiri unavyochagua kutotazama ponografia mara nyingi zaidi, ndivyo itakavyokuwa rahisi kwako kujiepusha na mazoea haya.

Tambua vichochezi vyako
“Ripoti”: Mwambie mtu unayemwamini
Waambie washiriki:
Jiulize: Je, kuna njia nyingine za kuvunja mzunguko wa vichochezi vyangu?
Jiulize: Je, kuna njia bora na yenye afya zaidi ya kukidhi hitaji hili?
Linda tabia zako za kiafya ili kujikinga na nyakati za udhaifu. Uwe na mazoea ya kuacha mlango wako wazi au angalau ukiwa umefunguliwa. Jijengee mazoea ya kutumia vifaa vyako vya rununu na dijitali ukiwa sebuleni au maeneo mengine “ya umma” nyumbani. Sakinisha vichungi kwenye simu mahiri na kompyuta ya mkononi,

Uwe mtumiaji mwenye busara! Usiruhusu vyombo vya habari kuamuru maisha, maadili na uhusiano yako. Linapokuja suala la vyombo vya habari:

Tunapokuwa watu wa kupokea tu jumbe kutoka kwa vyombo vya habari, tunaruhusu ujumbe wa kila aina katika akili zetu pasipokuwa na msimamo au uwezo wa kuzichuja, na namna ya kuzichukulia. Kwa mfano baada ya shughuli za siku nzima, sisi hutaka kurudi nyumbani na kujituliza mbele ya runinga. Kwa msingi sisi huketi chini na kuruhusu runinga ituzungumzie pasipokufikiria kuhusu ujumbe husika na namna unavyoathiri mtazamo na imani yetu.
Kuwa mtazamaji shirika, kunaanza na kuelewa jinsi tunavyoathiriwa na jumbe za vyombo vya habari na kisha kutenganisha (kuchuja) ujumbe mzuri kutoka kwa ule mbaya. Tunaanza kutambua jinsi vile matangazo ya biashara hutuchukulia, au maoni ambayo kipindi kinataka kuleta kwa mtazamaji, na kutathmini jinsi ujumbe huo unavyokubaliana au kutofautiana na misimamo na maadili yetu. Kisha tunaanza kuamua iwapo ujumbe husika ni wa ukweli au ni maoni yaliyopotoshwa na lengo la kumhadaa msikilizaji.
Si kwamba yote ambayo yamo kwenye vyombo vya habari ni mabaya.Jambo kuu ni : Ni nani anayesukuma mkokoteni?Je uko katika mkokoteni ukisukumwa hapa na pale, ukiruhusu vyombo vya habari kukuelekeza kiimla namna unavyofikiria au kukuamrisha kuhusu ni nini unapaswa kufanya? Au je, wewe unasukuma mkokoteni ukielekeza ujumbe huo kulingana na ule ujumbe ambao una uruhusu uje maishani mwako?
Teknolojia na vyombo vya habari ni nguvu ya manufaa tu wakati inaposimikwa na kuungwa mkono na maadili mema na chanya.

Mzazi mpendwa,
Katika Hakuna Majuto® Kitengo cha 2, tulijadili athari za vyombo vya habari katika utamaduni wetu.
Vyombo vya habari vichache sana huonyesha vijana ambao hawashiriki tendo la ndoa kwa mtazamo chanya. Ngono inauzwa, na vyombo vyetu vya habari huiuza wakati wote. Vijana wamezingirwa pande zote na jumbe za ngono. Kujaribu kuchuja jumbe hizo ni changamoto kwa vijana wanaokulia kwenye utamaduni huu.
Vijana walijifunza [GA 10] katika Kitengo cha 2 jinsi ya kukuza utambuzi kupitia kutathmini maneno, vipindi vya televisheni na filamu kutofautisha jumbe nzuri na zile zisiofaa. Pia walitathmini matangazo ya biashara na majarida ili kufuatilia jinsi utangazaji ambavyo hutegemea mvuto tofauti wa kihisia.
Kitengo hiki huwasaidia vijana wanaobalehe kuelewa kwamba kuweka mipaka ya kihisia na kimwili huleta uhuru wa kweli na ni muhimu katika kujenga mahusiano bora.
Kuwawezesha wanaoshiriki kuelewa umuhimu wa kuweka mipaka katika maisha yao – mipaka wanayoweka leo ina umuhimu kwenye maamuzi yao siku za usoni na kuna athari iwapo mipaka iliyopo haitazingatiwa vizuri. Mipaka inapashwa kutegemea maadili yetu na yale mambo ambayo ni muhimu kwetu.
Katika kitabu chao kinachohusu mipaka wakati wa uchumba , Daktari Henry Cloud na Dr John Townsend waliandika, ‘”Mipaka ina umuhimu na majukumu mawili. Kwanza, mipaka inatutambulisha kwamba tuko watu wa namna gani kwa yale tunayo kubaliana nayo, tusiyoyakubali, tunayoyapenda na tunayoyachukia.”
Tunawezakosa kujieleza kwa kina mbele ya marafiki, lakini wakati wa mazungumzo baina yetu, mahali ambapo mipaka ipo ama haipo panajieleza wazi na kuwaonyesha sisi ni watu wa hulka ipi. Ninapochagua kujiusisha katika tukio fulani, ninaonyesha kwamba ninakubaliana na matendo, maadili na hisia zinazoambatana na hilo. Kinyume chake, ikiwa ninakataa kabisa kutoshiriki katika mdahalo huo ni dhahiri ya kutofurahia matendo, maadili na hisia zinazoambatana na yale yatakayo afikiwa. Kwa mfano, ninaamua kushiriki katika michezo, kwa sababu ninaamini inasaidia kuishi maisha yenye afya bora na kufurahia uzima; ninakataa kujiunga wakati marafiki zangu wanapowadhihaki wengine, kwa sababu watu wanafaa kuheshimiwa jinsi walivyo na wasidharauliwe kutokana na maumbile yao, ulemavu, ama kasoro zao.
Dr Henry Cloud na Dr John Townsend pia wameandika, “Kazi ya pili ya mipaka ni kwamba inatulinda. Mipaka inahifadhi mambo mazuri na mambo mabaya yanawekwa pembeni. Tunapokosa kuwa na mipaka iliyo dhahiri, tunaweza jiusisha na vikundi vya marafiki wasio na tabia nzuri … Mipaka inawatambulisha wengine kama utalikubali hilo ama laa.”
Kukiwepo mipaka inajidhihirisha wazi kama unatendewa wema ama kuhusishwa na mambo yasiyo mema, na hilo litachangia ni maamuzi yapi utakayochukua katika kujilinda na hilo. Bila mipaka, itakuwa vigumu kwako na kwa wengine kujua ni ni lipi linalofaa na linalokubalika. Mara nyingi, watu ambao hawana mipaka iliyo wazi wanakerwa pasipo wao kufahamu ama linawapata ghafla.
Unapokuwa umeweka mipaka, unaweza kufanya maamuzi yaliyo mema, kwa mfano uhusiano kati ya msichana na mvulana, na umbali ambao mtakaribiana katika uhusiano huo?
Mipaka isipokuwepo mnaweza kuangukia katika vitendo ambavyo mtajutia baadae, ama kujikuta katika majukumu ambayo bado hamko tayari kuyashughulikia. Kinyume na hilo mipaka inakuletea uhuru zaidi wa kibinafsi- kuchagua- badala ya kuruhusu marafiki, homoni, na matokeo kukuchagulia.
Katika kitabu chake Boundaries, Where to Draw the Line, Anne Katherine aandika, “kwa kila tukio, sisi huonyesha kwamba tutalinda kile tunachothamini au kwamba tutajitoa. Mipaka yenye afya huhifadhi uadilifu wetu. Tofauti na ulinzi, unaotutenga na utu wetu wa kweli na wale tunaowapenda, mipaka huchuja madhara.”


Wasaidie washiriki kutambua maadili yao ya binafsi kwa sababu yanaathiri maamuzi yao na uwezo wao wa kuweka mipaka yenye afya maishani.
Tumia kipande kimoja cha karatasi kuandika na kubainisha yafuatayo:


Kila shughuli, mtu, lengo, milki unayopenda na kitu cha kumiliki siku moja, viandikwe kwenye kipande tofauti cha karatasi.
Kabla ya kuanza, waambie washiriki waviweke vipande vyao vyote vya karatasi juu ya meza zao.
Waambie washiriki utakuwa unasoma hadithi fupi. Baada ya kila sehemu ya hadithi, wataombwa kufanya uamuzi na watapewa sekunde 10 kufanya hivyo.
Soma hekaya iliyopo hapa chini kwa sauti, kila baada ya kitengo (sehemu) nyamaza kwa sekunde 10 ili kuwaruhusu washiriki kufanya uamuzi ni kipande kipi cha karatasi watakachochagua kutupa kando. Karatasi iliyotupwa lazima ikunjwe au kuchanwa.

MARA MOJA . . .

1. Ulienda kwenye mbuga za wanyama na kuumwa na aina ya mdudu adimu. Unaanza kujisikia kuwa mgonjwa, na daktari wako anagundua kuwa una ugonjwa mbaya sana. Hana uhakika jinsi ya kukutibu na pia hana uhakika kama ugonjwa huo unaua. Anasema ni lazima uache MOJA ya shughuli zako unazozipenda.

2. Umelazwa hospitalini kwa muda mfupi kwa sababu ya ugonjwa wako. Lazima uache MOJA ya malengo yako.

3. Kwa sababu ya kutokuwepo kazini kwa muda mrefu, huna pesa na huna budi kuacha MOJA kati ya vitu/mali zako unazozipenda.

4. Unahitaji kulazwa hospitalini tena kwa sababu ya ugonjwa mbaya wa kuambukizwa. Malipo ya matibabu ni makubwa sana na inabidi utoe MOJA ya vitu/mali zako nyingine uzipendazo.

5. Unajaribu kuendelea na kazi yako lakini umechoka kutokana na ugonjwa wako. Unapoteza MOJA ya malengo yako na lazima uachane na MOJA ya shughuli zako nyingine. Pia, kwa sababu sasa huwezi kudumisha mahusiano, watu WAWILI muhimu wametoka maishani mwako.

6. Ugonjwa wako unazidi kuwa mbaya na unapaswa kulazwa hospitalini moja kwa moja. Unaruhusiwa kuwa na mgeni (mtu) MMOJA tu na unaweza kuchukua kitu KIMOJA pekee unachokipenda hospitalini. Tupa watu WAWILI muhimu, kitu/mali MOJA unayoipenda na kitu kimoja ambacho ungependa kumiliki siku moja.

7. Daktari wako ameipata hospitali moja nje ya nchi yenye utaalamu wa kutibu walioumwa na wadudu nadra. Unahamia huko maisha yako yote ili kuishi karibu na hiyo hospitali, iwapo utapata dalili za ugonjwa tena. Lazima utoe karatasi zako TATU kati ya zilizobaki. Zitakuwa ni nini?

8. Unaanza maisha yako upya na mtu huyu tu, lengo, shughuli, mali au kitu ambacho ungependa kumiliki siku moja. (vipande 2 vya karatasi vimesalia)

ULIZA: Je, kuna baadhi ya uchaguzi uliokuwa mgumu zaidi kuufanya?
Maadili yetu yanapokuwa wazi, yanaweza kutusaidia kujibu maswali haya magumu sana:
Mifano ya kuwa na maadili fulani:
Toleo la dijitali la shughuli hii linaweza kupatikana hapa.


Wasaidie washiriki kutambua jinsi maadili yao yanavyoathiri maamuzi wanayoyafanya.
Waambie washiriki utasoma mfululizo wa chaguzi mbalimbali nao wanahitaji kuamua ni chaguo lipi katika hayo wanalolipendelea. Wanaweza kuonyesha chaguo lao kwa kusimama kama wanapendelea chaguo katika safu X, na kukaa chini kama wanapendelea chaguo kutoka safu ya Y. (Kwa kipindi cha mtandaoni, wanaweza kutumia majibu ya “dole gumba” kwa safu X na “makofi ” kwa safu Y).
Je ungependa X au Y:
| X | Y |
| Tumia Spotify | Tumia Netflix |
| Tumia Instagram | Tumia TikTok |
| Kuwa jukwaani | Kuwa katika hadhira |
| Poteza funguo za nyumba yako | Poteza simu mahiri |
| Kuwa mwanamichezo | Kuwa msanii |
| Fanya kazi katika kikundi | Fanya kazi peke yako |
| Kukwama kisiwani na mtu ambaye hawezi kuacha kuongea | Kukwama kisiwani peke yako |
| Kuwa na marafiki wengi wa wastani | Kuwa na rafiki mmoja mzuri sana |
| Kumuoa mwenzi unayempenda sana (mtu wa ndoto zako) | Uwe na kazi unayoitamani sana (ndoto yako) |
| Kuwa na muda na marafiki | Kuwa na muda na familia |
| Uwe na afya njema lakini maskini | Uwe mgonjwa karibu ya kufa lakini uko tajiri |
| Watu wafurahie matendo yako mema | Watu wakuheshimu kwa uwezo wako |
Wawezeshaji wanapaswa kujumuisha yale yanayofaa na maarufu katika nchi yao.
ULIZA: Je, kuna baadhi ya uchaguzi uliokuwa mgumu zaidi kuufanya?
ULIZA: Tunapata wapi maadili yetu?
Ni lazima kufikiria kwa makini ili kuweka mipaka yenye afya na kufanya maamuzi mazuri.


Wasaidie washiriki kuelewa mipaka – kujifunza kwamba mipaka inatambuliwa kibinafsi na maamuzi ya kipekee yanafaaa kuheshimiwa.


1. Elekeza “A” Kuchukua hatua moja baada ya nyingine kuelekea “B”na kusimama karibu na “B” karibu iwezekanavyo hadi “B” atakapoinua mkono kuomba asimame. “B” pia anaweza kumuomba “A” kurudi nyuma ikiwa anahisi kuwa “A” amekuwa karibu sana.
2. Umbali wa mwisho kati ya “A” na “B” unaashiria mipaka ya nafasi ya kibinafsi ya “B”. Unaweza kutumia mkanda unaonata kuashiria umbali lakini waambie wabakie kwenye nafasi zao.
3. Uliza kundi “B”: Je, ungejisikiaje ikiwa “A” atachukua hatua nyingine karibu nawe baada ya wewe kuinua mkono wako? Kwa nini?
4. Elezea kwamba “umbali salama” huu unatenganisha kile kinachojulikana kama “nafasi ya kibinafsi” ya mtu. Ni mpaka ambao kila mtu amejizungushia.

Mipaka inatutambulisha...


5. Waombe washiriki kuangalia na kulinganisha umbali uliopo kati ya kila jozi; kwa kawaida umbali unapaswa kuwa tofauti. Watu wengine wanahitaji nafasi zaidi; wengine nafasi ndogo, lakini kila mtu ana hitaji la nafasi ya kibinafsi na hii inapaswa kuheshimiwa.
Hatua hiyo, ina ambatana na mambo mengine, tunaweza amua kuweka mipaka kuambatana na lipi litatufaidi na sio jinsi tunavyo hisi.


ULIZA: Je, ni vikwazo gani unakumbana navyo wakati wa kuweka mipaka bora?
Majibu yanayowezekana:


Je, ni njia zipi za kushinda vikwazo hivyo?
Majibu yanayowezekana:
Maisha na mahusiano yanaweza kuwa ya kusumbua zaidi bila mipaka. Kuwa na uhakika wa maadili yako na kuweka mipaka yako ili kuyalinda.


Wasaidie washiriki kuona ya kwamba Mipaka inaweza kuonekana kama inakuzuia mambo mengi bali itakuwezesha kuwa huru zaidi.
1. Weka ngamba yenye maneno “Unapokataa” jambo hili leo … “unalikubali” jambo jingine siku zijazo.
2. Shikilia kichungi (faneli) juu mbele ya darasa ukielekeza upande wenye ncha pana.
3. Uliza: “Ni wangapi wenu kati yenu wanapenda uhuru? – hamna masharti; unaweza kutenda unalotaka.”
4. Inua faneli tena lakini uelekeze kwenye ncha nyembamba.

Mipaka ➡️Uhuru.

Badala ya kutuwekea vikwazo, huleta uhuru wa:

Huenda mipaka isivutie kila mara lakini hutulinda.
Kufahamisha washiriki kuwa ni rahisi kujikuta kwenye mtelemko mkali unaoteleza na wakajikuta mahali pabaya iwapo hawataeleza kwa uwazi mipaka yao waliyoweka kuhusu tabia hatarishi.
Kwa njia moja ama nyingine, tayari tunaweka mipaka katika maisha yetu. Kwa mfano tunaweka mipaka inayozunguka vitu vyetu, twaweza kutambulisha mipaka kama “chumba changu cha kulala na vilivyomo ndani yake ni vyangu- nafurahi mama yangu akichukua nguo zangu ili kuzifua lakini sitaki aanze kupanga upya chumba changu.”
Kuna mipaka mingi ambayo inaweza zingatiwa maishani, na kweli kadiri ya mipaka inayofaa tunayoiweka, ndivyo tunavyojifungulia milango ya maamuzi mengi zaidi siku zijazo.


Wasaidie washiriki kutafakari juu ya maadhara ya tabia hatarishi na hitaji la kuweka mipaka.

1. Gawa darasa lako katika vikundi vidogo (Kipindi cha mtandaoni: Gawa darasa katika vyumba vya vipindi vifupi)
2. Kipatie kila kikundi tabia hatarishi
3. Waombe washiriki kujibu maswali yaliyo hapa chini, nakili hoja zao kwenye ubao mweupe kulingana na tabia zao hatarishi. (Kipindi cha mtandaoni: Mteue mtu wa kuandika majadiliano)
Ni pombe aina ipi unayofahamu?
Je, nakili jina la pombe inayotambulika kote na wengi>inayo asilimia ngapi ya pombe?
Je pombe inakuwezesha kuhisije?
Je umri upi ni halali kununua ama kunywa pombe?
Baadhi ya madhara ya unywaji wa pombe kupindukia ni nini?
Ni kwa nini watu hunywa pombe?
Ni mihadarati ipi unayofahamu?
Je madawa ya kulevya yanamfanya mtu kujisikia namna gani?
Je ni halali kutumia mihadarati?
Baadhi ya madhara ya dawa za kulevya ni yapi?
Ni kwa nini watu hutumia dawa za kulevya??
Ni kemikali sampuli ngapi zinapatikana kwenye sigara?
Ni kemikali ipi inayosababisha uraibu wa uvutaji sigara?
Unastahili kuwa na umri upi ili ununue sigara?
Ni nini baadhi ya madhara ya kuvuta sigara?
Ni kwa nini watu huvuta sigara?
Kamari ni nini?
Je, kucheza kamari ni halali?
Watu hucheza kamari wakitumia vitu gani?
Ni yapi baadhi ya madhara ya kucheza kamari?
Kwa nini watu hucheza kamari?
4. Sahihisha kwa makusudi (na kwa upole) mitazamo isiyo sahihi, na utie mkazo taarifa sahihi.
5. Sisitiza kwamba orodha ya maswali inaisha na swali la kwa nini. Kwa nini watu wanajihusisha na tabia hatarishi :
Kwa nini watu wanajihusisha na tabia hatarishi?
6. Elezea kwamba kuweka mipaka mizuri sio tu kuhusu kile wanachokihisi wao kwamba ni sawa; ni kufanya uamuzi makini wa jambo lililo sahihi kwao wenyewe na kwa wengine, bila kujali jinsi wananavyojihisi, na kuzingatia uamuzi huo.


