Archive Page

Miongoni mwa mambo mengi ambayo vijana wanakabiliwa nayo leo, kufanya uamuzi kuhusu suala la ngono ni muhimu sana. Utamaduni wa leo umejaa picha za ngono, jumbe mbaya na ushauri mbaya kuhusu ngono. Vijana waliobaleghe na kuvunja ungo wanakua kwenye mazingira ambayo yana jumbe tofauti.

Hakuna Majuto ni mpango ulioanzishiwa na Focus on Family ® - shirika la kimataifa na lisilo la kibiashara. Mpango huu unahusu masuala ya ngono unaolenga kuwafundisha vijana kutoshiriki ngono hadi wakati wa ndoa. Lengo kuu la mpango huu ni kuwashauri vijana kuwa uamuzi wa kutoshiriki ngono kabla ya ndoa ni chaguo la busara, lililo la usalama na lenye kulinda afya ya mwili.

Kutoshiriki ngono kabla ya ndoa ni hatua ya kwanza ya muhimu ya kuwafundisha vijana juu ya ubora wa kujamiiana. Sio tu kusema hapana kwa ngono kabla ya ndoa, bali lengo letu ni kuwasaidia vijana kuelimika kuhusu swala hilo la ngono. Elimu ya ngono ni uwezo unaohitaji maarifa, uongozi na utendaji, ukifanya uamuzi wa kupata taarifa sahihi zinazosaidia kufanya uchaguzi wa busara kuhusu ngono na mahusiano bora. Ni pamoja na kujitambua na kujithibiti, ukiwa na uwezo wa kujiwekea mipaka yako binafsi kimwili na kihisia, kuwaelewa jinsia tofauti na wewe, na athari zako kwa watu wengine. Kuweza kujieleza kijinsia kwa njia inayofaa kimaendeleo na nyeti, ukijali utamaduni bila kuathiri malengo yako ya kibinafsi au maadili ya familia.

Tangu mwaka 1996, mipango ya Focus on the Family inayolenga kutoshiriki ngono kabla ya ndoa imetekelezwa kwa yamkini mataifa 70 kwa zaidi ya lugha 35 na kufikia jumla ya wanafunzi milioni 3.8 kati yao asilimia 84 wakiahidi kutoshiriki ngono kabla ya ndoa ulimwenguni kote.

Hakuna Majuto® inafundisha kanuni zifuatazo:

Whether you are conducting No Apologies as a 2-hour talk, 4-hour workshop, or 2-day camp, you can expect dynamic presentations, interactive discussions, and age-appropriate examples in this engaging, fun, and informative program. The extra material and background reading have been included to ensure that you are properly equipped to confidently deliver the program.