Pombe husababisha hisia tofauti kutoka katika tamaduni mbalimbali. Katika mataifa mengine kama vile Brunei ama Saudi Arabia pombe imepigwa marufuku kabisa, wakati nchi nyingine pombe ni sehemu ya urithi wa utamaduni wao kwa mfano nchini Ujerumani (bia) na Ufaransa (mvinyo).
Hata hivyo’ mataifa mengi yameweka kiwango cha unywaji wa pombe miongoni mwa vijana kupitia sheria ya kuwadhibiti. Kwa mfano taifa la Norway halina sheria inayolenga umri unaoruhusiwa unywaji pombe japo, lazima anayetumia awe na miaka kumi na minane ama ishirini ikitegemea na aina ya pombe. Kwa upande mwingine nchini Kanada, umri wa kunywa na kununua pombe ni miaka 18 au 19 (kulingana na sheria za mkoa), ingawa unywaji wa pombe chini ya uangalizi wa wazazi wao unaruhusiwa.
Sheria hizo zipo, vijana wanashiriki mvinyo kupitia njia zisizo tambulika kisheria ama kwa kukwepa macho ya wenye maduka au kupata usaidizi kutoka kwa wenzao wakubwa ambao wanaweza kununua pombe.
Sumu iletwayo na pombe hutokea wakati kiasi kikubwa cha pombe kimebugiwa katika muda mfupi. Hilo hutendeka wakati mtu anapokunywa pombe kupita kiasi katika kikao kimoja mara moja kila wiki mbili.
Kunywa pombe kupita kiasi ni jambo la kawaida na si kwa vijana tu. Kunywa pombe kupita kiasi kunaweza pia kusababisha midundo ya moyo isiyo ya kawaida, ambayo inaweza kusababisha kifo.
Wakati mtu anapokunywa pombe kupita kiwango, inaanza kuathiri ubongo hasa katika eneo ambalo husababisha mwanadamu kufikiri na hivyo kuathiri hisia na uwezo wa kuwaza, msukumo wa misuli hali ya mapenzi na njia za haja ndogo pia uathirika.
Kitengo cha mwisho kuathirika na pombe ni kitengo kinachoongoza mapigo ya moyo mwilini [medulla], hatimaye kipimo cha joto mwilini na kupumua. Inapofika hatua hiyo mtu anahisi usingizi na iwapo ataendelea na unywaji wa pombe, anazimia na vitengo muhimu vya mwili vinaacha kufanya kazi na hilo linaweza kusababisha kifo.
Japo utafiti umebaini kwamba pombe inaweza kuwa na manufaa kwa moyo, utafiti huu unaonyesha kuwa ni wale wanaotumia pombe kwa wastani, na ni miongoni mwa wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka arobaini na wanawake ambao wamepitisha umri wa kujifungua. Manufaa hayo yanaweza kupatikana kupitia kufanya mazoezi, na lishe bora. Zaidi ya kizingiti fulani, unywaji wa pombe huwa sababu ya kuathiri moyo na husababisha magojwa ya moyo.
Unywaji pombe kupindukia kunaathiri moyo. Kunywa pombe kiasi kingi mara kwa mara kunaweza kusababisha kupanuka kwa moyo. Hali hii husababisha ugumu wa kupumua wakati wa mazoezi na jambo hili litahitaji matibabu maalum na haliwezi kutenduliwa.
Bado haijabainika uhusiano kati ya kiwango cha pombe kinachotumiwa kusababisha maradhi ya ini. Utafiti katika taifa la Italia ulionyesha kiwango cha pombe kinapoongezeka mwilini ndivyo athari ya kupata maradhi ya ini huongezeka . Hata hivyo, uchunguzi kutoka taifa la China unaonyesha mtu anapobugia gramu ishirini za pombe kila siku anajiweka maradufu katika hatari ya kupata maradhi ya ini, lakini hatari haiongezeki mtu anapokunywa zaidi ya kipimo hicho. Hata hivyo jambo lililo wazi ni kwamba pombe huongeza hatari ya kupata maradhi ya ini.
Unywaji kwa wastani, ini linaweza kusindika pombe pasipo madhara. Lakini, utumizi wa pombe kupindukia huelemea ini na kusababisha madhara makubwa.
Kunywa kupita kiasi kunaweza kusababisha mafuta kujilimbikiza kwenye ini, na kusababisha seli kuwa duni na kudhoofisha afya ya mtu kiujumla. Ini lenye mafuta huingilia usambazaji wa oksijeni na virutubisho kwa seli za ini, na baada ya muda, husababisha seli za ini kufa. Seli hizi zilizokufa huunda tishu za makovu. Ingawa baadhi ya seli za ini zinaweza kuzaliwa upya kwa lishe bora na kutokunywa pombe, seli zilizozorota sana haziwezi kutenduliwa. Kupuuza hali hiyo kunaweza kusababisha ini kuharibika zaidi na kushindwa kufanya kazi kabisa..
Asilimia 20% ya pombe mwanadamu anayokunywa huenda moja kwa moja tumboni; asilimia 80% katika utumbo mdogo. Unywaji wa pombe kupita kiasi hudhuru utando wa viungo hivi na kusababisha maumivu na vidonda vya tumbo.
Madhara ya unywaji wa pombe katika mitazamo na kufanya maamuzi.
Mtu ambaye ameathirika na pombe, akipewa kazi fulani kufanya,
Ambacho kwa kawaida angekikataa, kwa mfano, kuwaomba watu kumi asiowajua kumbusu hapo hapo.
| TAIFA | UMRI ULIOKUBALIKA KISHERIA KUNUNUA NA KUNYWA POMBE |
| Argentina | 18 |
| Australia | 18 |
| Cameroon | 18 |
| Canada | 18 (MANITOBA, ALBERTA, QUEBEC) 19 (ALL OTHER TERRITORIES) |
| Colombia | 18 |
| Costa Rica | 18 |
| Dominican Republic | 18 |
| Ecuador | 18 |
| Misri | 18 |
| El Salvador | 18 |
| India | 18–25 (DEPENDING ON STATE LAWS) |
| Indonesia | 21 |
| TAIFA | UMRI ULIOKUBALIKA KISHERIA KUNUNUA NA KUNYWA POMBE |
| Ujapani | 20 |
| Malaysia | 18* |
| Mexico | 18 |
| Uholanzi | 16 (FOR MOST ALCOHOLIC BEVERAGES) 18 (FOR ALCOHOLIC BEVERAGES WITH >15% ABV) |
| Papua New Guinea | 18 |
| Paraguay | 20 |
| Peru | 18 |
| Singapore | 18 |
| Misri | 18 |
| Afrika Kusini | 18 |
| Taiwan | 18 |
| Thailand | 18 |
| Marekani | 21 |
[Sharia inawakataza waislamu wote kutokunywa vinywaji vya kulevya]

Mataifa mengi kote ulimwenguni yana sheria kuhusu matumizi, kumiliki, kuuza na kusafirisha dawa za kulevya na vitu vingine ambavyo sheria hairuhusu. Licha ya kutoelewana kuhusu njia bora ya kukabiliana na matumizi mabaya ya dawa za kulevya, kuna maafikiano juu ya jambo moja: Matumizi mabaya ya vileo ni tatizo na gharama katika jamii na uchumi wa nchi. Kwa mfano mwaka wa 2009, ilikisiwa dawa za kulevya ziliigharimu Uingereza karibia Pauni £16 billion mwaka huo.
Dhihirisho la hilo linatokana na maafikiano yaliyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa idara ya kupambana na mihadarati na uvunjaji sheria UNODC kujitolea kukabili swala hili. Wakati mihadarati inatumika, kemikali hiyo inaingia mwilini na inasababisha moja ya mambo mawili: mtu anaweza furahia hilo ama kujihisi vema, au kumfanya mtumiaji kujisikia kutulia ama mwenye uwezo fulani. Bila kujali athari, madawa ya kulewa udhuru ubongo.
Dawa ambazo usisimua ubongo husababisha vipokezi vya kwenye ubongo kuondokewa na hisia. Mtumiaji anahisi kama asiye na matatizo, kwamba amepanda” juu” haraka sana , baada hapo athari za dawa zikiisha, anahisi “ameshuka” kwa kasi sana kama vile alivyokuwa amepanda juu. Hata hivyo, ubongo si eneo la furaha tu, pia ni kitovu cha mantiki, hoja, na ubunifu. Pia hudhibiti hisia zetu na matendo yanayofanyika mwilini petu kama vile kuendesha moyo wetu na kupumua kwetu. Kwa hiyo kemikali yoyote ambayo inaathiiri ubongo wa mwanadamu ina madhara kwa haya yote pia.
Kwa sababu mihadarati inaathiri ubongo, pia inadhuru utendaji wa kazi, kutafakari na kuzalisha mali. Uzembe katika kampuni yoyote ile au kutokuwa makini kunamaanisha uzalishaji duni wa mali na kupungua kwa faida. Ingawaje hasara haionekani kuwa ni muhimu unapoangalia kampuni moja, wakati hasara ya makampuni yote nchini ikijumulishwa, inaweza kufikia mamilioni, ikiwa sio mabilioni ya fedha.
Wengi wanaotumia mihadarati, haswa wale walio na uraibu, huwa na afya mbaya, kwani hutumia muda mwingi kutafuta dawa hizo badala ya kujihusisha na shughuli za kiafya. Hali hii inasababisha mzigo mkubwa kutafuta tiba swala ambalo lingeepukikaa.
Mihadarati haipatikani kwa bei ya chini’. Kufuatia hali hii wengi hujihusisha na visa vya uhalifu minajili ya kupata fedha ya kukidhi hitaji lao. Ikitegemea uhalifu uliofanywa, uharibifu unaweza ukawa mdogo kiasi cha $10 kutelezeshwa kutoka kwenye pochi ya mtu hadi mamilioni ya dola, k.m., wizi katika benki au uchomaji moto nyumba ili kudai pesa za bima.Hii ni pamoja na maswala mengine ya usalama yanayosababishwa na utumizi wa mihadarati .
Ingawa gharama (katika hali ya kifedha) ya matumizi mabaya ya dawa za kulevya inaweza kupimwa kwa kiasi fulani kwa kuhesabu uharibifu wa mwili, uharibifu wa kisaikolojia na kijamii, nambari hizo hazionyeshi kikamilifu gharama halisi ya matumizi mabaya ya dawa za kulevya.
Kutokuwa na faida kazini wanaotumia madawa ya kulewa wanaweza wakajikuta wamefukuzwa kazi ama kuacha shule. Wasipokuwa na kazi au elimu wengi hujihusisha na uhalifu kama njia yao kujikimu maishani.
Mihadarati huwafanya watumiaji kuwa wakorofi sana na wenye kuudhika baada ya “safari” au kwa kukaa muda mrefu pasipo kutumia. Jambo hili linaweza kusababisha mvutano katika jamii, ukiukaji haki za watoto, na inaweza kusababisha kifo. Hali hiyo inaathiri mahusiano ya familia, jamii ambao wanakosa kupata suluu kutokana na hilo wanaweza kuamua kuhama na kusababisha kusambaratika kwa familia.
Hilo ni dhihirisho jinsi uamuzi wa mtu binafsi unavyo athiri uhusiano wake na jamii na mazingira anamoishi. Jinsi John Donne alivyosema, “hakuna mtu anayeweza kujitenga kama kwamba ni kisiwa cha pekee; kila mtu ni kitengo cha bara, liilo sehemu ya dunia, na hilo lizingatiwe.”
| ATHARI ZA MUDA MFUPI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| Hali ya kuhisi kuathirika B | Ulemavu wa kiakili D |
| Kuongezeka mpigo wa moyo, kupumua, na joto mwilini | Ugonjwa wa mtazamo unaoendelea wa maono E |
| Kufa ganzi | |
| Kizunguzungu | |
| Kupoteza hamu ya kula | |
| Mdomo kukauka | |
| Jasho mwilini | |
| Kichefuchefu | |
| Kutetemeka | |
| Kujizungumzia, maono C | |
| Kukosa uhalisia wa mambo kama vile muda |
| ATHARI ZA MUDA MFUPI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| Furaha isokikomo F | Uraibu |
| Ongezeko la matatizo ya moyo | Dalili zinazojitokeza unapotaka kuuwacha uraibu huo I |
| Kushindwa kuwa na mpangilio | Kutofaulu mambo mengi na tabia H |
| Matatizo ya kutafakari na kutatua mambo | Ugonjwa wa Mapafu - bronchitis |
| Kuathirika hali ya kuhisi | Matatizo ya kupumua |
| Kutokumbuka mambo | Saratani ya mapafu |
| Uoga F | Ubongo kuathirika N |
| Kushikwa na mshtuko F |
| ATHARI ZA MUDA MFUPI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| Kuwa na nguvu kupindukia | Uraibu |
| Kujiburudisha na kuhisi mwenye furaha | Dalili zinazojitokeza unapotaka kuuwacha uraibu huo K |
| Mwili kuwa na matatizo na vipimo vya joto mwilini J | Kupoteza uwezo wa kuwaza, kuona na kuyapanga mambo |
| Matatizo ya kutafakari na kutatua mambo | Kushindwa kulala |
| Mapigo ya moyo kuongezaka na shinikizo la damu pia. | Hisia kuchemka |
| Upotoshaji wa wakati na mtazamo | Unyogovu |
| Uwoga kupindukia | |
| Uwoga | |
| Kujizungumzia, maono | |
| Ini na figo kuathirika |
Mihemko, ikiwa ni pamoja na rangi, harufu na sauti, huonekana kuimarishwa sana, na katika hali nyingine, mitizamo ya hisi inaweza kuchanganyika katika hali inayojulikana kama sinaesthesia, ambapo mtu huonekana “kusikia” au “kuhisi” rangi na “kuona” sauti.
C. Maono haya hayawezi tabiriwa yanaweza kuwa mema ama mabaya. “Safari” nzuri ni za kufurahisha, za kusisimua kiakili na hutoa hisia ya uelewaji wa juu; kwa upande mwingine, “safari” mbaya zinaweza kusababisha vitu vya kawaida kuonekana vya kutisha na kuanzisha mawazo ya kutisha na hisia za jinamizi za kutia wasiwasi na kukata tamaa ambazo ni pamoja na hofu ya kupoteza fahamu, kifo au kupoteza udhibiti
D. Baadhi ya wanaotumia LSD wanapitia changamoto na kuudhika hali ambayo ilikuwa ya kustarehe inasababisha maumivu ya mda mrefu, na huenda ikasababisha kutoka hali ya kujifurahisha hadi majonzi. Hali hii inaweza kuwa ya mda mrefu.
E. Watumizi wa zamani wa LSD wanapitia changamoto, kuyakumbuka yaliyopita’na inaitwa “HPPD” na wataalamu. Hali hii hujirudia, na ni vigumu kubadilika kwa miaka mingi hata baada ya mwathirika kuacha kutumia mihadarati.
F. Wanasayansi wamebaini utumizi wa mihadarati waweza changia uzuri ama ubaya inategemea mazingara na huathiriwa sana na urithi, hasa wale walio na umri chini ya miaka 18.
G. Dalili unapojaribu kuacha matumizi ya dawa za kulevya ni pamoja na kuhamaki, kuwashwa, wasiwasi mkazo
H. Utafiti wa muda mrefu unabaini wanaotumia bangi miongoni mwa vijana waliopo chini ya umri wa chuo kikuu, watumiaji hawafaulu masomoni ukilinganisha na vijana ambao hawatumii. Wana tabia zisizopendeza, kukaidi mambo, uhusiano mbaya na wazazi, na kujihusisha na marafiki wanaotumia mihadarati.
I. Katika utafiti, kubaini wanaotumia mihadarati kupindukia na wanaotumia kiwango tu,watafiti walibaini wanaotumia kupindukia wanakuwa na ugumu zaidi wa kudumisha umakini, kujisajili, kuchakata na kufuatia maelezo. Hii inatokana na kuathirika kwa ubongo kwa sababu ya matumizi ya marijuana..
J. Madhara ya kimwili yanaweza kudumu kwa wiki kadhaa na kujumuisha mkazo wa misuli, kuuma meno bila hiari, kichefuchefu, kutoona vizuri, macho kusogea haraka, kuzirai, baridi kali na kutokwa na jasho.
K. Dalili za kujiondoa ni pamoja na uchovu, kupoteza hamu ya kula, wasiwasi, huzuni, hofu isiyoweza kudhibitiwa, kukosa usingizi, kupoteza udhibiti wa hisi na ukweli, na matatizo ya kuzingatia.
| ATHARI ZA MUDA MFUPI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| Kuhisi kutengwa na dunia | Uraibu |
| Kuondokewa na hisia | Dalili zinazojitokeza unapotaka kuuwacha uraibu huo L |
| Mapigo ya moyo kuongezaka na shinikizo la damu pia. | Kutoka damu puani |
| Kufa ganzi | Tatizo la kunusa |
| Kichefuchefu/kutapika | Maumivu tumboni |
| Kuchanganyikiwa | Matatizo ya kupumua |
| Kupoteza fahamu | Kitengo ya ya mkojo kuathirika |
| Matatizo kupumua | *While long-term effects seem less severe, immediate effects can lead to death. |
| Kupata shida kupumua. | |
| Kuacha kupumua kabisa |
| ATHARI ZA MUDA MFUPI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| Furaha isokikomo | Uraibu |
| Fikra zilizochanganyikiwa | Dalili zinazojitokeza unapotaka kuuwacha uraibu huo M |
| Kuwa na hali ya kuamka na kusinzia kila wakati | Kushindwa kuwajibika |
| Kushuka kwa mapigo ya moyo na matatizo ya kupumua | Kuhisi uchovu |
| Kuvimbiwa | Kuathirika kwa ngozi (mahali unapodunga sindano). |
| Mapafu, figo, na ini kuathirika |
L. Dalili hizo ni uchovu, unyogovu, kukasirika, kuwashwa na kukosa usingizi.
M. Dalili zingine ni pamoja na kukosa usingizi, macho kulia, kutokwa na kamasi, kuudhika, kuhisi mwenye mashaka, kutetemeka, maumivu mwilini, kusikia baridi kali, kutokwa na jasho mwilini, kuhara, kutapika na kuwa na tamaa kubwa sana ya kutumia mihadarati.
| ATHARI ZA MUDA MFUPI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| Matatizo ya mpigo wa moyo | Uraibu |
| Kuongezeka kwa mpigo wa damu na joto mwilini | Dalili zinazojitokeza unapotaka kuuwacha uraibu huo N |
| Mwenye fujo | Kuchanyanyikiwa hisia |
| Kuwashwa | Wasiwasi na kukasirika |
| Kuchanganyikiwa | Kuchanganyikiwa |
| Kukosa usingizi | Tabia ya kuzua balaa |
| Ongezeko la kutokuwa na usingizi | Meno kuuma |
| Kutetemeka na degedege | Kujizungumzia na maono |
| Uwoga/wasiwasi na kujutia | Matatizo ya kiakili |
| Hasira | Fikra za kujitia kitanzi |
| Kiharusi | Maradhi ya ini na figo |
| Kuathirika kwa moyo na neva | |
| Kifo cha gafla |
| ATHARI ZA MUDA MFUPI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| Kujihisi mchangamfu na nguvu | Matatizo ya mpigo wa moyo |
| Vipimo vya joto kuongezeka mwilini, shinikizo la damu na mapigo ya moyo kuongezeka | Maumivu ya kifua na/au matatizo ya moyo |
| Mwenye fujo | Maatatizo ya kupumua |
| Kuwashwa | Kiharusi |
| Kutoona vizuri | Mshtuko wa moyo na maumivu ya kichwa |
| Kujizungumzia, maono | Maumivu tumboni na kuhisi kutapika |
| Kichefuchefu | Uraibu |
| Kifo cha gafla baada ya matumizi hata mara ya kwanza | Dalili zinazojitokeza unapotaka kuuwacha uraibu huo O |
N. Dalili zinaojitokeza unapoamua kuacha ni kama vile uchovu na njaa kupindukia, wasiwasi, unyogovu, kuwashwa na kukosa usingizi.
O. Dalili zinazojitokeza unapoamua kuacha ni kama vile wasiwasi, unyogovu, hasira, hisia mchanganyiko, uchovu, kichefuchefu, kutapika na kukosa hamu ya kufanya chochote.
| ATHARI ZA MUDA MFUPI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| Kulewa | Uraibu |
| Ganzi | Dalili zinazojitokeza unapotaka kuacha S |
| Kupoteza hisia | Kuvuja damu na vidonda |
| Kupoteza ufahamu | Maumivu na kukohoa |
| Matatizo ya kupumua hewa safi P | Kushindwa kujidhibiti |
| Mshtuko wa moyo Q | Kupata maruwiruwi |
| Kifo cha gafla | Kupoteza fahamu |
| Kifo kutokana na kunusa R | Kuathirika kwa macho |
| Kuathirika kwa mhimili wa hisi | |
| Kuathirika kwa uboho | |
| Kuathirika kwa ubongo, ini na figo | |
| Kuathirika kwa kinga ya mwili | |
| Kifo cha gafla |
P. Wakati wakuvuta, mvuke unaosababishwa na kemikali hizo unakusanyika katika mishipa ya damu na kuzuia hewa safi kuingia kwenye damu, hicho ndicho chanzo cha mtu kuzimia ama kushindwa kupumua.
Q. Hili hutokea wakati hewa safi haipenyezi kwenye moyo.
R. Wakati mtumiaji anapokufa kutokana na kushindwa kupumua ama matatizo ya moyo inajulikana kama Kifo cha Ghafla cha Kunusa..
S. Dalili hizo ni kama wasiwasi, unyogovu, kufadhaika, tabia ya ukatili, kizunguzungu , kutetemeka, kichefuchefu, kutokua na usingizi usiku.
| ATHARI ZA MUDA MFUPI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| VIWANGO VYA CHINITT T | Uraibu |
| Furaha ya ajabu ajabu/starehe. | Dalili zinazojitokeza unapotaka kuuwacha uraibu huo U |
| Kupoteza fahamu. | Kupoteza uzito |
| Kuhisi kujitenga | Matatizo kuongea na kuwaza |
| Wasiwasi au kuchanganyikiwa | Kupoteza fahamu |
| Kusahau mambo | Unyogovu |
| Kuropoka | |
| Kutoona vizuri | |
| VIWANGO VYA KADRI | |
| kufadhaika | |
| Kutokwa na mate kupita kiwango | |
| Kupoteza fahamu ya kutafakari | |
| Kutoafikiana mambo kutokana na uoga | |
| Kubadilisha msimamo mara kwa mara | |
| VIWANGO VYA JUU | |
| Mshtuko wa moyo | |
| Kiharusi | |
| Maatatizo ya kupumua | |
| Kupoteza ufahamu | |
| Kifo cha gafla |
T. Mtumiaji hana udhibiti wa matumizi yake. Wengine wanaweza kufurahia wakati wengine wanaweza kuwa katika uchungu.
U. Dalili zinazojitokeza ukitaka kuacha ni pamoja na kuharisha, baridi na kutetemeka.


Utafiti unabaini wingi wa madhara ya wanaovuta sigara. Tangia miaka ya 1999, kampuni nyingi tu zinazo tengeza tumbaku wamekubali madhara yanayotokana na uvutaji wa sigara.
Moshi unaotokana na sigara moja una kemikali 7,000. Hizi ni pamoja na:
Kuambatana na Shirika la Afya Ulimwenguni [WHO] Uvutaji wa sigara ni sababu kubwa ya vifo vingi na ulemavu kuliko maradhi mengine yoyote.
| TAIFA | UMRI ULIOKUBALIKA KISHERIA KUNUNUA NA KUNYWA POMBE |
| Argentina | 16 / 18 (KUTEGEMEA SHERIA ZA MKOA) |
| Australia | 18 |
| Cameroon | 18 |
| Canada | 18 (IN MOST STATES) 19 (INAKUBALIKA MAENEO YA MANITOBA, ALBERTANA QUEBEC) (MAENEO MENGINE YOTE) |
| China | 18 |
| Colombia | 15 |
| Costa Rica | 18 |
| Dominican Republic | 18 |
| Misri | 18 |
| India | 18 |
| TAIFA | UMRI ULIOKUBALIKA KISHERIA KUNUNUA NA KUNYWA POMBE |
| Ujapani | 20 |
| Malaysia | 18* |
| Mexico | 18 |
| Uholanzi | 16 |
| Papua New Guinea | 18 |
| Peru | 18 |
| Singapore | 18 |
| Afrika Kusini | 18 |
| Syria | 18 |
| Taiwan | 18 |
| Thailand | 18 |
| Marekani | 21 |
Kamari, pia inayojulikana kama michezo ya bahati nasibu, inaweza kuchukua aina nyingi. Mifano ya kamari ni pamoja na mbio za farasi, dau la soka, tikiti za bahati nasibu, michezo ya kubahatisha (Roulette, Blackjack, Baccarat) na hata dau ndogo ndogo na marafiki.
Katika tamaduni nyingi, kucheza kamari ni tabia inayokubalika. Kwa mfano, huko Singapore, wengi hununua tikiti za bahati nasibu ya serikali mara kwa mara, na wengine wako tayari kupanga foleni kwa masaa kwenye “vituo vya bahati nasibu” kwa droo kuu. Nchini Australia, katika baadhi ya majimbo, ni kawaida katika baa na vilabu kupanga mashini za kamari. Lebanon ina kasino, ambazo mara kwa mara huwa na matukio ya poka. Kimataifa, mchezo wa kitaalamu wa poka unachukuliwa kuwa mchezo halali.
Hata hivyo nchi nyingi pia zina sheria dhidi ya aina fulani za kamari. Baadhi, kama Saudi Arabia, wana sheria zinazopiga marufuku kabisa kucheza kamari. Nyingine, kama Singapore (kabla ya michezo ya kasino kuhalalishwa mnamo 2005) ilifanya kamari ya kibiashara kuwa haramu, lakini ikaweka masharti ya kamari ya kijamii (mchezo wa poka miongoni mwa marafiki siku ya Ijumaa usiku) na huluki za kamari zinazodhibitiwa na serikali. Hata nchi huria zaidi kama vile Uingereza inaruhusu kamari ya kibiashara mradi tu sheria fulani (kama vile malipo ya ya viwango vya chini, usajili au ushuru maalum wa faida inayotokana na shughuli za michezo ya kubahatisha) kufikiwa. Bila kujali jinsi huria sheria za michezo ya kubahatisha zinavyoweza kuwa, serikali zinatambua hili: kamari huleta matatizo ya kijamii - waziwazi au kwa njia isiyo wazi.
Kamari ina uwezo wa kumfanya mtu kuwa mraibu na ni hatari. Madau madogo kwenye michezo au matokeo mengine inaweza kuonekana kuwa isiyo na madhara yoyote.
Yamkini, kuna mstari mwembamba unaotenganisha uchukuaji hatari uliokokotolewa na kuwa mraibu kwelikweli.
Wengi wa watu wanaocheza kamari ni wacheza kamari walio katika hatari ndogo. Wanafanya hivyo kwa ajili ya kujifurahisha tu au kama shughuli ya kujumuika na marafiki. Kwa kawaida hutumia muda unaodhibitiwa na huwa wameamua mapema kiwango cha hasara. Walakini, uraibu hukua wakati watu hutumia kamari kama njia ya kuyakimbia matatizo au kupata msisimko wa kujihatarisha. Kwao, kushinda imekuwa aina ya kujithibitisha, kuyakimbia matatizo au kusisimka.
Kamari huendelea kutoka kuwa mchezo au shughuli ya kujumuika na jamii na kuwa ni njia yao ya kujithamini au inakuwa ni tumaini la uwongo kama suluhisho la haraka ya shida zao. Lakini familia nyingi za wale waliozoea kucheza kamari watakuambia kwamba wachezaji hao wanashindwa mara nyingi zaidi ya wanavyoshinda, na pesa haziwezi kununua furaha au kufuta maumivu.
Kulingana na Mwongozo wa Uchunguzi na Takwimu za Matatizo ya Akili, Marekebisho ya Maandishi ya Toleo la 4 (DSM IV TR), uraibu wa kamari unaainishwa kama ugonjwa wa kisaikolojia. Kwa utambuzi wa uraibu wa kamari, mteja lazima aonyeshe tabia mbaya ya kamari inayoendelea na inayojirudia ambayo inatimiza angalau vigezo vitano kati ya vifuatavyo:
Uraibu wa kamari unajidhihirisha kwa njia nyingi, pamoja na malalamiko juu ya shida za pesa, unyogovu na mawazo ya kujiua. Waraibu wa kamari wanaweza pia kujikuta hawana kazi na wenye afya mbaya, kwani hawawezi kupata usingizi mzuri na huhisi wasiwasi wakati mwingi.
Pia uraibu wa kamari huingilia uhusiano kati ya watu, na kusababisha kuvunjika kwa familia au mahusiano mabaya ya familia.
Uchunguzi wa kawaida kutoka kwa wanafamilia wa waraibu wa kamari ni pamoja na:
Tabia hizi zote hudhuru uhusiano wa kifamilia, kwani wanafamilia wote hawawezi kutegemea mcheza kamari kuchangia mahitaji ya familia, au hata kutekeleza mahitaji yake mwenyewe. Kunakuwepo na suala la kuaminiana kwani hawawezi kuwa na uhakika kwamba mcheza kamari anaweza kuchangia fedha zozote kwa ajili ya maslahi ya familia.
Ikiwa mcheza kamari amekata tamaa, anaweza kugeukia njia zisizo halali za kupata pesa, kama vile kukopa kutoka wakopeshaji pesa wasio na leseni au kwa kujihusisha na uhalifu. Vyovyote vile, hii ina athari kwa usalama wa umma. Wakopeshaji hao hunyanyasa wadeni, familia zao na majirani zao wasio na hatia, na shughuli za uhalifu huhatarisha watu na mali.


Kuhimiza washiriki kuweka mipaka katika tabia hatarishi.
1. Waeleze washiriki kwamba sasa wana ukweli wanaohitaji kufanya uamuzi sahihi na wako katika nafasi nzuri sana ya kuamua wapi wanataka kuweka mipaka yao kuhusiana na tabia hatarishi iliyojadiliwa.
2. Katika kitabu cha mazoezi, kila moja ya tabia nne hatarishi inazo kauli sita, kila moja ikielezea hatua zinavyofuatana kadiri tabia hizo zinavyoendelea. Waulize washiriki ni wapi watakapoweka mipaka yao kwa kila moja ya tabia hizi. Wachore mstari mmoja katika hatua hiyo.

Mstari wa mpaka uliopendekezwa umechorwa hapa chini, lakini kufuatana na maadili yako na utamaduni wako unaweza kuusogeza popote huo mstari.
3. Baada ya wote kumaliza zoezi, waombe wachache wao kueleza wameweka wapi mpaka na kwa sababu gani. Na wewe waeleze mipaka yako and sababu zako. (Ili kudumisha mpaka ulio salama na bora, hatupashwi kuvuka mipaka yetu)

Ukosefu wa mipaka iliyo wazi maishani unaweza kusababisha matokeo mabaya.
Katika maisha tunapata majuto tunapofanya jambo ambalo baadaye tunatamani tusingelifanya. Majuto yanaweza kuja haraka, kwa mfano kuuguzaa majeraha na maruirui ambayo huambatana na unywaji pombe. Wakati mwingine majuto yanaweza kuchukua miezi au miaka, mfano mtu wa umri wa makamu ameathirika na sigara baaada ya kutumia miaka mingi tangu alipokua kijana anapotambua ana ugonjwa wa saratani ya mapafu. Je, inawezekana kukawa na maisha yasiyo na majuto?
Huenda tusiondoe majuto yote, lakini ikiwepo mipaka iliyo wazi tunaweza kutarajia kufanya maamuzi bora yanayolingana na kile tunachfikiria ni muhimu na si kwa kufuata hisia zetu, homoni, kushawishika na marafiki na kadhalika.
Pasipo kuwepo na mipaka iliyo wazi, ni rahisi kujiingiza katika tabia za hatari na hata kinyume cha sheria. Kuendesha gari ukiwa mlevi, kutumia mihadarati na kudhulumu wengine ni baadhi ya tabia zinazoghalimu kiasi kikubwa sana kwa wahalifu, familia zao, wahasiriwa wao na jamii.
Baadhi hubisha kwamba wakipata shida ni matatizo yao wenyewe, je hiyo ni kweli?
Dereva mlevi anaweza hatarisha maisha yake na hata ya wengine wanaotumia barabara. Kwa kutokuwa na mipaka muathiriwa na wale walio karibu naye wasio na hatia yoyote wanahasiriwa.
Katika mazingira ambapo hakuna mipaka iliyo wazi na wakati watu wawili wanapendana na mmoja wao au wote wanajiweka katika hali ya hatari, mfano unywaji pombe kupindukia au kutumia mihadarati, ubakaji unaweza kutokea. Hali hiyo ya kubakwa na rafiki inatokea kati ya watu wawili waliozoeana bila ridhaa ya mmoja wao. Hili linaweza kuwa matokeo ya shinikizo kali la kisaikolojia, ingawa kwa kawaida mbakaji anatumia pombe au dawa za kulevya ili kumfanya mwanamke apoteze fahamu. Wanawake wengi ambao wamebakwa kwa njia hii hawakumbuki kilichotokea, ama kutokana na athari za pombe au madawa ya kulevya, au kwa sababu ya kiwewe cha tukio hilo.


Maswali ya kujiuliza kabla ya kusema sio jambo la kutilia uzito?

Je, tabia hatarishi huathiri vipi malengo ya baadaye?
Kuwafahamisha wanaoshiriki kufahamu wanaweza kunaswa katika hali tata wasipoweka mipaka wazi ya kimwili na kihisia kwenye mahusiano yao.
Mahusiano yaliyo bora yanahitaji mipaka ya wazi ya kihisia, kisaikolojia na kimwili. Hilo ni kweli katika uhusiano wowote, lakini haswa uhusiano baina ya mvulana na msichana.
Wakati mvulana na msichana ni marafiki wa karibu sana, mipaka kati yao kama marafiki tu bila kitu kingine cha ziada inahitajika. Kwani mmoja wao anaweza kufikiri kuwa wao ni marafiki wa kawaida tu, huku mwingine anafikiri wao wanachumbiana. Wakajikuta wameingia kwenye eneo lenye matata linalosababisha kuumia, kukata tamaa na kuchanganyikiwa.
Mipaka iliyo wazi zaidi ni mipaka ya kimwili. Wanafafanua ni tabia gani inayofaa, iwe katika urafiki au uhusiano wa uchumba. Wakati mpaka umevukwa bila idhini, humwacha mtu anahisi kukiukwa. Kuweka mipaka ya kimwili ni pamoja na kutumia haki yako ya kusema hapana wakati mtu anajaribu kudharau au kudhalilisha mwili wako.
Watu wengi hawapotezi ubikira wao, siku moja tu. Ni mchakato wa taratibu wa kuvuuka mipaka iliyowekwa, kwenda kinyume na hulka yao na na kuhalalisha matendo yao. Ghafla wanajikuta katikati ya uchu na shauku ya ngono na wanafanya kile wanachohisi kuwa ni sawa kwa wakati huo.
Mipaka ambayo inafaa kuzingatiwa ni ya hisia, na inafaa kulindwa. Mipaka hiyo hukiukwa iwapo mhusika mmoja atakuwa na hitaji zaidi au kumdhibiti mwingine. Katika uhusiano wa mvulana na msichana, wanaochumbiana, wanaoyaweka wazi wakiongea hasa siri za moyoni siku ya kwanza wanapokutana, inawaweka katika hali tata ya uhusiano wa kihisia.
Aina ya hila zaidi ya mipaka ni mipaka ya kihisia, na hii inachukua fomu ya kudanganywa kwa hisia. Mstari huvukwa wakati upande mmoja unapoanza kuwa "uhitaji" au udhibiti wa mwingine. Katika uhusiano wa uchumba, wanandoa ambao walifunua sana na haraka sana, kama vile kushiriki siri zao zote za kina katika tarehe ya kwanza, wanajiweka tayari kwa hali ya juu ya uhusiano wa kihisia.


Kuweka wazi matarajio yanayotokana na mipaka tofauti iliyopo katika kila aina ya uhusiano baina ya msichana na mvulana.
1. Waombe washiriki watie alama ya ndio katika kisanduku ikiwa wanafikiria kuwa ni matarajio ya kuridhisha ya mtu mwingine katika muktadha wa mahusiano yafuatayo baina ya mvulana –na msichana:


Matarajio
Namtarajia:
2. Waombe wachache wao washiriki majibu yao na chunguza zaidi kama unahisi wako katika eneo tata.
3. Waeleze washiriki kutumia muda mwingi mkikaa pamoja kunaleta matarajio [hasa kwa wasichana]. Tunahitaji kufahamu mipaka ya hisia inayofaa katika kila hatua ya uhusiano. Iwapo mmoja kati yao anaweza jenga matumaini zaidi ya mwingine jambo hilo linaweza ingiza wasiwasi katika uhusiano.
4 Washirikishe maoni yako kuhusu matarajio yenye afya katika mahusiano mbalimbali ukitoa mifano yako ya kibinafsi.
| RAFIKI WA KAWAIDA | RAFIKI WA KARIBU | WANAOCHUMBIANA | WAPENZI/ WALIPEANA POSA | NDOA |
| A | ✔ | ✔ | ✔ | ✔ | ✔ |
| B | — | — | ✔ | ✔ | ✔ |
| C | — | — | — | ✔ | ✔ |
| D | — | — | — | ✔ | ✔ |
| E | — | ✔ | ✔ | ✔ | ✔ |
| F | — | — | — | — | ✔ |
| I | — | — | — | ✔ | ✔ |
| H | — | — | — | ✔ | ✔ |
| N | — | ✔ | ✔ | ✔ | ✔ |
| J | — | — | — | — | ✔ |

Kuwepo katika eneo lisiloeleweka kwa muda mrefu kunaweza kuleta kuchanganyikiwa, na hali hiyo hudhohofisha uhusiano uliokuwa mwema.
Mfano halisi ni wakati kijana anavyoweza kukiuka mipaka ya kihisia katika urafiki wao:
Kijana mmoja alipata fursa kuelezea aliyoyafahamu kutokana na “urafiki wao”:
Haupaswi kumpa mtu udhibiti mkubwa juu ya hisia zako, miliki hisia zako na kuweka mipaka.

1. Chunga matarajio yako
Fahamu lile utakalo, na usilolitaka, miongoni mwa marafiki. Iwapo ulikuwa na siku mbaya na ungelipendelea rafiki kukusikiliza, lakini si mtu ambaye umemfahamu siku mbili au miezi miwili tu. Iwapo una rafiki mwema, asiye wa jinsia yako ni bora kuweka mipaka ya kihisia, pasipo na mipaka mwenzako anaweza kuwaza uhusiano wenu unaendelea kukomaa na wewe unafikiria nyinyi ni “marafiki tu”.
2. Jihadhari na uhusiano wa kihisia
Ni vema kufahamu kwamba unaweza kumweleza matatizo unayokumbana nayo rafiki yako, na unatambua kwamba atakusikiza. Japo ni bora kuchunga na kuweka mipaka katika hisia zako ili usimtegemee mwingine kila wakati jambo linapokusibu. Unahitaji mtu huyo “kukuokoa” kila wakati. Uhusiano wenye utegemezi wa hali hiyo huziacha pande zote mbili kuhisi mmenaswa.
3. Tambua usaliti wa kihisia
Ni vizuri kuwa makini kutokana na matamshi kama vile, “iwapo hutakula nami maakuli ya mchana sitafurahia, sitakula tena .” Kuna tofauti kubwa kati ya kuwa mkweli na mwaminifu kwa marafiki zako kuhusu hisia zako, na kudhibiti hisia zao ili kupata unacho kitaka.


Kuonyesha hitaji la mipaka katika urafiki wa kimwili na athari zisizoweza kutenduliwa vinginevyo.
Vinginevyo, unaweza kutumia:

1. Wapatie nusu ya darasa biskuti za sandwich ya Oreo yenye vanilla krimu na biskuti za Oreo zilizo na krimu ya chokoleti kwa nusu nyingine ya darasa.
2. Waombe washiriki waliopata biskuti za sandwich ya vanilla krimu kuoanisha na mtu aliyepata biskuti za sandwich ya krimu ya chokoleti.
3. Waombe washiriki wote waigize hadithi hii unapoisimulia. Unaweza kupata majina ya uwongo ya kuwakilisha biskuti hizo mbili (k.m., Jack na Jill). Hadithi inaweza kusikika kama hi:
4. Waulize washiriki wanachokiona wanapotenganisha biskuti ya sandwich. Baadhi ya vanila au cream ya chokoleti imehamishiwa kwenye kipande kingine cha biskuti.
5. Waeleze kwamba maendeleo ya ukaribu wa kimwili yanaweza yasiwe ya haraka/na makali kama jinsi yalivyotokea katika hadithi hii, lakini jambo moja linaweza kusababisha lingine kwa urahisi.
6. Eleza kwamba ngono hujenga uhusiano unaobadilisha wahusika. Kama tu kipande cha biskuti kilicho na vanila na cream ya chokoleti, pande zote mbili huacha sehemu yao kwa mwingine. Hata wanapojaribu kwenda njia mbalimbali, alama walizoweka hubaki.
7. Sisitiza kwamba tendo kali la kimwili na la kihisia kama ngono ni salama ndani ya mipaka ya ndoa tu. Ngono hujenga uhusiano unaothibitisha ahadi ambayo wanandoa waliyoitoa siku ya harusi yao.


Kuelezea jinsi suala la ngono linavyo jenga uhusiano.
1. Ikiwa unaanza na karatasi mbalimbali za samawi na waridi, zigundishe karatasi hizi pamoja.
2. Onyesha washiriki karatasi iliyobandikwa awali na ueleze kuwa watu wawili wanapofanya ngono, mwili hutoa homoni inayoitwa oxytocin, inayowakilishwa hapa na gundi. Homoni hii hujenga uhusiano mkubwa kati yao (kwa maelezo zaidi kuhusu oxytocin ni nini, tafadhali angalia Maudhui ya Ziada - Oxytocin mwishoni mwa zoezi hili).
3. Wakati gundi imekauka, jaribu kuzitenganisha karatasi. Haijalishi jinsi unavyojaribu kutenganisha karatasi kwa uangalifu, mgawanyiko safi hauwezi kufanyika - karatasi zimeshikamana pamoja.
4. Waeleze kwamba shughuli za ngono zinahusisha na kujumuisha sehemu zote za mwanadamu na kuimarishwa na homoni ya oxytocin inayotolewa na mwili wakati wa ngono. Ukishiriki ngono kabla ya ndoa na mkaachana, matokeo yake ni ni makovu ya kuvunja uhusiano sio kimwili tu bali kihisia, kiroho, na kihomoni pia.
5. Sisitiza kwamba tendo kali kama hilo la ngono ni salama tu ndani ya mipaka ya ndoa. Uhusiano unaotokezwa na urafiki wa kimwili ni gundi inayoimarisha ahadi ambayo wanandoa waliitoa siku ya arusi yao.

Ile hatua ya kukuza uhusiano kati, ya wawili wanaopendana kufuatia tendo la kujamiana sio tu ni kutokana na hisia ama maamuzi , mwili wa mwanadamu pia una utaratibu unaosaidia kuunda vifungo vya kihisia vya bio-kemikali kati ya watu. Oxytocin ni homoni ambayo hutolewa wakati mama mja mzito anapojifungua mtoto wake. Homoni inajitokeza na inawezesha mama huyo kuhusiana kwa karibu na mwanawe, ni uhusiano unaomfanya awe mlinzi. Kemikali hiyo hiyo vilevile hutolewa kwa mfano mwanamke anapokumbatiwa kwa sekundi 20 au zaidi.
Wanaume vilevile wanatoa oxytocin pamoja na vasopressin, kemikali yenye nguvu inayosababisha wanaume kushikamana kwa undani sana na wenzi wao kwa maisha yao yote na kuwafanya kuwa kinga yao.
Wakati watu wawili wanaposhiriki ngono, miili yao hutoa homoni hizi ambazo huwawezesha kujenga uhusiano wa kihisia kati yao. Wanaposhiriki ngono na si mara moja, homoni za oxytocin na vasopressin zinatolewa zaidi. Je unaweza kuwazia ni jinsi gani mshikamano hou ulivyo na nguvu ?
Kemikalia ya oxytocin na vasopressin hutolewa pasipo kujali iwapo wawili wameoana ama ni tendo la ndoa la usiku mmoja, hakuna kitu kama “ngono isiyo na masharti” - daima kutakuwa na uhusiano wa kihisia unaoundwa. Kemikali hizi hazina maadili—hazitofautishi kati ya mazuri na mabaya, mema na maovu.
Oxytocin na vasopressin zinapotolewa, huwasha sehemu za ubongo ambazo zinahusiana na tabia ya kijamii kama vile hisia za uhusiano wa kina, na ikiwezekana kuwa “katika mapenzi.” Homoni hizi huimarisha uhusiano kati ya washirika wa ngono. Kwa kweli, shughuli za ngono, zinazoimarishwa na mfumo wa malipo ya kemikali katika ubongo, zinaweza kuleta uraibu. Hivyo ngono ndani ya ndoa ni afya na manufaa, lakini ngono nje ya ndoa ni hatari. Ingawa oxytocin hutolewa kwa wanaume na wanawake, athari zake zinaonekana kuwa na nguvu zaidi kwa wanawake.


Kuwasaidia washiriki kuelewa nini hutangulia tendo la ngono.
1. Waombe washiriki wote wasimame. Kwa kila kauli, washiriki watakaojibu ndiyo watapaswa kukaa chini wale watakaojibu hapana watabakia wamesimama.
2. Kauli: “Je, unaweza kusema “ulishiriki ngono” na mtu ikiwa shughuli ya karibu zaidi uliyoshiriki ilikuwa ________?”
3. Iwapo wengi wa washiriki wanafikiri kuwa inachukuliwa kuwa ni “ngono” tu wakati wa kujamiiana na si kila kitu kingine kabla ya hapo (kubembeleza bila kuvaa nguo zao au kubembeleza sana), kuna uwezekano kwamba watachora mstari/mpaka kwenye hatua za mwisho za ukaribu wa kimwili.
4. Vijana wengi huamini kwamba wanaweza kufanya “chochote isipokuwa . . .” na bado wawe “bikira” Kwa nini hiyo sio busara? Je, ni uwezekano gani ambao vijana wengi wataacha kabla tu ya kujamiiana?


Kuwasaidia washiriki kuzijua hatua mbalimbali za ukaribu zinazosababisha kuimarika kwa uhusiano.
1. Waliojitolea wasimame katika vikundi viwili, kimoja cha wavulana na kingine cha wasichana wakiacha nafasi kati yao inayotosha kuunda mstari kati ya hivi vikundi viwili.
2. Sambaza seti moja ya kadi kwa wasichana na seti moja kwa wavulana. Kila mtu aliyejitolea anapaswa kuvaa lebo moja, ambayo iko wazi inaweza kusomwa na wengine wote.
3. Ndani ya vikundi vyao, waombe waliojitolea wajipange kulingana na wanavyofikiria mlolongo wa uhusiano unavyoendelea.
4. Watakapomaliza, linganisha mipangilio ya kati ya kikundi cha wavulana na cha wasichana.
5. Mwombe mvulana wa ziada aliyejitolea asimame kwenye mstari pale ambapo anafikiria urafiki unatafsiriwa kuwa uhusiano. Vivyo hivyo msichana wa ziada wa kujitolea naye afanye.
6. Wavulana wanaweza kuchora mstari baada ya kugusana kwa kiasi kikubwa kimwili kama vile “mkono hadi kiuno,” ambapo kwa wasichana, “mkono kwa mkono” kwa kawaida ikiwakilisha kushikana mikono katika uhusiano.
7. Jadili yanayofanana na yanayotofautiana katika mitizamo na matarajio ya ukaribu wa kimwili kati ya jinsia hizi mbili.
Dkt. Desmond Morris, mwandishi wa kitabu kuhusu tabia [Intimate Behavior], anaeleza kwamba wanaochumbiana wanahitaji kupitia hatua mbalimbali za urafiki wao ikiwa wanapenda uhusiano wao uwe wa kudumu, yaani kuelekea kuoana, waanze na hali ya kawaida.

Kwa nini tunahitaji kwenda kwa utaratibu na polepole kupitia hatua za kuimarisha uhusiano?


Kuwasaidia washiriki kufanya uamuzi sahihi na kujua wapi pa kuweka mipaka ya ukaribu wa kimwili katika uhusiano.
1. Elezea umuhimu wa kujua jinsi mwanadamu alivyoumbwa katika maswala ya unyumba.
| MSWADA | KITENDO |
| Joe anaelezea jinsi sisi sote ndani yetu tunao mshumaa uliyowashwa wa kuwapenda wale wa hisia tofauti. Wakati uhusiano unapoanza,unaridhika mkiwa pamoja lakini baada ya muda unakuwa na hitaji la kushikana mikono. | Washa mshumaa. Washa kiberiti kwa kutumia mshumaa. |
| Baada ya muda, unataka kuendeleza uhusiano huo na
hisia ya mapenzi inaanza kuchipuka.
Usipokuwa makini utaanza kutomasana na swala moja
litazua jingine mpaka mnajikuta mmeshiriki ngono. Kama
tendo hilo ni nje ya ndoa, mara nyingi uhusiano unaishia
hapo na kuvunjika Kilichokuwa kizuri na kilicho leta furaha tele kimegeuka kuwa kichungu kama ndimu.Vijana wengi ambao walijiusisha katika vitendo vya ngono kabla ndoa wanajihisi hatia, aibu, na kujuta kwa kuwa tendo hilo halitafutika mioyoni mwao. Maji yaliyomwagika hayawezi kuzoleka. Shikilia baruti iliyochomeka waeleze wanaoshiriki wanaona nini (kilichoungua, kimechomeka, na cheusi). | Washa kiberiti cha pili kutumia kiberiti cha kwanza, washa kiberiti cha tatu kutumia cha pili. Washa baruti ukitumia kiberiti cha tatu. Baruti itaisha wakati ambapo unapofika eneo la uhusiano kuvunjika. |
2. Onyesha slaidi ya “umbali upi ni mbali zaidi?”:
Ni wapi mipaka itaafiki msimamo wako?
3. Chagua swali moja au mawili kati ya yafuatayo ya kuuliza:
4. Wakumbushe washiriki uhusiano unapovunjika, aliyejihusisha na tendo la ngono ndiye atakayeathirika mawazo. Walioshiriki ngono hawawezi kuachana kihisia bila mabaki (kama katika shughuli za “Hali ya Kunata” na “Mchanganyiko wa Vidakuzi”). Wameitoa sehemu yao wenyewe na kumpatia aliyeachwa. Pitia vipengele vitano vya ukuaji vilivyotajwa katika Sura ya 1 “mwili wa mwanadamu ” : Akili, mazingira, hisia, mwili na maadili mema, – katika kutoa ukumbusho swala la ngono, si tendo la mwili peke yake.
Waombe washiriki, kuchora mstari wima kwenye sehemu ya grafu katika kitabu cha mazoezi mahali ambapo wataweka mipaka ya binafsi kuhusu kukaribiana kimwili.
Unavuka mipaka pale?

Kuwasaidia washiriki kufahamu matokeo yanayohusu hisia, jamii, na mwili wanaposhiriki ngono kabla ya ndoa.
Dkt. Henry Cloud na Dkt John Townsend katika kitabu chao kinachoitwa Mipaka (Boundaries) wameandika kwamba “Uamuzi wowote una matokeo yake; mema ama mabaya, hiyo ni sheria ya maisha . Ikiwa unavuta sigara, kuna uwezekano mkubwa kwamba utaendeleza utapeli wa mvutaji sigara, na unaweza hata kupata saratani ya mapafu. Ukitumia fedha kupita kiasi, kuna uwezekano mkubwa utapata simu kutoka kwa wadai, na unaweza hata ukawa na njaa kwa sababu huna pesa za kununua chakula. Kwa upande mwingine, ikiwa unakula vizuri na kufanya mazoezi mara kwa mara, utapata matatizo machache ya afya. Ukiweka bajeti kwa busara, utakuwa na pesa tele za kulipa mahitaji yako ya chakula.”
Kila tendo lina matokeo yake; mema ama mabaya. Suala la ngono nje ya ndoa lina matokeo mengi yaliyo tofauti na magumu. Wanaoathirika sio tu wale wanaohusika katika tendo la ngono, lakini wale walio karibu nao pia, yaani, familia, marafiki na hata jamii.


Kuwaonyesha washiriki mtandao wa matokeo ya kujamiiana kabla ya ndoa unavyoonekana katika maisha halisi.

Mifano:
1. Mpatie lebo ya jina kila aliyejitolea, kadri iwezavyo wapatie wasichana majina ya kike na vile vile wavulana majina ya kiume.
2. Tandaza shuka sakafuni mbele ya chumba. Hakikisha kuna nafasi ya kutosha kwa waliojitolea kusimama hapo.
3. Waambie kwamba watakaposikia “jina” lao linaitwa, waje mbele na kusimama kwenye shuka.
4. Anza kuwasomea kwa sauti :
5. Katika hatua hii, waambie washiriki walio na HI kwenye kona ya chini, upande wa kulia wa lebo ya majina yao kuinua mikono yao. Waambie kwamba HI inawakilisha VVU na wale walioinua mikono yao wanawakilisha wale ambao sasa wameambukizwa VVU. Unaweza kuendelea kusoma baadhi ya ukweli kuhusu VVU. Kama bado kuna muda wa kutosha, unaweza kueleza maana ya herufi zao nyingine (CH, HP, TR) na kusoma ukweli kuhusu magonjwa hayo ya zinaa.
Unaweza kuangazia uchunguzi ufuatao:

6. Onyesha slaidi inayoonyesha utando mgumu wa mahusiano na jinsi magonjwa mbalimbali ya zinaa yalivyoambukizwa.
Ni tendo moja tu mwanadamu hutenda kabla hajajipata katika hatua tata ya kupata maradhi yanayo sababishwa na ngono asipo kuwa mwangalifu. Mwanadamu anastahili kuwa na mchumba mmoja na kuzingatia uwaminifu. Wakati wa harusi yako, ni wewe tu na mke/ mme wako je unataka ujihusishe na watu 17? Kabla ya kuoa/kuolewa.
Unaweza kujumuisha taswira ya slaidi ya makala ya jarida la Time, “Picha ya Ngono za Vijana,” ya Februari 14, 2003, ili kuonyesha kuwa haya hutokea katika maisha halisi. Katika utafiti huu mahususi wa shule moja ya sekondari ya Marekani, wanafunzi wengi walikuwa na mpenzi mmoja au wawili tu lakini hata hivyo waliounganishwa na mtandao wa wanafunzi 288, na kuwaweka katika hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa kwa sababu walioshiriki nao ngono walikuwa nao wameshiriki ngono na wengine.

| DALILI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| WANAWAKE | Matatizo ya ukuaji |
| Uchungu wakati wa kujamiiana | Matatizo ya uzazi |
| Uchungu wakati wa kukojoa | |
| Kutapika | |
| Kitengo nyeti kuwa yenye rangi ya manjano ama kijani kibichi | |
| WANAUME | |
| Usaha kwenye uume | |
| Maumivu/kusikia kuungua wakati wa kukojoa | |
| WOTE | |
| Kuwashwa kwa mkundu | |
| Usaha toka mkunduni | |
| Maumivu kwenda choo | |
| Kuwashwa na maumivu ya koo | |
| Shida kumeza |
| DAWA AU TIBA? KISONONO KINAWEZA KUTIBIWA KUPITIA KUMEZA DAWA ZA KUUA BAKTERIA. |
| DALILI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| DALILI ZA MWANZO | Maumivu yanayotokea mara kwa mara kutokana na mkururo wa mawazo ugonjwa,uchovu , kukaa juani au hedhi |
| makundi ya vidonda venye uchungu | |
| Maumivu wakati wa kukojoa | |
| Dalili kama za mafua |
| MEDICATION OR CURE? There is no cure for herpes. However, medication can help to speed up healing and lessen the pain of the sores, as well as control recurrences. |
| DALILI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| Dutu za uzazini | Saratani ya kizazi |
| Mara nyingi hakuna dalili zinaonekana | Saratani ya uume |
| Maumivu wakati wa kukojoa | Saratani ya mkunduni |
| Dalili kama za mafua | Saratani ya mdomo |
| DAWA AU TIBA? Haina tiba. Hata hivyo, zipo chanjo na matibabu.V |
V. Wakati HPV ikitokea, madakatari wanashauri kwenda kupimwa mara kwa mara hospitalini kwa ajili ya swala la saratani; kwa wanawake wengi ,virusi hivyo hutoweka pasipo kuathiri afya iwapo vitashughulikiwa . Chanjo ya HPV inalenga aina mbili zinazosababisha asilimia 70% za saratani ya uzazi; hata wale ambao waliopata chanjo wanaweza kupata maradhi hayo
| DALILI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| Uchovu | Ugonjwa wa ini |
| Maumivu upande wa chini tumboni | Saratani ya ini |
| Kupoteza hamu ya kula | |
| Kichefuchefu/kutapika | |
| Maumivu ya viungo | |
| Kuumwa na kichwa | |
| Homa | |
| Vipele | |
| Hakuna dalili W |
| DAWA AU TIBA? Tiba zake ni nadra sana. Hata hivyo, inaweza ikaondoka yenyewex.X |
W. Asilimia 50% ya walioathirika hawaonyeshi dalili yoyote. Dalili huonekana kati ya wiki sita na miezi sita baada ya mtu kuambukizwa.
X. Watu wengi walioathirika virusi vinatoweka kati ya wiki nne mpaka nane. Watu wachache wanabaki na virusi kuwaambukiza wengine maisha yao yote.
| DALILI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| Mwanzoni hakuna dalili Y | Kuwa tasa Z |
| Kutoka damu kusiko kawaida | Mimba za ectopic |
| Kutokwa uchafu ukeni | Maumivu ya muda mrefu |
| Maumivu ya tumbo na mgongo | |
| Homa/kusikia baridi | |
| Kichefuchefu/kutapika | |
| Maumivu ya uke wakati wa ngono |
| DAWA AU TIBA? Madaktari wanaweza kuagiza antibiotics na kushauri kupumzika kitandani na kujiepusha na ngono. Kesi mbaya zaidi zinaweza kuhitaji upasuaji ili kurekebisha au kuondoa kizazi. |
Y. Mwanzoni, PID haionyeshi dalili zozote. Hata hivyo, wakati maambukizi yanavyoendelea, dalili zinaweza kuanza kuonekana.
Z. Kadiri idadi ya maambukizo ya PID ambayo mwanamke amekuwa nayo, ndivyo hatari ya kuwa mgumba inavyoongezeka.
| DALILI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| Usumbufu wakati wa kukojoa | VVUTrichomoniasis isipotibiwa huongeza hatari ya kuambukizwa na |
| Kuwashwa kidogo hadi kuvimba sana | |
| Kuwashwa au maumivu ndani ya uume | |
| Kutokwa na uchafu kwenye uume | |
| Kuwashwa, kuwaka, uwekundu au maumivu ya uke |
| DAWA AU TIBA? Trichomoniasis inaweza kutibiwa na dawa zilizoagizwa na daktari. |
| DALILI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| HATUA YA MWANZO (SIKU 21 - 90 BAADA YA MAAMBUKIZI): | HATUA YA MWISHO: |
| Maumivu mahala ambapo virusi vilipata kupenyeza | Mshtuko wa moyo |
| Kupoteza hamu ya kula | Maumivu makali |
| Kufura kwa tezi | Dementia |
| DALILI ZA KATI (WIKI 3 - 6 BAADA YA VIDONDA): | Kifo cha gafla |
| 2-to-6-week-long body rashes, often on the palms or soles of the feet | |
| Dalili kama za mafua | |
| Kufura kwa tezi |
| DAWA AU TIBA? Inapotambulika mapema inaweza kutibika kwa antibiotics. Ikiwa imekaa sana inaweza pia kutibika na antibiotics lakini matibabu yake ni mazito zaidi na inaweza kusababisha madhara ya daima. |
| DALILI | ATHARI ZA MUDA MREFU |
| Dalili kama za mafua | Unyonge/kutokuwa na kinga ya mwili |
| Kufura kwa tezi | Kupata UKIMWI |
| Homa | Kifo cha gafla |
| Kuumwa na kichwa | |
| Uchovu | |
| Maumivu ya misuli | |
| Kunaweza kusiwepo na dalili zozote mpaka UKIMWI unapoanza |
| DAWA AU TIBA? Hakuna tiba ya VVU au UKIMWI. Dawa zinaweza kuboresha Maisha au kuyarefusha tu.. |


Kusaidia washiriki kuelewa kwamba kushiriki ngono kabla ya ndoa kunaleta hatari ya kupata magonjwa ya washirika wote wa zamani wa wale unaofanya nao ngono.
1. Tayarisha kikombe kimoja kwa kila mshiriki:
2. Nasibu mpe kila mshiriki kikombe na umwombe azunguke chumbani kumwaga na kuchanganya “maji” yaliyo kwenye kikombe chake na kile cha washiriki wengine. Usiwaambie washiriki kwamba baadhi ya vikombe vina siki.
3. Waache waendelee kwa dakika 2-3 kabla ya kuwaomba washiriki warudi kwenye viti vyao na vikombe vyao.
4. Washirikishaji wazunguke chumbani na kuweka soda ya kuoka kwenye kila kikombe.
5. Mapovu yatatokea kwenye vikombe vyenye siki. (Hii itakuwa ni karibu ya wote waliomimina na kuchanganya.)
6. Waombe washiriki ambao wameshika vikombe vilivyowekwa alama ya nukta nyeusi kusimama. Lielezee darasa kwamba washiriki waliosimama wanawakilisha wale ambao tayari walikuwa na magonjwa ya zinaa na walikuwa wanawaambukiza wengine walipokuwa wakizunguka kuchanganya vikombe vyao vya “maji.” (Wale walio na mapovu kwenye vikombe vyao wanapaswa kuwa wengi kuliko wale ambao vikombe vyao vina nukta nyeusi.)
7. Onyesha kwamba washiriki wanaweza “kufanya ngono” (kuchanganya “maji” yao) na mtu mmoja tu, lakini mtu huyo anaweza “kufanya ngono” na watu wengine wawili ambao wamekuwa na wapenzi wengi.

Kumbuka: Unalala na kila mtu ambaye mpenzi wako amelala naye. Ngono kabla ya ndoa inajumuisha hatari ya kupata magonjwa ya washirika wote wa zamani wa yule unayeshiriki naye ngono.


Kuwasaidia washiriki watafakari madhara ya kujihusisha na ngono kabla ya ndoa.

1. Kwenye ubao, andika maneno haya: “Madhara ya Ngono Kabla ya Ndoa.”

2. Waombe washiriki wapendekeze madhara yanayoweza kutokea iwapo watashiriki ngono kabla ya ndoa. Wanapotaja majibu yao, yaandike ubaoni kama hivi inavyoonyeshwa hapa chini..

3. Iwapo kuna jambo linakosekana katika huu mchoro wafahamishe washiriki na uliongeze ubaoni.
4. Baada ya kuorodhesha madhara ya ngono kabla ya ndoa wafahamishe washiriki kuwa mtayaangalia haya madhara moja moja ili waelewe kwa nini na wapi pa kuweka mipaka inapokuja kwenye swala la ngono.

Tanbihi:
Mafanikio ya zoezi hii yanategemea uwezo wa mwezeshaji kuwashirikisha washiriki bila kuwadharau au kunaswa katika kuwapatia taarifa nyingi kupita kiasi.

Chagua mbadala hapa chini ikiwa kikundi hakikuweza kupendekeza madhara ya ngono kabla ya ndoa.

1. Onyesha slaidi ya “Mtandao wa Matokeo: Madhara ya Ngono Kabla ya Ndoa”.
2. Watu 3 waliojitolea kushikilia kadi za “Madhara ya Kihisia,” “Mimba” na “magonjwa ya zinaa”, wasimame sehemu tofauti za chumba pakiwapo na nafasi kati yao.
3. Sambaza kadi 19 zilizobaki kwa watu watakaojitolea.
4. Wakisikia neno “Nenda,” watu 19 waliojitolea wakimbie na kusimama pamoja na mmoja wa wale watu 3 wenye kadi za matokeo.
5. Hakiki makundi, kuanzia na Madhara ya Kihisia, kisha Ujauzito, na mwisho magonjwa ya zinaa. Kadi 3 za madhara ya magonjwa ya zinaa ziwe za mwisho kabisa, na usisitize kwamba haiishii tu kwa magonjwa ya zinaa. Kuna hatari nyingi zaidi za kiafya zinazokuja pamoja na magonjwa haya ya zinaa.
6. Waelezee kundi kwamba huu mtandao wa madhara haya utarejelewa mara kwa mara kwenye hili somo.


Athari za kihisia



1. Kubadili misimamo
Ngono kabla ya ndoa haisababishi tu kujihisi duni bali pia hutufanya kupoteza msimamo wa sisi ni akina nani. Tendo hilo linatuondolea kushtakiwa na dhamira zetu. Kama vile vidole vyetu vinakuwa sugu baada ya kucheza na gitaa kwa muda mrefu na kutosikia maumivu. Tendo la ngono linakuwa ni jambo la kujitosheleza tu na bila kuhesabu gharama yake au kufikiria jinsi linavyoathiri watu wengine.
2. Majuto
Licha ya uhuru wa kijinsia ambao umeenea katika jumuiya ya leo, wasichana wengi huishia kutumaini mvulana waliyelala naye atapiga simu, hata kama walikubaliana kwamba ni ushirika wa usiku mmoja tu. Wavulana pia, wanakuwa na majuto, haswa wakati uhusiano mzuri unaharibiwa kwa sababu ya kushiriki ngono.
Hatia inaweza kutokea kwa kushtakiwa na dhamiri baada ya tendo la ngono; kwa wengine, inatokana na imani za dini yao. Hatia inakuja wakati mtu anatoa mimba ya haramu. Ingawaje anaweza kujiona kama kwamba ameepukana na majukumu mengi lakini, athari za muda mrefu za uavyaji mimba hujumuisha majuto na hatia ya muda mrefu. Hili litashughulikiwa kwa mapana zaidi baadaye.
3. Hofu
Jinsi tutakavyoona hakuna kinga yoyoye inayotoa kinga asilimia 100% . Daima kuna changamoto ya kupata mimba ama magonjwa ya zinaa. Hivyo kushiriki ngono kabla ya ndoa kunasababisha wasiwasi unaotokana na kutokuwa na hakika ya matokeo.
4. Hofu ya kuwajibika
Vijana ambao walisalitiwa baada ya kushiriki ngono katika uhusiano wa mwanzo si rahisi kuwaamini wengine katika uhusiano utakaofuata, wanaogopa kusalitiwa tena.
5. Kujihisi duni na kutojiheshimu
Aibu inaweza kutokea kutokana na hisia za kutumiwa, kuambukizwa magonjwa ya zinaa, kutenda kwa msukumo au kukubali shinikizo au majaribu.
Hata ngono ya mdomo inaweza kusababisha wasichana kupoteza heshima yao. Wasichana wengine hufikiri kwamba kuanzisha au kufanya ngono ya mdomo ni kumpa mvulana kile anachotaka huku akiepuka kupata mimba. Walakini ukweli kuhusu ngono ya mdomo unabaki:
Vijana wengi wanasema wanaota ndoto ya kuwa na ndoa yenye furaha siku moja. Jinsi gani ngono kabla ya ndoa huathiri ndoa vibaya?
Kwanza kunaweza kuwa na tabia ya kumlinganisha mwenzi wako na washirika wako wa zamani ambao mlitengana miaka mingi tu iliyopita. Wakati mwingine ni ile taswira tu na swala hilo linaweza athiri uhusiano wenu wa ngono katika ndoa.
Pili, kuna hatari ya kutokuwa mwaminifu katika uhusiano huo. Ikiwa hatukujifunza kukataa majaribu kabla ya ndoa, ni jinsi gani tunatarajia kuweza kukataa baada ya hapo?
Kushiriki ngono nje ya ndoa ni jambo linaweza sababisha uhusiano uliokuwa bora kuvunjika. Wakati lengo lililokuwa jema la kufahamiana linabadilika ghafla na kuwa ngono, vipengele vingine vya uhusiano vinaacha kuendelezwa na kukua. Hilo husababisha hisia hasi kutokea na uhusiano kuharibika.
Hisia hasi sio tu huathiri watu « wanaotambua hisia zao » bali hata wale wasiotambua. Watu wanaweza kuzikandamiza hisia kwa akili zao, lakini zinapata njia ya kujitokeza hatimaye kwa njia nyingine. Ukweli ni kwamba mwili wa mwanadamu una uwezo wa kuunda vifungo vya kihisia baina ya watu. Hilo hutokana na kemikali ya oxytocin, homoni hiyo inaongeza uhusiano wa kihisia baina ya watu wawili.
Kwa sababu oxytocin hutolewa bila kujali ikiwa ni ngono katika ndoa au tendo la usiku mmoja tu, hakuna kitu kama “ngono isiyo na masharti” - daima kutakuwa na uhusiano wa kihisia.
Kuna chaguo tatu::
Kuna Kuavya mimba kwa asili wakati mwanamke “anapoteza” mtoto. Kwa upande mwingine, utoaji mimba wa kuchagua, ni wakati mwanamke anachagua kutumia utaratibu ulio na madhumuni ya kuiondoa mimba.
Katika baadhi ya nchi, utoaji mimba unakuzwa kama njia halali ya kudhibiti uzazi.
Walakini, utoaji mimba hauwezi kuchukuliwa kama vile kuondoa uvimbe au saratani. Sio “tu” kuondolewa kwa “lundikizo la seli.” Ni kuyaondoa maisha ya mwanadamu, ambayo huja na athari kubwa kwa mama. Kutoa mimba sio tendo lisilo na hatari zake. Uavyaji mimba husababisha madhara ya kimwili na ya kihisia pia.
Mwanamke anapokuwa mja mzito ana uamuzi wa kuibeba mimba ile hadi atakapojifungua na kuchukua jukumu la kumlea mtoto wake peke yake, na baba wa mtoto, au kupata msaada kutoka kwa wazazi wake. Hata hivyo kuna mambo mengi ya kuzingatia wakati wa kufanya uamuzi huu, kwa mfano.
Vijana wanaweza kuwa wazazi wazuri ikiwa wako tayari kuvumilia kunakohitajika ili kumlea mtoto. Wanahitaji msaada mwema na wao kuwa wamekomaa kuchukua jukumu la kuwa wazazi. Kutenga vizuri muda wa masomo, kazi, na uzazi si jambo la kuchukuliwa kuwa la mzaha! Baadhi ya vijana hawako tayari kuacha uhuru wa ujana wakati wanapopata mtoto, wanaweza kusahau majukumu yao ya kila siku. Hivyo wanaweza kushindwa kuwa wazazi wazuri wanao fahamu majukumu yao.
Ikiwa hauko tayari kuwa mzazi katika hatua hii ya maisha yako, unaweza kufikiria chaguo la tatu kufanya mpango wa kuasili mtoto wako.
Kumtoa mtoto wako kwa wazazi wengine kumlea haimaanishi kwamba humpendi mtoto wako au kwamba unaepuka wajibu wako. Ukweli, inamaanisha kinyume kabisa—kwamba unataka mtoto wako aende kwenye familia iliyo bora zaidi iwezekanavyo, na kwamba unataka kuwajibika kwa maisha yako wewe mwenyewe pia.
Katika baadhi ya nchi, wazazi wa kibaolojia wanaweza kuchagua familia ya kuasili kwa ajili ya mtoto wao. Katika nchi nyingine, mashirika ya kuasili watoto huwachunguza wazazi wanaoweza kuwalea kulingana na vigezo vilivyofikiriwa kwa uangalifu ambavyo ni lazima wavitimize kabla ya mtoto kuwekwa katika familia hiyo.
Ukizungumza na shirika la kuasili haimaanishi kuwa unafanya uamuzi usioweza kutenduliwa. Inamaanisha tu kwamba unapata taarifa inayohitajika ili ufanye uamuzi bora. Baadhi ya maswali ya kuuliza wakala wa kuasili ni:
Hakuna majibu rahisi unapopata ujauzito ambao hukupangwa. Jipatie muda wa kutafakari ukweli wote na uchaguzi wote ili kufanya uamuzi bora kwa ajili yako na mtoto wako.


Kusaidia washiriki kuelewa kwamba kushughulikia mimba ya ujana kunahusisha kufanya uamuzi mzito kuhusu maisha ya mwanadamu mwingine.

1. Weka slaidi ya “Mtoto ambaye hajazaliwa”.

2. Anza kwa kumshika mtoto kwenye ngumi iliyofungwa au kumtoa mfukoni ili kueleza jinsi fetasi ilivyo ndogo karibu wiki 14. Walakini, katika kamwili haka kadogo:
Wiki ya 3
WIKI 11
3. Weka slaidi ya “Wiki ya 18” mshale kitengo ya wiki kumi na nane toa maelezo kwamba jinsia ya mtoto inaweza kutambulikana waziwazi.
4. Weka Slaidi ya “Wiki ya 22” onyesha mshale ule. Nywele zipo kichwani na mwilini na mtoto anaweza hisi maumivu. Kuanzia hatua hii hadi wiki ya 32, mtoto anahisi uchungu zaidi kuliko wakati mwingine wowote wa ukuaji wake.
5. Weka slaidi ya “Wiki ya 28”. Waambie washiriki kuwa ikiwa mtoto huyu atazaliwa basi
anaweza kuishi akitunzwa kwa uangalifu mkubwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi.
6. Wafamishe washiriki iwapo watachagua kushiriki vitendo vya ngono mapema wanajiweka katika hatari ya kupata mimba na ni bora wafanye maamuzi yaliyo bora kutokana na hilo. ULIZA: Je mimba ni swala la msichana tu? Inaathirije wavulana? Sio swala la msichana tu! Na wavulana wanashiriki pia jukumu linaloambatana na kumleta mtoto duniani na changamoto za kihisia zinazoambatana na uamuzi mkubwa namna hiyo.
Hata kama hutapata mimba, wakati wowote unaposhiriki tendo la ngono unakuwa hatarini kuambukizwa magonjwa ya zinaa. Ingawa baadhi ya maradhi haya ya zinaa yanaweza yakatibiwa iwapo yatagundulika mapema ,mengine hayana tiba na yanaweza kudhibitiwa tu.
Unaweza kweli? Je mmefahamiana kwa muda gani hata umwamini na maisha yako? Na unajuaje kwamba anasema kile anachojua unataka kusikia ili kusudi mshiriki ngono? Na iwapo anadai kwamba yeye angali bikira, kwamba anapendekeza kujamiiana nawe inapaswa kukufanya ujiulize kama hajawahi kumpatia mwingine ombi hilo.


Kuonyesha washiriki jinsi ukimwi unavyoathiri mwili wa mwanadamu.
1. Watu watakaojitolea sita kuigiza mchezo huo. Wape majukumu yafuatayo:
2. Wapange waigizaji ifaavyo:
3. Anza kukisimulia kikundi kwa mtiririko: “Huu ni Mwili wangu. (Onyesha Mwili wangu.)
Mwili wangu ni imara na una afya. (Mwili wangu unaruka juu na chini ukitutumia misuli yake kuonyesha nguvu na afya yake)
Mwili wangu unalindwa na mlinzi aitwaye WBC. (Elekeza kwa WBC, ambaye anarusha ngumi chache hewani.)
Sasa, WBC haimaanishi bondia wa kimataifa bali Chembe Nyeupe za Damu. Hizi ndizo hukinga Mwili wangu ili maradhi yoyote yasiupate. Wacha tuone kinachotokea wakati kikohozi kinaposhambulia Mwili wangu. (Kikohozi kinaukaribia Mwili wangu, kikikohoa kwa nguvu na Mwili wangu unaanza kukohoa pia. Lakini kikohozi kinapokaribia Mwili wangu, WBC anakuja kati yao na kuwatenganisha.)
WBC yu tayari kupigana na kikohozi. (WBC na Kikohozi wanaanza kupigana. Mwili wangu unaendelea kukohoa.) Mara WBC anamshinda Kikohozi ambaye anarudi nyuma. (Kikohozi kinatoka kwenye jukwaa . Mwili wangu unarukaruka na kujitanua tena.) Tumpigie WBC makofi. (pigeni makofi pamoja na watazamaji. WBC anapokea shangwe zile kwa heshima na kuinama.)
Sasa Homa inamvamia Mwili wangu. (Homa, inaukaribia Mwili wangu huku ikitetemeka.) Pengine ni homa ya malaria au homa ya matumbo. (Mwili wangu unaanza kutetemeka.) Lakini WBC yuko tayari kupigana na Homa. (Kwa mara nyingine, WBC anasimama baina ya Homa na Mwili wangu na kuwatenganisha.) Kunazuka vita … (WBC na Homa wanapigana. Mwili wangu unaendelea kutetemeka. WBC anaishinda Homa. (Homa inatoka kwenye jukwaa. Mwili wangu unaacha kutetemeka.) Ni shukrani kwa WBC, kwani Homa ilibidi iondoke kwenye Mwili wangu. Mwili wangu una nguvu na afya tena. (Mwili wangu unarukaruka ukitabasamu na kujitanua.) Tumpigie WBC makofi. (pigeni makofi pamoja na watazamaji. WBC anapokea shangwe zile kwa heshima na kuinama.)
Sasa Kuhara kunakuja kushambulia Mwili wangu. (Kuhara kunaukaribia Mwili wangu huku kuhara kunjishikilia tumbo lake kukilia kwa maumivu. Mwili wangu pia unaanza kulia kwa maumivu na kuinama ukijishikilia tumbo.) Lakini kwa mara nyingine WBC yu tayari kuulinda Mwili wangu. (Kwa mara nyingine, WBC anasimama baina ya Kuhara na Mwili wangu na kuwatenganisha.) Kuna zuka vita. (WBC na Kuhara wanapigana. Mwili wangu unaendelea kujishika tumbo na kulia kwa maumivu. (WBC anamshinda Kuhara. (Kuhara kunatoweka kwenye jukwaa. Mwili wangu unaacha kujishikilia tumbo na kulia kwa maumivu.) Kwa mara nyingine WBC ameulinda Mwili wangu. Shukrani kwa WBC, kwani Mwili wangu una nguvu na afya tena. (Mwili wangu unarukaruka ukijitanua kuonyesha afya yake nzuri.) Sasa tunaona jinsi WBC alivyo muhimu kwa Mwili wangu. Tumpigie WBC makofi. (pigeni makofi pamoja na watazamaji. WBC anapokea shangwe zile kwa heshima na kuinama.)
Lakini sasa Mwili wangu umepatwa na VVU, virusi visababishavyo UKIMWI. (VVU anaanza kuunyemelea Mwili wangu.) Pengine hii ilitokea kupitia ngono na mtu mwenye virusi au kutoka kwa damu ya mwenye virusi. (VVU anatoa tabasamu kubwa. WBC anaingia kati yake na Mwili wangu. Mwili wangu unaendelea kusimama hapo kana kwamba hakuna tatizo lolote.)
Wacha tuone kitakachotokea. (WBC na VVU wanaanza kupigana. Wakati huu, VVU anaonekana ndiye mpinzani mwenye nguvu zaidi ya WBC.) VVU anapigana na WBC kwa muda mrefu na kwa nguvu zaidi kuliko magonjwa mengine yalivyofanya. (WBC na VVU wanapigana kwa muda mrefu, lakini VVU anamshinda WBC. WBC anasalimu amri.)
Haiwezekani! VVU amemwangamiza WBC? (VVU anasimama kwa ushindi na kujitanua misuli. WBC anatingisha kichwa kwa huzuni na kusimama nyuma ya Mwili wangu huku akionyesha hadhira mgongo. Mwili wangu unaendelea kuonyesha kana kwamba hakuna kasoro yoyote.)
Mwili wangu hauonyeshi dalili zozote kwa wakati huu. Mwili wangu bado unaonekana kuwa mwenye nguvu na afya. (Mwili wangu unatabasamu na kujipongeza. VVU anasimama kando yake huku naye pia akitabasamu na kujipongeza.)
Baada ya muda mfupi tutaona kitakachotokea wakati Kikohozi kinapokuja kuushambulia Mwili wangu tena. (Kikohozi kinaukaribia Mwili wangu kikikohoa kwa nguvu. Mwili wangu unaanza kukohoa kwa nguvu pia. WBC anageuka, kuwaonyesha hadhira kuwa hana uwezo na kuupa Mwili wangu mgongo wake. VVU anasimama kwa maringo kando ya Mwili wangu. Kikohozi anashikana mikono na VVU kando ya Mwili wangu na VVU. Mwili wangu unazidi kukohoa kwa nguvu.)
Sasa Homa inarudi kuushambulia Mwili wangu. (Homa inamkaribia Mwili wangu ikitetemeka. Huku Mwili wangu, ukiendelea kukohoa, unaanza kutetemeka pia. WBC anageuka kwa sikitiko kuwaonyesha hadhira kuwa hana uwezo na kisha anageuka nyuma ya Mwili wangu. Homa inashikana mikono na VVU na inasimama kando ya Kikohozi. Mwili wangu unaendelea kukohoa na kutetemeka.)
Kuhara sasa kunashambulia Mwili wangu. (Kuhara kunaukaribia Mwili wangu, kukiinama kwa maumivu. Mwili wangu ukiendelea kukohoa nakutetemeka, unaanza kulalamika na kujishikilia tumbo. WBC anageuka, anatikisa kichwa na kurudi nyuma ya Mwili wangu. Kuhara kunashikana mikono na VVU na kusimama kando ya Homa. Mwili wangu unaendelea kukohoa, kutetemeka, kulia kwa maumivu na kujishika tumbo. VVU anaikunja mikono na kutabasamu.)
Mwili wangu, sasa ni mgonjwa sana una Kikohozi, Homa na Kuhara.
WBC hawezi kuusaidia na hivyo Mwili wangu unadhoofika zaidi. Sasa umepatwa na UKIMWI. (Mwili wangu, unaendelea kukohoa na kutetemeka pamoja na kulia kwa maumivu kisha unaanguka chini.)
Hatimaye, Mwili wangu unaaga dunia. (Mwili wangu unaanguka chini kwa njia ya kutatanisha. VVU anawashika mikono ya ushindi Homa, Kikohozi na Kuhara.)”

4. Waeleze dasara kuwa VVU husababisha UKIMWI na hivyo kusababisha chembe nyeupe za damu kudhoofika na kushindwa kupambana na magonjwa. Hatimaye magonjwa hayo humuua mtu asiye na kinga ya mwili.


Kuonyesha washiriki jinsi ukimwi unavyoathiri mwili wa mwanadamu.
1. Waeleze washiriki kwamba mtungi unawakilisha mwili wako, na tishu, kama seli zako nyeupe za damu (WBC).
2. Wakati Mafua, Kikohozi, Homa au Kuhara vinapojaribu kuingia kwenye mwili wetu (weka
mawe madogo kwenye tishu),
WBC italinda mwili wetu. Ingawa sisi ni wagonjwa, tutapona na
tutapona haraka.
3. Lakini VVU inapojaribu kuingia katika mwili wetu (kumwaga maji kwenye tishu), haishambuli mwili wetu mara moja, lakini inashambulia na kudhoofisha WBC yetu. Ndiyo maana mtu aliye na VVU anaweza kuonekana kuwa wa kawaida bila dalili.
4. Baada ya hayo, tunapoambukizwa na Mafua, Kikohozi, Homa au Kuhara, (weka mawe juu ya uso wa tishu zenye unyevu), zinaweza kuingia kwa urahisi katika mwili wetu kwa sababu WBC yetu imedhoofika. Wakati huu, hatuponi vizuri au haraka na hatimaye tunaweza kushindwa na magonjwa na maambukizo mabaya.
VVU hukua na kuwa UKIMWI, mfumo wa kinga ya mwili (chembe nyeupe za damu) hupoteza uwezo wake wa kupigana na magonjwa mengine na, hatimaye, magonjwa hayo mengine huua mwili usio na kinga.

Pengine ugonjwa wa zinaa unaoangamiza zaidi ni VVU/UKIMWI.

UKIMWI ni VVU?
UKIMWI ni nini?
VIRUSI vya UKIMWI VINASAMBAZWA VIPI? Virusi vya ukimwi vina sambazwa vinapoingia kwenye damu. Hii inaweza kutokea kupitia:
1. Majimaji ya uke ama shahawa
2. Damu
3. Mama hadi mwanawe
Nani yuko hatarini?
JE UKIMWI UNA TIBA? HAPANA!
VVU/UKIMWI kwa Hesabu


Kuwasaidia washiriki kuelewa jinsi virusi vya ukimwi vinavyoenezwa.

1. Weka slaidi ya “Salama au hatari?” na uwaambie washiriki kufungua vitabu vyao vya mazoezi.

2. Waombe washiriki kutathmini kama ni ‘hatari” au “salama’ kwenye zoezi lifuatalo (ikiwa muda hautoshi, chagua maswali machache tu)
3. Wanaweza kuonyesha chaguo lao kwa kunyoosha mikono yao ikiwa ni “Salama” na kutengeneza alama ya mkato kwa mikono yao ikiwa ni “Hatari” (kwa kipindi cha mtandaoni, wanaweza kutumia majibu ya “dole gumba” kama ni “Salama” na majibu ya “X” kama ni Hatari).
4. Kukumbatia mtu aliye na virusi
5. Kufanya ngono na mtu aliyeathirika.
6. Kula kwenye meza moja na mtu aliyeathirika.
7. Kulala nyumba moja na mtu aliyeathirika pasipo kujamiiana
7. Kushikana mikono na mtu aliyeathirika
8. Kulala nyumba moja na mtu aliyeathirika pasipo kujamiiana
9. Kumsaidia aliyeathirika kuingia ndani ya gari
10. Kula chakula kimoja.
11. Kutumia mswaki wake mtu aliayeathirika
12. Kusafisha matapishi ya mwenye virusi.
13. Kupigana busu na mtu aliye athirika
14. Mtu aliyeathirika anapokohoa ama kupiga chafya karibu nawe.
15. Kuogelea na mtu aliye athirika salama.
16. Kutumia wembe pamoja.
Matendo ya hatari kubwa
Matendo salama
VVU haisambazwi kwa njia ya:
Kamilisha “Mtihani wa Urafiki” mtandaoni kwa kiungo hiki kiungo hiki cha tathmini.


Kusaidia washiriki kuelewa ukweli kuhusu Virusi Vya Ukimwi (VVU)/Ukimwi.
Waambie washiriki wajibu maswali yafuatayo kama ni ukweli au ni hadithi.

1. Kufanya ngono na bikira utapona virusi vya Ukimwi.
2. Watu walio na virusi vya HIV wanaweza kuishi miaka mingi vila kufahamu hali zao.
3. Unaweza kuishi maisha mazuri ukiwa na HIV.
4. Virusi vya ukimwi/UKIMWI husambazwa kupitia mguso wa damu na kidonda cha mtu aliye na virusi.
5. Unaweza kupata virusi vya Ukimwi hata ukitumia kondomu.
6. Yeyote aliye na VVU/UKIMWI alipata kuutokana na kutokuwa mwaminifu katika ndoa.
7. Watu walio na VVU/ukimwi wanaweza ishi miaka mingi iwapo watakula vyema na kupokea matibabu.
8. VVU/Ukimwi hudhofisha mwili na maradhi kama malaria, kifua kikuu na pneumonia kumkumba mtu aliye athirika.
9. Mtu anayeonekana kama ana afya njema (hakuna dalili kudhibitisha huyu ana VVU) bado anaweza kuwaambukiza watu wengine.
Kamilisha “Mtihani wa Urafiki” mtandaoni kwa kiungo hiki kiungo hiki cha tathmini.


Kuwasaidia washiriki kutafakari jinsi VVU huathiri zaidi ya mtu mmoja.
1. Kwa kutumia nchi yako au kuchagua nchi yenye kiwango cha juu cha maambukizi ya VVU, jadili: Je, itakuwa na maana gani katika nchi wakati watu wengi wataambukizwa VVU na kufa kutokana na UKIMWI?
Andika athari hizi kwenye chati /ubao mweupe. Baadhi ya athari ni kama zifuatazo:
2. Wape muda kama kundi au kama mtu binafsi kuandika insha fupi, shahiri, au mabango kwa mada zifuatazo:
Jadili na uwasilishe
3. Wapatie muda wa dakika tano ili wawasilishe mawazo yao.

Kwa sababu mtu ana VVU haimaanishi kwamba tumtendee tofauti na vile tungemtendea mtu ambaye hana VVU. Kwa kweli, kuwa na uangalifu zaidi kunaweza kuonekana kama kumdhihaki au kumshusha. Kwa hivyo tunawezaje kuonyesha kuwajali watu walio na VVU?
Urafiki wako na watu walioathirika sio lazima ubadilike. Mtazamo wao haubadiliki, tabia na hekima yao bado ni ile ile, ni mtu yuleyule kabla ya wao kuwa na virusi vya ukimwi. Hakuna haja ya kumwepuka au kumbagua.


Washiriki waunde mpango wa kushughulikia janga la VVU/UKIMWI katika nchi mahususi duniani Wanaolengwa ni watu kati ya umri miaka 15 hadi 24 . Mpango ni pamoja na lengo la jinsi watakavyo endeleza kampeni hiyo na rasilimali watakayotumia kufanya hilo. Washauri kuwaza na kubuni mbinu bora.
Kuwasaidia washiriki kufahamu ni njia gani zilizopo ambazo hupunguza hatari ya kupata mimba na maradhi yanayotokana na ngono na kuwasaidia kutambua kwamba njia pekee ya uhakika ya kuepuka matokeo haya mi mpaka bora wa kutoshiriki ngono kabla ya ndoa.
Jinsi ilivyodhihirika katika vitengo vwa mwanzo, kujamiiana kabla ya ndoa kuna madhara mengi mengine yanaweza kuzuiliwa na mengine hayawezi. Madhara ya kihisia hayaepukiki, ya mwili baada ya tendo hilo yanaweza kuepukika, mbinu tofauti za ulinzi, hutoa viwango tofauti vya kupunguza hatari. Ni njia gani iliyo na dhamana bora zaidi? Kati ya mbinu hizo zote kutojiusisha na ngono kabla ya ndoa kunatoa ulinzi wa asilimia mia ya kinga.
Mwanafunzi bora mwenye umri wa miaka 23 alikataliwa na chuo kikuu cha hadhi kwa sababu alikuwa ameambukizwa VVU.
Baadaye alikubaliwa katika chuo kikuu kingine lakini kuna vikwazo kwa madarasa ambayo anaweza kuhudhuria. Alifanya ngono tangu akiwa na umri wa miaka 16, Timmy (si jina lake halisi) alijipatia ujuzi kuhusu “ngono salama”.
Alipogundua alikuwa ameambukizwa VVU, alimwambia daktari wake wa magonjwa ya akili, “Nilikuwa na wapenzi wachache tu wa ngono, na nilichukua tahadhari muhimu. Kwa nini mimi?”
Uliza:


Kuwasaidia washiriki kuelewa tofauti kati ya kupunguza hatari na uondoaji hatari kabisa.
1. Katika eneo lingine la ubao andika kishazi.

2. Waombe washiriki kupendekeza njia za kupunguza hatari. Wanapopaza sauti kutoa majibu yao, yaandike ubaoni. Majibu hayo yanaweza kuonekana kama hii picha ifuatayo:
3. Ikiwa kuna vitu vyovyote vilivyokosekana kwenye orodha, vipendekeze kwa kikundi na uviongeze kwenye ubao pia.
4. Baada ya kuorodhesha njia zote zinazowezekana, eleza kwamba utakuwa ukiangalia kila moja, ili waweze kufanya uamuzi sahihi kuhusu wapi wataweka mipaka yao linapokuja suala la ngono

Tanbihi: Hakikisha kuwa kutoshiriki ngono ni jambo la mwisho kujadiliwa kwenye wavuti ili uweze kusisitiza ujumbe wa kuondoa hatari ukilinganisha na kupunguza hatari kunakotolewa na njia nyingine zote za ulinzi.
Wape fursa wanaoshiriki kutoa maoni yao kwa yale ambayo tayari wanayajua .
Wezesha zoezi kwa kuuliza maswali ya kuongoza, kutoa taarifa zinazokosekana na kurekebisha dhana potofu.
Mafanikio ya zoezi hii yanategemea uwezo wa mwezeshaji kuwashirikisha washiriki bila kuwadharau au kunaswa katika kuwapatia taarifa nyingi kupita kiasi.

| MBINU YA KUJIKINGA | KIWANGO CHA KUTOFAULU KUPANGA UZAZI | KUJIKINGA NA MAGONJWA YA ZINAA |
| Vikinga Zinaa vya Mdomoni | Hakuna kinga dhidi ya kushika mimba | Hakuna kinga dhidi ya kushika mimba |
| Vififisha chembe-ume (manii) | 29% | Hakuna |
| Kutomwaga Manii kwenye Uke | 27% | Hakuna |
| Mipira ya kondomu ya wanawake | 21% | Haijulikani |
| Kiwambo-uke | 16% | Kuna idhibati ya kukinga ugonjwa |
| Mipira ya kondomu | 15% | HIV ≈ 80%
(ikitumiwa wakati wote) HPV = 70% Kisonono ≈ 50% Herpes ≈ 50% |
| Upangaji Uzazi wa Kawaida | 12-25% | Hakuna |
| Tembe za baada ya ngono/ Tembe za dharura | 11-25% | Hakuna |
| Tembe za kupanga uzazi | 8% | Hakuna |
| Vifaa vya kizazi (IUD) | <1% | Hakuna |
| Uhasiwaji | <1% | Hakuna |
| Kutoshiriki Ngono Kabla ya Ndoa | 0% | 100% |



Kusaidia washiriki kuelewa kondomu hupunguza hatari lakini haiondoi hatari kabisa.
1. Mpe kila mtu aliyejitolea puto, waeleze kwamba utakapo hesabu mpaka tatu, wanapaswa kupuliza puto yao haraka iwezekanavyo mpaka ifikie ukubwa wa vichwa vyao. Unaweza kutoa zawadi kwa yule atakayeijaza puto wa kwanza.
2. Puto iliyo na matundu inapaswa kushindwa kupanuka au kupasuka
3. Onyesha slaidi ya “Kondomu hutoa upunguzaji wa hatari kwa VVU kwa asilimia 80% pekee”..
4. Eleza kwamba kondomu 1 kati ya 5 haifanikiwi kwa sababu ya dosari za utengenezaji; ama inapasuka au inavuja.
5. Ongezea kwamba hata kwa matumizi kamili na sahihi kwa kila tendo la ngono, kondomu haiwezi kumlinda mtu kikamilifu dhidi ya VVU. Takwimu zinaonyesha kuwa hupunguza hatari kwa asilimia 80% tu.
Matumizi ya kondomu hayawezi kuhakikisha ulinzi wa asilimia 100% dhidi ya magonjwa yoyote ya zinaa.[97] Hata kwa “matumizi kamili,” bado kuna nafasi kwamba msichana anaweza kuwa mjamzito. Matumizi kamili yanafafanuliwa kuwa kutumiwa kila wakati (100% ya wakati) na yakiwa matumizi sahih.
Kulingana na shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), ufanisi wa kondomu kuzuia mimba unafikia asilimi 97%, kwa matumizi thabiti na sahihi.[98] Kwa matumizi ya kawaida, hata hivyo, ufanisi wa kondomu hushuka hadi kati ya 86 hadi 90%. [99] Ili kuhitimu kama matumizi thabiti na sahihi, watumiaji wa kondomu lazima wazitumie kwa kila tendo la ngono, na kufuata maagizo yaliyotolewa kwenye kisanduku (ambacho kwa kawaida huwa na takriban hatua saba). Kwa bahati mbaya, katika kusisimka kabla ya ngono, wachache wanachukua muda ili kuhakikisha kuwa wanaitumia kondomu kwa usahihi, au kila mara.
Uliza:
Je, unafikiri ni jambo la kweli au haki kutarajia vijana kutumia kondomu kikamilifu?
Mfano mwema ni mwanamke aliyepata mimba licha ya kutumia mpira wa kondomu:

Kuambatana na upungufu wa aina nyingine zote za kujikinga, je ni maamuzi yapi ambayo yatalinda hisia, mawazo na afya njema?

Chagua moja kati ya manne:
Watu ambao hawajachagua kutoshirikii ngono hadi ndoa inabidi kuelewa kuwa uamuzi wao unawawekwa katika kitengo kimoja kati ya viwili vifuatavyo:
Watu katika vikundi hivi viwili wapo katika hatari ya kuathirika kimwili na kisaikolojia, kwa kushiriki ngono nje ya ndoa. Madhara yanaweza kuwa kupata maradhi yanayotokana na ngono kama vile herpes, klamadia au VVU, kupata mimba ya haramu, kuavya mimba ama kuzaa, kuvunjika kwa uhusiano, na unyogovu.
Vijana wanahitaji kufahamu madhara ya tendo la ngono kabla ya ndoa yenyewe na hilo linaweza kuhatarisha maisha yao. Kwa asili ya ujana wao, vijana wengi wanaamini kwamba mimba au magonjwa ya zinaa hayawezi kuwapata wao. Wanahitaji kukumbushwa kuwa linaweza kuwakumba na kuathiri malengo na ndoto zao walizojiwekea kwa ajili ya maisha yae baadaye.
Uamuzi wako ni upi?
Kuwasaidia washiriki kufikiria kila hatua katika mchakato wa maamuzi kuhusu ngono na kuwatayarisha kupima matokeo ya kila chaguo wanalolifanya badala ya “kufurahia papo hapo” na kujutia matokeo yake ya baadaye.
Mshirikishi ahitimize somo hili kwa kusisitiza uwekaji mipaka kabla ya kushiriki ngono ili kujiepusha na majuto ya matokeo yasiyofaa


Kuwasaidia washiriki kuorodhesha faida na hasara za kushiriki ngono kabla ya ndoa.
1. Chora mchoro ufuatao kwenye ubao mweupe/chati mgeuzo
| KUSHIRIKI NGONO KABLA YA NDOA | NDIYO | HAPANA |
| FAIDA | ||
| HASARA |
2. Wahimize washiriki kupendekeza faida na hasara za kusema NDIYO kwa kushiriki ngono kabla ya ndoa, na pia kusema HAPANA kwa kushiriki ngono kabla ya ndoa.
3. Tathmini matokeo na kikundi, ili waelewe kanuni na pia kulimiliki suala hilo..
Majibu yanayowezekana:
| KUSHIRIKI NGONO KABLA YA NDOA | NDIYO | HAPANA |
| FAIDA | Kujisikia vizuri Kutopoteza urafiki Kila mtu anafanya | Kujistahi Kutopata magonjwa ya zinaa, mimba, wasiwasi, na majukumu yasiyo ya lazima |
| HASARA | Uwezekano wa kupata mimba Kuambuizwa/Magonjwa ya zinaa Kupoteza ubikira Majuto | Kupoteza urafiki Uwezekano wa kudhihakiwa |
4. Sehemu ya tabia njema ni kufanya maamuzi mazuri, kwa hivyo wasaidie washiriki kufanya uchaguzi mzuri kwa kutathmini matokeo ya uchaguzi wao na matokeo ya muda mfupi/mrefu wa maamuzi yao.
Kutojiridhisha papo hapo na kusubiri mpaka baadaye huleta thawabu kubwa zaidi kuliko kuyafurahia maisha wakati huu huu ambako kunaweza kuwa na majuto ya kudumu maishani mwako kote.
Eleza kwamba faida za kushiriki ngono kabla ya ndoa ni za muda mfupi lakini hasara zake ni za muda mrefu; na hasara za kutoshiriki ngono mpaka wakati wa ndoa ni za muda mfupi lakini faida zake ni za muda mrefu.
Kutoshiriki ngono sio tu kusema hapana. Kwa kweli, ni kusema ndiyo kwa mambo mengine mengi. Sio kizuizi lakini ukweli ni kwamba kunaruhusu vijana kuwa na uhuru mwingi wanaoutamani. Unavuna thawabu za kujidhibiti kingono
| KUSHIRIKI NGONO KABLA YA NDOA | NDIYO | HAPANA |
| FAIDA | MUDA MFUPI | MUDA MREFU |
| HASARA | MUDA MREFU | MUDA MFUPI |


Mipaka na uchaguzi wa uhuru wa kweli na usio na majuto
Badala ya kutuwekea vizuizi, mipaka hutupatia usalama wa kuwa watu halisi na kufurahia
mahusiano mazuri—na kuishi maisha ya “kutokuwa na majuto.”

Mzazi mpendwa,

Katika Sehemu ya 3 ya Hakuna Majuto, wanafunzi walijifunza kuhusu umuhimu wa kuweka mipaka inayofaa na matokeo ya kuvuka mipaka ya ngono.
Mada hii inawasaidia vijana kuelewa kwamba kuna changamoto katika kujenga mahusiano mema, lakini inawezekana kwa mtazamo na kanuni zenye afya, na kujifunza umuhimu na thamani ya kusubiri kushiriki ngono mpaka wakati wa ndoa.
Kuwasaidia washiriki kubainisha kati ya hisia za watu wa jinsia tofauti na kujifunza tofauti kati ya upendo, tamaa na kuvutiwa.
Neno upendo hutumika sana kwa ulegevu kwenye lugha ya Kiingereza, kwamba njia bora ya kufafanua upendo ni kueleza kile ambacho sio upendo. Hali ya kuwa kwenye “upendo”, ama kule kuvutiwa na mtu huenda ikawa ndio mwanzo wa uhusiano. Kuwa na hisia za mapenzi kwa mtu au kuvutiwa naye sio vibaya, ila hiyo peke yake haitatosha kuupitisha uhusiano kwenye wakati mgumu. Uaminifu na upendo wa kudumu unahitaji tabia nzuri – subira, heshima, uzingativu, ulinzi, ustawi, matumaini na uaminifu.
Wakati hisia ya kuvutiwa na mtu inapozidi kiasi, inaweza kuwa tamaa. Tamaa ni ubinafsi. Unapomtamani mtu unamchukulia mtu huyo kama chombo cha kutimizia haja zako kingono. Katika mchakato huu mzima hakuna hali ya kuzingatia maslahi ya mtu mwingine.


Wasaidie washiriki kutambua dhana sahihi ya upendo.
Wahimize washiriki kuorodhesha maneno au vishazi ambavyo vimetumika kufafanua au kuelezea upendo. Wawezeshaji waandike majibu ya washiriki kwenye ubao mweupe.
Baada ya zoezi, wawezeshaji watajadili na kuamua ni majibu gani ni maelezo ya upendo, tamaa au kuvutiwa tu kulingana na ufafanuzi wao.

Wawezeshaji wanaweza kuchora:
Watu ni wagumu na mahusiano yanaweza kuwa magumu. Tunapoanza kutambua na kuelewa tofauti kati ya upendo, tamaa na kuvutiwa, tunaweza kuanza kujenga msingi imara katikati ya utamaduni wa “kuunganisha” na kuendeleza mahusiano yenye maana na ya kudumu.


Wasaidie washiriki kutambua dhana sahihi ya upendo kupitia maoni ya watu wengi.

1. Cheza baadhi ya maonyesho kwenye filamu ama vipindi vya televisheni vinavyoonyesha sifa za upendo halisi.
2. Uliza:
Mnaonana kwenye chumba kilichojaa watu. Macho yenu yanakutana. Mioyo yenu inanyong’onyea. Mara moja “unafahamu”: Umempata yule uliyekuwa ukimtafuta.
Ni upendo wa “kuona kwa mara ya kwanza”… lakini kile tunachokiita “upendo wa kumwona mara ya kwanza” mara nyingi hugeuka kuwa “tamaa mara yakwanza.”
Mimi ndiye mlengwa, jinsi ninavyohisi na kile ninachotaka.
Kwa kweli, hizi sio hisia za upendo, bali ni msingi wa KUVUTIWA. MVUTO.
Upendo ni…
Upendo huvumilia na hufadhili.
Upendo hauhusudu, hautakabari, haujivuni au haukosi kuwa na adabu.
Upendo unajali wengine zaidi yako hautafuti mambo yake,
Upendo hautaki kile usichokuwa nacho,
Haujilazimishi kwa watu wengine, sio kila mara “mimi kwanza”.
Upendo hauoni uchungu,
na Hauhesabu mabaya.
Haufurahii udhalimu bali
Hufurahia ukweli unaposhinda.
Upendo haufi moyo, huvumilia yote, huamini yote,
hutumaini yote, hustahimili yote, hutafuta kilicho bora,
Upendo hauangalii yaliyo nyuma, haupungui neno wakati wowote.
Upendo haushindwi kamwe.
Kinyume na imani ya mwanadamu kuwa hitaji letu la msingi ni “kuingia” kwenye mapenzi, lakini kuchagua kumpenda mwengine na kupendwa kwa dhati-licha ya kutokamilika kwa mtu. Msingi wa aina hii wa upendo sio hisia tu, bali unahitaji juhudi na nidhamu.

Mapenzi ni kama mfuko imara ambao unaweza kuendelea kusimama hata usukumwe chini kwa nguvu kiasi gani kwa sababu ya msingi wake imara, unaolinganishwa na utunzaji, kujitolea, mawasiliano n.k. [sukuma begi la bop huku na huko].
Mapenzi ni kama mfuko imara ambao unaweza kuendelea kusimama hata usukumwe chini kwa nguvu kiasi gani kwa sababu ya msingi wake imara, unaolinganishwa na utunzaji, kujitolea, mawasiliano n.k. [sukuma begi la bop huku na huko.


Wasaidie vijana kutafakari kwa undani zaidi upendo wa kweli ni nini kwa kutafakari maswali haya. Unaweza kuwezesha na kujadili maswali haya.


Wasaidie washiriki kuelewa kuvutiwa tu au kupendezwa ni nini. [Mwezeshaji anaweza kutumia neno kuvutiwa tu au kupendezwa, kulingana na umuhimu wa kitamaduni]

1. Cheza klipu kutoka kwenye filamu za hivi majuzi au programu za televisheni zinazoonyesha vipengele vya mtu kuvutiwa au cheza video ya hivi majuzi ya muziki inayoonyesha vipengele vya kuvutiwa jumuisha maneno ya wimbo kwenye kitini au slaidi tofauti.
2. Uliza washiriki kuangalia muziki na kuchagua semi zenye maneno ya mapenzi. Watofautishe kuvutiwa (hisia) na upendo (chaguo).
Pia inajulikana kama kupendezwa, mara nyingi ni hisia zisizo halisi, za kupita kiasi au za msukumo wa kuvutiwa na mtu mwingine k.m, jinsi mtu anavyofanana, tabia zake pamoja na taswira yake. Kuvutiwa kunawezekana kukawa ni ishara za mwanzoni ambazo zinaweza kukua na kukomaa na hatimaye ukawa upendo uliokomaa na usio na masharti.

[Piga viputo kuelekea juu]
Angalia mapovu haya, je, si yanapendeza? Lakini je, yanadumu kwa muda mrefu? Ni nini kinachotokea ninapoyagusa? [gusa moja ya mapovu nalo litapasuka] Waeleze washiriki kwamba kuvutiwa na mtu ni kama kiputo hiki. Kunaweza kutokea haraka sana lakini hakukai muda mrefu kuvutiwa kunabadilika au kuisha kwa urahisi.
Nini kinatokea tukivutiwa na mtu?
Tunahisi hisia za ghafla mwilini
Tunaanza kubadili tabia
Unaanza kuwa na picha potovu/isiyo halisi kwa mtu huyo. Unapovutiwa na mtu wa jinsia tofauti, unaanza kujenga picha na mawazo ya kuwa mtu huyo ni mkamilifu-huoni upungufu wake!
Hisia hizo zinapanda zikishuka– zinapotea haraka kama zilivyokuja
Kufuatilia aliyekuvutia kwenye mitandao ya kijamii—kutakuumiza zaidi


Wasaidie washiriki kutofautisha kati ya upendo na kuvutiwa tu.
1. Kwenye bodi nyeupe, chora jedwali lenye laini mbili– moja lenye neno “Upendo” na nyingine “Kuvutiwa”.
2. Wajumuishe waliojitolea 12 (wawili wawili) na uwagawie kadi sita za majibu.
3. Wambie kuwa kila swali unaloweka ubaoni, litaelezea iwapo jibu ni upendo ama kuvutiwa.
4. Waambie wabandike kadi zenye majibu kwenye safuwima inayostahili na waeleze kwanini
majibu yanaangukia upendo ama kuvutiwa.
Baada ya maswali yote sita kujibiwa, hivi ndivyo jedwali lenye rangi nyeupe
linafaa kufanana:
| MVUTO | UPENDO |
| Nini ambacho hunivutia kwake zaidi? | Umbo la kuvutia, Kipaji/ujuzi | Hulka/ tabia |
| Wengine wana maoni gani kutuhusu? | Familia yangu na marafiki wa karibu hawataki uhusiano huu | Familia yangu marafki wa karibu wanaelewana naye |
| Mahaba yalianzaje? | Haraka (siku ama wiki); yalikuwa ni “mahaba Mara tu nilipomwona” | Baada ya kumfahamu kwa miezi/ miaka michache |
| Ninahisi vipi kumhusu? | Kuvutiwa kwangu kunabadilika kulingana na mudi Yangu | Kuvutiwa kwangu ni thabiti na kunaweza kubashiriwa |
| Mahaba yana athari gani kwangu? | Sijihisi, wakati mwingine natenda jambo ambalo si kawaida yangu | Mimi nafurahia hali yangu. Mimi ni mtu bora zaidi sasa. |
| Mtazamo wangu kwa jumla ni upi kuhusu uhusiano? | Namtarajia atoe; Ninahisi wivu haraka | Sote tunagawa na kutoa; nataka awe bora zaidi |
Mshirikishi anaweza kubadilisha maswali yaangazie umuhimu ama mambo ambayo hutokea kwenye kijiji/jumuiya yako kila mara.
Nini ambacho hunivutia kwake zaidi?
Wengine wana maoni gani kutuhusu?
Mahaba yalianzaje?
Ninahisi vipi kumhusu?
Mahaba yana athari gani kwangu?
Mtazamo wangu kwa jumla ni upi kuhusu uhusiano?
Kimsingi, mvuto hukua haraka na mara nyingi huzingatia vitu visivyo vya kudumu kama vile sura, uwezo na hata sauti ya mtu. Hukufanya ukatenda tofauti na jinsi wewe ulivyo kwa kawaida. Lakini jinsi mvuto unavyotokea kwa haraka ndivyo unavyopotea hivyo hivyo. Athari za kuvunjika kwa mahusiano hayo ya kuvutiwa hukaa kwa muda lakini baadaye hutoweka pia.
Upendo, kwa upande mwingine huchukua muda wa kuukuza na hukuzwa ninyi wawili mkichukua muda wa kufahamiana kwa kina. Unajifurahia nakujipenda unapokuwa na mwenzako na hata kumkubali mwenzako jinsi alivyo. Iwapo mwenza ataondoka kwa sababu yoyote, uchungu utakaotokea utakuwa mchungu na utachukua muda mrefu kupona kuliko inayotokea kwenye uhusiano wa kuvutiwa tu.
Mfano halisi wa tofauti kati ya upendo na kuvutiwakulingana na swali, “Mahaba yalianzaje”:


Wasaidie washiriki kuelewa ubaya wa tamaa.
Washa cheche za kumelemeta na uwaulize washiriki, “Nani anayetaka hizi?”
Tamaa ni kama mng’aro huu, (sisitiza kila neno) kali, inaleta shauku, ya kusisimua, ya kufurahisha, ya kuvutia, ya kustaajabisha, nzuri na ya kutamanika (isubiri iteketee). Lakini kama mng’aro huu, tamaa haidumu. Na mara inapoungua, inapoteza mvuto wake na kutupiliwa mbali.
Tamaa ya ngono inaweza ikaelezwa kuwa ni hamu kubwa sana ya msukumo wa mwili,na uchu wa kutaka kushiriki ngono. Kiasili ina ubinafsi na haizingatii hisia na maslahi ya mtu mwingine
Hatupaswi kuchanganya kuvutiwa kwa kawaida na tamaa.
Kuvutiwa kwa kawaida ni kitu cha asili. Wakati mtu mzuri anapopita na tunazingatia uzuri wake (jambo ambalo hutokea mara kwa mara), sio sawasawa na kumtamani mtu huyo.
Tamaa inahusisha uchaguzi na tendo la utashi. Kwa kiasi fulani ni uamuzi wa kukifuatilia kitu unachokitaka badala ya kukiachia kipite. Ni kujitoa kwa msukumo wa asili bila kujizuia.
Tunapoamua kujizuia na kutofuatilia huu msukumo wa ngono inaweza kuleta kukata tamaa.
Lakini habari njema ni kwamba kujidhibiti binafsi kunawezekana. Tunaweza kujifunza kuruhusu msisimko wetu wa hisia utupite bila kukita mizizi akilini na moyoni. Ni kama methali hii iliyoshirikiswa kwa muda mrefu: Huwezi kuwazuia ndege kuruka juu ya kichwa chako, lakini unaweza kuwazuia wasijenge kiota kwenye nywele zako. Hiyo ndiyo maana ya kuishinda tamaa. Itachukua kujitolea na mapambano, nidhamu, na kukua—haya yote ni hatua za kukomaa na kuwa mtu mzima.
Njia nyingine ya kushinda tamaa ni kumuona mtu huyo kuwa ni mtu wa thamani na wa kuheshimiwa. Badala ya kushawishiwa na tamaa, mtazame mtu huyo ukitabasamu kama rafiki, ugeuke na kuondoka. Jifunze kushiriki katika urafiki wenye maana na mazungumzo bora na watu wa jinsia tofauti.
Tunaweza kushinda tamaa kwa kutomtazama mtu kama kitu cha kutumika bali kumpenda kwa usahihi - wa thamani na wa kuthaminiwa.
Je, unatumika kukidhi haja za ngono za mwenzako au umenaswa katika uhusiano wa unyanyasaji?
Ikiwa ni hivyo, tafadhali wasiliana na mshauri wa shule ama mtu mzima mwaminifu akusaidie ili
uondoke kwenye uhusiano huo
Ni muhimu kukiri wakati mtu amevuka mipaka yako. Uhusiano mzuri ni ule ambao msingi wake ni wa urafiki, heshima na thamani. Zungumza na sauti yako isikike.
Tazama maudhui juu ya Alama za Uhusiano Usiofaa hapa chini.

Kwa Wawezeshaji:
Ukipata swali linalohusiana na unyanyasaji au ubakaji:
Kukabiliana na madai ya unyanyasaji na ubakaji kwa kijana ina ugumu lakini ni lazima lichukuliwe kwa uzito na kushughulikiwa kwa uangalifu na haki.
MAMBO AMBAYO USIFANYE:
Ripoti madai ya unyanyasaji shuleni au kwa mfanyakazi wa kijamii aliyeteuliwa.


Hakuna mkataba – huwezi kushiriki ngono kupata upendo, na kushiriki ngono hakumaanishi kuwa unampenda mtu huyo.
Kimsingi, kuna dhana kuwa wasichana hushiriki ngono na wanaume iliwa wapendwe. Wavulana kwa upande mwingine hukidhi hisia/upendo wa msichana ili washiriki ngono naye.
Huenda ikawa ni kati ya tatu tulizozitaja – upendo, kuvutiwa, ama tamaa. Kama kijana, ni asili kuwa na mvuto kwa mwenzako – sio makosa. Lakini hizo hisia hazipashwi kukuthibiti na kuamua matendo yako.

Hivyo basi kua ukomae ili uweze kutenda yale ambayo yana manufaa kwako na kwa wengine.
Je Unatambua tofauti?
| UPENDO | INFATUATION | TAMAA |
| Ni... | kujitoa | hisia | hamu |
| Hujengeka... | Baada ya muda | haraka na kutoweka | haraka |
| Huthamini... | Utu, tabia | Anavyopendeza, talanta | binafsi |
| Msingi wake... | ukweli | udanganyifu | msukumo |
| Huzingatia... | “WEWE” | “MIMI’ | “MIMI’ |
Kuwawezesha washiriki kujifunza njia za kuwasiliana kiafya na watu wa jinsia tofauti bila kuingia katika hali za kutatanisha.
Shukrani kwa mitandao ya kijamii, kutuma ujumbe mfupi na kukutana kwa kirafiki mtandaoni, teknolojia mpya imefafanua kwa upya jinsi tunavyowasiliana, ambayo ni sehemu kubwa ya uhusiano, kulingana na Kevin Carr, mwandishi mahiri, mzungumzaji na mtangazaji wa Television. https://www.youtube.com/watch?v=70HdOIiWfe4
Hamu ya matokeo ya papo hapo na kujiridhisha papo hapo haitusaidii kuungana vyema katika uhusiano wa maana. Hata kwa maendeleo ya teknolojia ya kisasa yenye chaguo na fursa zisizo na kikomo, hatuwezi kuepuka hamu yetu ya uhusiano wa kina na wa maana na ushirika.
Kuwa na uhusiano na kubarizi kwa mvulana/msichana kumekuwa na umaarufu na kunakubalika miongoni mwa vijana. Kwa sababu ya hili, shinikizo ni kwa vijana kujitosa kwenye uhusiano huu wa mvulana-msichana.
Ingawa uhusiano huu unaweza kuonekana kuwa mzuri, shinikizo ambalo vijana hukabiliana nalo ikiwa ni mtu kutoka shuleni kwao, ikiwa wataachana, kulingana na marafiki waliowazunguka, inatia aibu wao kukutana na mpenzi wao wa zamani kila siku - na hii inaweza kuwa mateso kiakili na kuchosha. Hii inaweza kuwa sababu kwa nini vijana zaidi wanageukia uhusiano wa mtandaoni.
Shinikizo lingine ni kwamba ni rahisi kuingia katika hali zenye kuleta maelewano au kuwa katika “hali”.
Hali hii (wakati mwingine pia inajulikana kama “urafiki-husiano”), ambapo watu wawili ni zaidi ya marafiki. Wanaweza kuwa wanakaa muda mwingi pamoja na wanaweza hata kuwa na upendo wa kimwili lakini wanahisi kuwa hawajajitoa kama marafiki hasa. Wanaweza kuwekezwa katika uhusiano fulani wa kihisia lakini bila kujitoa. Mpangilio huu unaweza kuwa mchungu na wa utata kwa angalau mmoja wa wahusika.
Shinikizo la vijana kuunganishwa vizuri katika jambo hili la mvulana-msichana sio lazima liwe gumu. Kunaweza kuwa na mwingiliano mzuri na wa maana kati ya wavulana na wasichana bila kuingia katika hali za utata.


Kuwa katika uhusiano kumebadilika sana; itafaa kuwauliza washiriki jinsi wanavyoifafanua ili kuelewa mtazamo na mawazo yao.


Wasaidie washiriki kuelewa hatua za uhusiano na faida za kuendelea polepole. Sio mbio, ni marathoni..
1. Onyesha washiriki slaidi ya “Hatua za Uhusiano”.
2. Wakusanye washiriki katika vikundi vidogo kwa ajili ya majadiliano au wahimize kutoa majibu yao kwa sauti.
3. Uliza: Ni vipengele gani muhimu unavyohitaji kwa kila hatua ya uhusiano?
4. Baada ya washiriki kujibu, wawezeshaji wanaweza kutoa mawazo yao kwa kila kategoria yenye maudhui yafuatayo..

Rejelea mahusiano yote kati ya mvulana na msichana kwenye soma la 3 – urafiki wa juu juu, urafiki wa karibu, kuvutiwa, uhusiano thabiti na kisha ndoa.
Hatua ya 1: Urafiki

Hatua ya 2: Burudani na jinsia tofauti
Hatua ya 3: uhusiano thabiti/uchumba
Hatua ya 4: Ndoa
Mfano halisi wa kuendelea kutoka urafiki kufikia ndoa:


Kulingana na Scott Stanley, Ph.D. na Galena Rhoades, Ph.D. katika ripoti iliyoitwa “Kabla Sijaamua Kuoana” iliyofadhiliwa na Mradi wa Kitaifa wa Ndoa katika Chuo Kikuu cha Virginia, kizazi kimoja au viwili vilivyopita, watu waliunda uhusiano na kufanya ahadi tofauti na wanavyofanya leo. Wakati huo, wapenzi walikusudia na kuamua kufunga ndoa, kuishi pamoja, na kuzaa watoto.
Leo, kulingana na Stanley na Rhoades, ndoa inafikiriwa mwishoni. Takriban asilimia 90 ya wapenzi hushiriki ngono kabla ya ndoa, kulingana na utafiti mmoja, na takriban watoto wanne kati ya kumi huzaliwa na wazazi ambao hawajafunga ndoa. Wapenzi wengi huishi pamoja kabla ya kufunga ndoa.
Baada ya kuchunguza zaidi ya wapenzi elfu moja Waamerika, Stanley na Rhoades walifikia mkataa muhimu:
Wapenzi wengine huendelea na mahusiano bila kufanya maamuzi maalum yoyote, wakati wapenzi wengine hufanya maamuzi kwa makusudi kupitia hatua mbalimbali za mahusiano. Wanandoa katika kategoria ya mwisho wanafanikiwa zaidi katika mahusiano yao.
Wasiofanya maamuzi maalumu yoyote, mmoja au wote wawili wanajikuta wanakubali kuoana kwa sababu inaonekana kama hatua inayofuata “ya kimantiki”.
Kujitoa ni muhimu. Kulingana na Dk. John Gottman: Ni kuhusu kuonyesha kupitia maneno na matendo yako kwamba uko katika uhusiano kwa hali zote kwa mema na mabaya, na kwamba mnaweza kutegemeana.
Kama Mtaalamu aliyeidhinishwa Gottman Zach Brittle anavyosema, “Kujitoa ni juu ya chaguo. Na sio tu kuchagua mwenzi wako, bali pia ni kuchagua uhusiano siku baada ya siku.
Bila kujitoa, wapenzi huanza kukuza chuki kwa kile wanachofikiri kinakosekana katika uhusiano wao badala ya kuwa na shukrani kwa kile walicho nacho.
Ikiwa una wasiwasi kuwa unaweza kuingia kwenye ndoa bila kuamua, hapa kuna maswali matano ya kujadili na mwenzako kuhusu nia ya uhusiano wenu.
Kuishi pamoja ni wazo baya kwa sababu huondoa msingi inayojenga uhusiano imara, ndoa na familia.
[Angalia maudhui zaidi juu ya Kuishi Pamoja hapa chini]
Ufafanuzi mpana, ni wakati watu wawili wa jinsia tofauti wanafurahia shughuli za jumuiya, kwa mfano, kutazama filamu, kwenda ufukweni, n.k. Kwa ufafanuzi wake haimaanishi uhusiano “mzito”. Vijana wengi wanatafuta mtu ambaye anawapenda jinsi walivyo, mtu ambaye wanaweza kushiriki naye mawazo na hisia zao.
Sio burudani na mtu wa jinsia tofauti zote ni za mahaba, lakini zinaweza kusababisha mapenzi. Kwa kweli, burudani nyingi huanza bila mahaba, lakini uhusiano unapoendelea, zinakuwa za kimapenzi. Sio lazima tayari kuwa katika uhusiano thabiti ili kuwa na burudani.
Burudani thabiti huleta matarajio. Ikiwa mnakutana mara kwa mara, k.m., kila Alhamisi jioni baada ya darasa ili mpate chakula cha jioni na kuzungumza kuhusu maisha, inajenga matarajio ya kukutana kila Alhamisi. Ukiamua kwa ghafla kufanya mipango mingine siku ya Alhamisi, utamwacha mwenzako akijiuliza, Je! nilifanya jambo baya?
Burudani pamoja inaweza kuwa na afya ikiwa tutajifunza jinsi ya kuweka mipaka iliyo wazi (ya kimwili na ya kihisia). Tatizo huanza wakati vijana wanaingia katika eneo lisilo na mwelekeo (kimwili na kihisia) na hali ya uhusiano inaanza kuwachanganyikia. Mara nyingi hutokea wakati vitendo na tabia zinatangulia kabla ya kujitoa kwa kila mmoja.
Kwa mfano, marafiki wa karibu wanaoanza kushikana mikono au kukaribiana kimwili, mmoja anaweza kutoka burudani akifikiri kuna mengi zaidi kwenye urafiki huu huku mwingine akiwa amependa tu hisia za “ukaribu.” Matokeo yake mara nyingi ni mmoja au pande zote mbili kuumia.
Burudani na jinsia tofauti haitakuletea ukamilifu. Ni vyema kutoshiriki burudani na mtu wa jinsia tofauti ukiwa shule ya secondari au chuo kikuu na kufurahia kuwa na marafiki na wewe kuwa rafiki mzuri. Hakuna njia ya uchawi ya kuchumbiana. Kutokengeushwa wakati wa ujana wako kunaweza kukusaidia kuepuka maumivu ya moyo ya uhusiano wa kimapenzi, ambayo kwa umri huo mara nyingi hayaendi popote na hayafiki mbali.
Dhibiti teknolojia yako. Mitandao ya kijamii, kutuma SMS na simu yako mahiri hurahisisha maisha na mawasiliano ya papo hapo kupatikana kwa urahisi lakini haiwezi kuchukua nafasi ya muunganisho na uhusiano wa maisha halisi. Ni jukumu letu kutumia zana hizi za ajabu za kiteknolojia kwa busara ili kuimarisha na kujenga uhusiano wetu kupitia njia tofauti za mawasiliano.
Ni jambo la kawaida kudhania kuwa mazungumzo ya mtandaoni yanavutia zaidi kuliko maingiliano ya ana kwa ana, lakini hakuna kibadala cha kutumia muda halisi pamoja. Pata usawa mzuri wa wakati kati ya maisha ya mtandao na halisi.
Waombe washiriki kuangazia madhumuni ya burudani baina ya jinsia tofauti kabla ya kufichua majibu hapa chini:
Kuchagua kwa hekima “wakati gani” na “ni nani” kwenda burudani naye kunaweza kumaanisha kwamba utalazimika kukataa baadhi ya mialiko. Kukataliwa kunaweza kuwa kuchungu sana ikiwa hakukufanyika vizuri. Wakati mvulana anapomuomba msichana kwenda burudani naye (au msichana kumuomba mvulana), yeye sio tu kumwomba atoke naye; pia anamjulisha kuwa anampenda. Anauweka wazi moyo wake. Ikiwa msichana atakataa tu na kuondoka bila kusema chochote, anabaki na swali la “kwa nini?” Bila kupewa sababu inayofaa, anaweza kufikiria, bila shaka mimi si mzuri wa uso ya kutosha, sina haiba ya kutosha, au sikumuomba kwa usahihi. Kwa maneno mengine, anafikiria amekataliwa kwa sababu ya jinsi alivyo, wakati inaweza kuwa ni kwa sababu msichana hayuko tayari kuwa kwenye uhusiano. Je tunawezaje kusema hapana tunapoombwa kwenda burudani bila kumuumiza mtu?
Waombe washiriki watoe mapendekezo ya kukataa mwaliko wa kwenda burudani bila kumuumiza mtu moyo.
Mahusiano ya zamani – Namna ya kukabili matengano?
Ikiwa unamjua mtu aliyevunjika moyo, uwe na huruma, kwa sababu msaada wa kijamii umeonekana kuwa muhimu katika kupona. Na uwe na subira, kwa sababu itachukua muda mrefu zaidi kwa rafiki yako kupona na kuendelea na maisha kuliko vile unavyofikiria.

Katika uhusiano wowote, kuna baadhi ya tabia mbaya, ambazo zinaweza kutatuliwa, lakini ikiwa zinaanza kuunda muundo usio bora, hupaswi kuishi na hasi.

Binafsi: Tabia hizi za uharibifu huleta tu madhara kwako kwa muda mrefu, kwa mfano.:
Mtu binafsi: Wakati mwingine sifa za uharibifu hujitokeza wakati mtu anapohusiana na wengine, kama vile:

Kimsingi, chagua mtu anayekuheshimu na kukupenda! Chagua mtu asiyepuuza maoni yako, asiyekugandamiza mbele ya wegine, asiyepuuza hisia zako, au kukushinikiza kufanya kitu ambacho hutaki kufanya (pamoja na kushiriki ngono).
Kusaidia washiriki kuelewa utamu wa ngono na wakati mwema wa kushiriki ngono ni kwenye ndoa.
Vyombo vya habari vinaweza kutuambia kuwa ngono ya mapema ni sehemu ya asili ya kujitosa kwenye mapenzi; thamani ya ubikira na usafi vinaonekana kama utamaduni wa zamani na umepitwa na wakati. Lakini tunaona ngono ya mapema inawaacha wakiwa wapweke wakikata tamaa ya kupata upendo wa kweli. Ukweli ni kuwa burudani ya jinsia tofauti huridhisha wakati ambapo hakuna ushirikiano wa ngono maana kunakuwa hakuna matatizo ya kihisia yanayotokana na kushiriki ngono kabla ya ndoa.
Waeleze washiriki kuwa ujinsia wetu ni kama gundi (shughuli ya awali katika Sura ya 3: Karatasi ya Rangi).

...katika ndoa.
Ngono inakusudiwa kuwaunganisha watu pamoja. Hatuwezi kuchagua ikiwa kila tendo la ngono litawaunganisha washirika. Tendo la ngono haliwezi kuondolewa kutoka kwenye madhumuni yake ya kuunganisha. Kutumia kipande cha mkanda wa gundi ambacho kilishatumika, kunasababisha kupoteza kunata kwake. Kwa njia hiyo hiyo, ngono kabla ya ndoa hutufanya tupoteze uwezo wetu wa kuunganishwa siku zijazo.
Wapenzi wanaosubiri kushiriki ngono hadi ndoa wanafurahia:

Waulize washiriki kama moto ni mzuri au mbaya [wengi watajibu kuwa ni mzuri na pia ni mbaya]
Moto unaweza kuwa jambo zuri sana kwa sababu unaweza kututia moto au kupika chakula kitamu kwa ajili yetu. Lakini pia unaweza kuwa jambo baya sana. Unaweza kuchoma na kuharibu nyumba na misitu ikiwa hauko ndani ya mipaka iliyo salama.
Moto katika shimo la kuchoma nyama/mekoni (mipaka) ni mwema—lakini unapoutoa nje ya mahali pake, unaweza kutudhuru.
Tamaa ya ngono ni kama moto. . . ambayo inaweza kuwaka vizuri mekoni pake ambako ni kwenye ndoa.

Ni kuhusu kusema “NDIO!” Kwa uhuru! [wakumbushe washiriki Kitengo cha 3 Faneli ya Maisha]
Sote tunapenda wazo la kuwa huru, haswa vijana. Kutoshiriki ngono kunaruhusu vijana uhuru wa kukua na kufarahia mahusiano, bila kuwa na wasiwasi wa kukabiliwa na athari za ngono kabla ya ndoa.
"Unapompenda mtu, utamfanyia yaliyo mema pekee,”
– Tim Stafford
Nitajuaje iwapo yeye ndiye sahihi?
Unajua ikiwa wewe na yule unayempenda mmesimama mbele ya marafiki na familia na kuahidi kuoana na kuishi kwenye ndoa siku zote za maisha yenu.
Anayefaa kwa ngono ni yule utakayemuoa.
Kuna wakati mwema unaokwenda sambamba na moyo, akili na mwili wakati unaposema “Nakubali”siku yako ya ndoa Wakati ufaao wa ngono na mahaba ni siku ya ndoa.
Ngono imelengewa ndoa.
Inaweza tu kutendwa na mtu mmoja ambaye ameahidi kujitoa kwako maisha yako yote.
Kusubiri ni ishara ya upendo wa kweli na uvumilivu. Mtu yeyote anaweza kusema. Ninakupenda,” lakini sio kila mtu anaweza kusubiri na kuthibitisha kuwa ni kweli.


Kutambulisha kwa washiriki dhana sawa ya ndoa.
1. Wambie washiriki kuwa unaposoma taarifa kuhusu ndoa, fikiri kuhusu zile ambazo ni za kweli ama za uongo?

2. Kwa kila taarifa, washiriki wainue kadi za kijani iwapo wanafikiri kuwa taarifa ni ya kweli na kadi ya njano ikiwa ni uongo.

Ndoa ni kitu cha kudumu, ngono hufanyika kati ya mume na mke ambao wamejitoa na kila mmoja wao anamjali mwenzake.
Katika ndoa tunachagua :
kupenda bila kujali…
Upendo ni uamuzi. Ndoa ni ahadi.
Pia kuna wapenzi ambao huona kwamba wazo la ndoa halina maana, halihitajiki, ni kandamizi na la zamani. Badala yake, wanachagua kuishi pamoja na kupata uzoefu wa kuwa na ukaribu na mtu, lakini bila kujitoa kwake. Wao huwa na hisia kwamba upendo ni kuhusu kuwa “katika wakati huu,” na kwamba ili kufurahia mahusiano ni kuishi dakika kwa dakika. Hata hivyo, mara tu wakati unapoisha na hawahisi tena kwamba mtu huyo ni “sahihi”, wanaondoka kwenye mpango huo na kwenda kwa mtu mwingine. Hakuna msingi wa kujitoa kwa mwenzao katika uhusiano wa namna hiyo, ni dhaifu kabisa.
Kuishi pamoja kunahusisha mpangilio unaozingatia kile ninachotaka, na kile ambacho ni bora au kinachofaa mimi. Makubaliano hayo ni kama haya: “Unaweza kunitumia mradi tu uniruhusu na mimi nikutumie.” “Niko tayari kukuruhusu unitumie kama bidhaa, mradi tu unaniruhusu nikuchukulie kama bidhaa pia.” Lakini haya ni makubaliano ya uongo. Tunaweza kusema mwanzoni kwamba tunakubali kuwa “tuko wagumu kama chuma,” lakini hakuna mtu anayeweza kuahidi kwa hakika kwamba hakutakuwa na hisia za majuto ikiwa uhusiano huo utaharibika.
Tofauti na ndoa, wapenzi wanaoishi pamoja hujizoeza kutojitoa kikamilifu katika maisha yao ya “pamoja”. Wanaweza kuhisi hofu mara nyingi, wakishangaa kama wenzi wao kwa namna fulani watachukua fursa ya kuathirika kwao. Kwa hivyo, kuna uwezekano wa kuwa na mguu mmoja nje ya mlango, katika muda wote wa mpangilio huu.

Ukweli ni kwamba kuishi pamoja kunaweza kuwatenganisha. [Hii haimaanishi kwamba kila wapenzi wanaoishi pamoja kabla ya ndoa watapata mambo yafuatayo; wala hatusemi kwamba kutoishi pamoja kunahakikisha uthabiti. Hata hivyo tunachunguza mitindo na data kwa ujumla, na inaonyesha matokeo haya.]
Utafiti unaonyesha wapenzi wanaoishi pamoja:
Unaweza ukawa unajua kinyume cha hayo hapo juu, lakini utafiti huu unaonyesha matokeo yanayowezekana mkiishi pamoja. Je, uko tayari kucheza kamari kwa matumaini kwamba unaweza kuwa mmoja wa walio tofauti?
Kuwasaidia washiriki kuelewa maana ya kutoshiriki ngono na thamani ya kuwa safi zaidi ya usafi wa mwili tu.
Wengi wamebisha kuwa kutoshiriki ngono hakuwezekani kwa vijana. Lakini je, ni kitu ambacho hakiwezekani? Cha muhimu kwenye suala hili ni kutambua thamani ya mtu, kujenga tabia nzuri ya kufanya maamuzi mema, na thamani ya ngono katika uhusiano wa maisha wa ndoa.
Kutoka kwa hatua ya utafiti, kusubiri kushiriki ngono hadi wakati wa ndoa kuna faida. Hata hivyo, tunapaswa kukumbuka kwamba ujinsia unahusisha mambo mapana zaidi (na ya kina) zaidi ya kubaki tu safi au kushiriki ngono au la; inahusisha utambulisho wako, kujistahi, hisia yako ya kuwa na mtu anayekuthamini kipekee na hamu ya ukaribu na mtu huyo. Tunapaswa kwenda ndani zaidi ya kuwafundisha vijana wetu sio tu “kusema hapana,” ila kuwasaidia kufuatia ukamilifu, mahusiano yenye afya, na yenye ukaribu.
Mwandishi na mzungumzaji mashuhuri Dk. Juli Slattery anatukumbusha kwamba ukaribu ni zaidi ya ngono ya kimwili—ni hisia ya kujulikana, kuthaminiwa, na kupendwa.
Tunaishi katika ulimwengu unaohujumu uhusiano wa karibu katika kila hatua huku wakikuza ngono kama mbadala wa kutosha. Hakuna kiasi cha ngono (halisi au ya kichwani) kinaweza kufidia ukosefu wa ukaribu.
Vijana wetu wanaweza kuolewa au kutoolewa mbeleni, lakini bado wanaweza kuwa na mahusiano ya ukaribu na ya maana yaliyo ya kina kirefu. Tunahitaji kuwasaidia vijana wetu kuelekeza hamu yao ya urafiki wa karibu kwa njia zinazofaa.
Zaidi ya hayo, mapambano ya kukaa safi hayaishi siku ya sherehe ya harusi. Usafi wa kijinsia ni vita katika maisha yote ya watu wazima. Inachukua sura tofauti tu katika ndoa.


Wasaidie washiriki kukiri thamani ya usafi.
1. Waombe washiriki waonyeshe au waeleze kitu ambacho ni cha thamani sana kwao.
2. Mara tu wanapofichua kipengee chao, waulize washiriki wachache kwa nini wanafikiri kitu hiki ni cha thamani kwao.
3. Waulize wanafanya nini ili kukitunza, kukilinda na kukihifadhi. (Wana mipaka gani ili kukilinda?)
4. Baada ya hayo, wawezeshaji wanaweza kutoa mfano wa kibinafsi wa kile ambacho ni cha thamani kwao na kile wanachofanya ili kukilinda na kukihifadhi. Kwa mfano, unaweka vitu vyako vya thamani kwenye sefu (mipaka) ambayo inakusudiwa kulinda kile unachokithamini.
USAFI pia ni kitu chenye thamani na thamani kubwa. Je, tutaweka mipaka gani ili kuutunza, kuulinda na kuuhifadhi?
Kufuatia usafi ni kutafuta utimilifu kama mtu

Fuata usafi na KICHWA chako
Fuata usafi kwa MOYO wako
Fuata usafi na MKONO wako
NDIYO MAANA NI WA THAMANI SANA


Kusaidia washiriki kuimarisha sababu za kutoshiriki ngono na kuwa wasafi kwa kuwa na mtazamo wa “muda mrefu ujao” na “picha kubwa”.
1. Waombe washiriki kuandika barua kwa wana wao watarajiwa wa kiume/kike wakijumuisha hoja zifuatazo:
2. Kisha washiriki watie saini mwisho wa barua “Mama” ama “Baba” – sio majina yao.
Shiriki mfano halisi wa kile ambacho wewe (mwezeshaji) ungemtakia mwanao. Yaweza kuwa kwa njia ya kusoma barua ulioandika kwa mwanao unayemtarajia.


Kuwasaidia washiriki kujua kwamba ngono ya mapema kwenye mahusiano hututawanya na huchukua muda kuponywa ama kurejelea hali ya kawaida, LAKINI tunaweza kuanza upya tena.

1. Gawanya washiriki kwa makundi madogo ya washiriki 6-7.
2. Pitisha picha kwa kila kikundi. Inamisha picha hiyo (uso chini).
3. Agiza kila mtu kwenye kikundi akate sehemu ya picha hiyo na kuipitisha kwa mwenzake, picha hiyo ikiinamishwa wakati wote.
4. Changanyaa vipande vya picha hiyo ikiwa bado imeinamishwa.
5. Onyesha slaidi ya “iliyochanika” na uelezee kuwa kila mara tunaposhiriki ngono, tunawapatia sehemu yetu – kiakili, kijamiii, kimwili na hata kitabaka– kwa kila uhusiano mpya. Kila uhusiano unapokwisha, mshikamano unavunjika. Hisia zinazozunguka “kuvunjika” mara nyingi ni mseto –wakati mwingine kuna maumivu makali kuona umeachwa, wakati mwingine tunaona nafuu na hata mara nyingine kukasirika. Hii inaitwa “mizigo mizee” ambayo tunaileta kwenye ndoa, na kusababisha kutoaminiana, kuogopa tutaachwa, hofu ya hisia za uchungu, magonjwa ya zinaa – mambo mengi ambayo huleta msongo kwenye ndoa. Hata hivyo mtu ambaye amekuwa akishiriki ngono kwa muda anaweza kuamua kuacha na kuanza tena. Anaweza kujithibiti na kutoshiriki ngono hadi wakati wa ndoa.
6. Washiriki waweke sehemu zilizokatwa (zikiinamishwa) pamoja kwa kutumia gundi. Wakishakamilisha wazigeuze. Washiriki watagundua kuwa kuna mapengo kwenye picha hiyo.
7. Onyesha picha “iliyogundishwa pamoja” na uelezee mapengo yanawakilisha majeraha ama alama ambayo zinasalia – athari za kihisia, kisaikolojia ama kiroho (na wakati mwingine kimwili) . Vipande hivyo vipo, lakini vinahitaji uangalifu na umakinifu kuviweka pamoja. Inawezekana kujifunza tena kujiamini na tabia zenye afya njema katika mahusiano.

Washiriki ambao wamekuwa wakishiriki ngono wanahitaji kufahamu kuwa inawezekana kuacha na kupata uthabiti wa kujitoa kutoshiriki ngono hadi siku ya ndoa. Kurejelea uthabiti baada ya kushiriki ngono ya mapema sio rahisi haswa wakati vijana wako bado kwenye uhusiano ambao ndipo waliposhiriki ngono. Uamuzi wa kudunisha kutoshiriki unahitaji kuvunjilia mbali uhusiano huo ili kupata uthabiti na kupata muda wa kufanikisha malengo yako.
Iwapo ungependa kupata uthabiti na usishiriki ngono hadi siku ya ndoa, unafaa kufuata hatua hizi. Hatua:
Baadhi yenu mnaweza kujiona kuwa ni wa ajabu au wa kuchosha na mmekosa furaha zote. Lakini hiyo ni hadithi.
Ukweli ni kwamba muda uliosubiri SIO wakati ulioupoteza.

Ni wakati ambapo:
Kupitia kusubiri unajitayarisha, unajiweka katika nafasi nzuri, na unaishi kadiri ya kusudi lako la kipekee!
Unaposubiri weka nia na kuishi ukifuata kusudi lako la kipekee.

Kutoshiriki ngono kuna maana ya kujitenga; kuepuka. Sio kama vile njia nyingine za kujikinga, kutoshiriki sio jambo analoweza kukushauri daktari ama unaweza kununua. Njia hii ya uzazi wa mpango, ikiwa itaitwa hivyo, inaleta kinga asilimia 100.
Na ni hakikisho la kuepuka mimba zisizohitajika, maradhi ya zinaa na miseto ya hisia. Hata hivyo ili kudumisha uamuzi huo, washiriki wanafaa kutafuta makundi ambayo yana mawazo sawa na hayo yatakayowaunga mkono na pia kuwahimiza.
Kutoshiriki ngono hadi siku ya ndoa, ni uamuzi ambao mtu huchukua na kuepuka vitendo vyote vya ngono hadi siku ya ndoa. Inajumuisha kufanya uamuzi wa kuepuka hali zote za ngono, ya mdomoni, ya mkunduni, kutomasana, na kupiga punyeto kwani huamsha hisia zetu za ngono na kuharibu usafi wetu.
Ngono ni zaidi ya kitendo chenyewe. Inahusisha pia shughuli nyingine ambazo zinatangulia kabla ya tendo lenyewe. Tunafaa kuchora mipaka kabla ya kujikuta tumesisimka na uchu.
Sio tu kuhusu “La” – hakuna picha za ngono, hakuna busu, hakuna ngono, nk. Kwa kweli unasema “Ndio” unapojithibiti na kuamua kuweka mipaka. Kutoshiriki ngono ni kujithibiti na kufanya maamuzi ya afya na ya busara.
Ni wito wako. Unathibiti vipi maisha yako ya ngono kwenye ujana wako na miongo inayokuja? Kufahamu athari za kushiriki ngono kabla ya ndoa hakutakusaidia iwapo hutafanya uamuzi kuzihusu.
Uamuzi kuhusu ngono na mahusiano sio wa kubahatisha. Uamuzi wako leo utaathiri maisha yako ya baadaye.
Kutoa changamoto kwa washiriki kuchagua uamuzi wa kutoshiri ngono/kuwa safi hadi ndoa.
Awamu hii ni ya muhimu sana kwa warsha hii. Yote uliyoyasema na kuyafanya kabla ya kiwango hiki, yanalenga kujenga mazingira mazuri ambapo washiriki wanapewa fursa ya kufanya uamuzi.
Washiriki sasa wanapashwa kuelewa ya kutosha ama kufahamu kuhusu athari za ngono ya mapema ili wafanye uamuzi wa busara, jinsi wanavyotaka kuishi maisha yao na kufanya mahusiano yao
Ni muhimu uwaelekeze washiriki kutumia ufahamu wao kufanya maamuzi wakizangatia kile walichojifunza. Kumbuka kushirikisha mioyo na akili zao ili uamuzi wa kutoshiriki ngono ufanywe kwa moyo wote wala sio kwa sababu ya hisia, shinikizo au kwa huzuni.


Kuwahimiza washiriki kuahidi kuwa wasafi na kutoshiriki ngono kabla ya ndoa
1. Elezea kuwa kufahamu athari za ngono ya mapema hakutakuwa na maana iwapo mshiriki hatafanya uamuzi. Wahimize wajitolee kufanya ahadi hiyo LEO.
2. Elezea kuwa kadi hizo zitawahimiza kuthamini malengo na ndoto zao kwa kutoshiriki ngono hadi siku ya ndoa. Wakati mwingine ni rahisi kuwajibika tukinakili ahadi zetu kwenye daftari na kuahidi uaminifu wetu kwa kuandika majina na kutia sahihi. Kutia saini kadi hizo kunamaanisha kuwa haijalishi maisha uliokuwa ukiishi, kuanzia leo unaahidi kutoshiriki vitendo vya ngono ama tabia hatarishi zitakazo athiri usafi wako.

3. Anza kushiriki hadithi yako (muziki wa chini kwa chini utasaidia) Ukielezea safari yako na kujitolea kwa usafi. Lengo ni kuwachochea wanafunzi kuwa na mtazamo wa kuona usafi kuwa zawadi kuu ambayo ni ya thamani.
4. Washiriki wasome kwa sauti kwenye kadi zao: hii inaashirikia kujitolea kwangu, familia yangu, mwenza wangu na wana wangu wa siku za usoni kutoshiriki ngono kuanzia leo hadi siku nitakayofungua ndoa.
5. Watie changamoto washiriki kujitolea kutoshiriki hadi siku ya ndoa. Wambie wachukue zile kadi na kuzitia saini. Kisha watafute shahidi atakayetia saini pia. Shahidi huyo anafaa kuwa mtu mzima wa kuaminika, mzazi ama mwelekezi [sio rafiki ambaye anakabiliwa na changamoto hizohizo za maisha] ambaye atawawajibisha na kuwaunga mkono katika uamuzi wao.
6. Wakumbushe washiriki kwamba kufuata usafi si tu kuhusu kutoshiriki ngono kabla ya ndoa—ni kuhusu kufuata utimilifu kama mtu. Thamani ya kweli ya chaguo lao haipo katika malipo ya ndoa bora na ngono katika siku zijazo, lakini malezi ya sifa chanya za tabia, kujithamini na utambulisho ambao utawapa uwezo wa kusema hapana kwa ushawishi mbaya, tabia hatari na ndio, hata. ngono kabla ya ndoa. Usafi wa kijinsia unatokana na ufahamu wa kina ya kwamba wewe ni nani—Mtu wa kipekee—kama mwanamume au mwanamke—mkamilifu, wa thamani, na sifa za kipekee, aliyeumbwa kwa ajili ya mahusiano yenye afya.
7. Malizia warsha kwa kuwathibitisha washiriki juu ya thamani na ujasiri wao katika kuweka msimamo. Ikiwa muda unaruhusu, washiriki waulize maswali.


Kuacha kufanya ngono ni hatua muhimu ya kwanza ya kuwafundisha vijana wetu kuhusu kujamiiana kwa afya. Sio tu kusema hapana kwa ngono kabla ya ndoa. Inatokana na kuelewa kwamba muundo asilia wa ngono ni katika muktadha wa ndoa na kujaribia nje ya mipaka ya ndoa huleta matokeo mabaya.
Utamaduni wa sasa umedhamiria kupotoka kutoka kwa muundo huu wa asili kwa kufanya kile kinachohisi vizuri na sawa.
Shinikizo la ndani na nje ambalo vijana wetu wanakabiliwa nalo linahitaji zaidi ya elimu ya kujiepusha tu shuleni na ndani ya jamii. Vile vile, ahadi yenye nguvu ya usafi inaweza kuwa ishara ya nje ya kujitolea kuacha ngono, lakini vijana wetu lazima wapatiwe picha kamili ya ujinsia.
Tunahitaji kufanya kazi pamoja kama wazazi, washauri, shule, jumuiya, mashirika ya kidini, n.k., ili tusafiri pamoja na vijana wetu.
Tunahitaji kwenda zaidi ya usafi wa kijinsia hadi utimilifu wa kijinsia, tukiwasaidia vijana KUISHI MAISHA WAKIWA WAZIMA, BILA MAJUTO.

Mzazi mpendwa,
Katika Kitengo cha Hakuna Majuto® 4, wanafunzi walijifunza kuhusu umuhimu wa mahusiano mazuri na thamani ya kungoja hadi ndoa ili kufanya ngono.
Kwa madhumuni ya maswali ya majadiliano, fasili za upendo usio na masharti, tamaa na mvuto vilivyotumika katika Sura ya 4 ni kama vifuatavyo:

Maswali: